Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,279
- 120,689
Wanabodi,
Anza na hii clip
View: https://youtu.be/lBC3xKODSvY?si=9RxFyI43cF6ff0og
Anza na hii clip
View: https://youtu.be/lBC3xKODSvY?si=9RxFyI43cF6ff0og
- Kufanya kosa, sii kosa, kosa kurudia kosa, nchi yetu ya Tanzania, tuko hapa tulipo, kwasababu tumefanya makosa mengi tuu ya kisiasa, ya kiuchumi na ya kijamii, ambapo baadhi ya makosa hayo, ni makosa ya kijinga tuu kwasababu ya ujinga wetu!. Tulikuwa ni wajinga, kwasababu tulikuwa hatujui!. Sasa tumeelimika, tumeerevuka, ujinga umetutoka, sio wajinga tena!. Swali ni, pamoja na werevu wetu wote huu, kwanini bado tunataka kurudia ujinga ule ule tena?!, kwa kufanya kosa lili lile tulilolifanya wakati ule tulipokuwa wajinga?!. Mjinga ukimuelimisha, ujinga unamtoka, anageuka mwerevu, anaerevuka, ila mjinga ambae hata baada ya kumuelimisha, na bado anaendelea kuwa mjinga kwa kufanya ujinga, hii maana yake ni ujinga haujamtoka!. Mjinga wa aina hii, anakuwa sio mjinga!, huyu ni ... (naomba nisimalizie). Msikilize Baba wa Taifa
View: https://youtu.be/4AWaU_8FYhQ?si=ZeZk_294GlwUP3bK - Kosa la muswada fulani wa ujinga ulifanywa na serikali yetu na Bunge letu lilolopita, na ukathibitika ni ujinga kwasababu ya ubatili. Kitendo cha Serikali yetu ya sasa, imepeleka tena Bungeni muswada wa mabadiliko ya sheria ya uchaguzi, yenye ubatili ule ule ulioshabatilishwa na mahakama, huku kutakuwa ni kurudia kosa, hivyo hili ni bandiko elimishi la kuelimisha kuwa japo huko nyuma tulifanya makosa, kufanya makosa kule sii kosa kwasababu tulikuwa hatujui, lakini kurudia kosa ndio kosa!. Sheria ya Uchunguzi iliyopo sasa ni kosa!, tumeleta muswada wa sheria wenye kosa lile lile !. Kwanini tunataka kurudia kosa?!.
- Kosa la sheria hiyo ni ubatili unaotokana na kunyima na kuminya haki zilitolewa na ibara ya 5 ya katiba, haki ya kupiga kura, na ibara ya 21 ya katiba, haki ya kupigiwa kura. Niliwahi kusema humu kuhusu Asante Rais Samia kwa kuwasisitiza watendaji wa vyombo vya haki kuwa haki sio hisani, bali ni stahiki. Watende haki, tubadili Katiba kurudisha haki tunaomba Bunge letu, litutendee haki!
- Ujinga ninao uzungumzia hapa ni ujinga fulani wa kisheria uliotokana na serIkali yetu kutunga muswada batili, uliaokwenda kinyume cha katiba ya JMT ya mwaka 1977, Bunge letu likaitunga hiyo sheria batili ikawa sheria, mahakama ikaitengua kuwa ni batili, serikali ikakata rufaa kupinga uamuzi wa mahakama, ikashindwa, serikali ikaichukua hiyo sheria batili, ikapeleka Bungeni kwa muswada wa kufanya mabadiliko ya katiba kwa hati ya dharura, ikaichukua sheria ile batili na ikaichomekea kwenye katiba, na kweli Bunge likafanya mabadiliko ya katiba, na kuichomekea batili ile ndani ya katiba yetu kiubatili!. Batili hiyo mpaka hivi ninapoandika hapa, bado ipo kwenye katiba yetu na kwenye sheria zetu. Hili ni kosa kubwa ambalo Bunge letu limetukosea Watanzania na limetutendea Watanzania!. Niliuliza humu Katiba Yetu Ina Matobo: Serikali Ikikosea, Inashitakika. Je, Bunge na Mahakama Zinapowakosea Watanzania Kama Makosa Haya Tunawashitaki Wapi?, kosa hilo sasa linataka kurudiwa kwenye huu muswada wa sheria mpya ya uchaguzi.
- Mihimili yetu yote mitatu, ya Serikali, Bunge na Mahakama, inaongozwa na binadamu na sio malaika, hivyo binadamu hawa wanaweza kufanya makosa na kukosea, kwenye sheria hii iliyopo ya uchaguzi, Serikali, Bunge na Mahakama, zimetukosea sana Watanzania Sheria ya Uchaguzi ni mbovu! Kuendelea kuitumia sio Ujinga? Kuwabebesha masikini gharama za Uchaguzi sio Dhambi?
- Sheria ya uchaguzi iliyopo inayokwenda kubadilishwa, ina makosa fulani ya kikatiba, na kisheria, yaliyopelekea sheria hiyo kuwa na ubatili Fulani. Hili nimelizungumza sana humu!.
- Kwa vile ubatili wenyewe, ulikuja kuchomekewa kwenye katiba yetu, kiubatili, hii sheria mpya tunayoijadili, leo, nayo inauendeleza ubatili ule ule!, swali ni kwanini tutunge sheria mpya batili yenye ubatili ule ule, ulioshabatilishwa na Mahakama Kuu ya Tanzania?!.
- Katiba ndio sheria mama, sheria nyingine yoyote inayokinzana na katiba ni sheria batili. Kutafsiri ya kifungu hiki, anayebatilisha sheria batili inayokwenda kinyume cha katiba ni katiba yenyewe ya JMT, na sio serikali iliyotunga ubatili huo!, sio Bunge lililopitisha ubatili huo, na wala sio Mahakama iliyoutamka na kuithibisha ubatili huo!. Hili nimeliendeshea darasa kabisa humu. Ijue Katiba kwa Jicho la Mtunga Katiba: Mtunga Katiba alimaanisha nini aliposema "Katiba ni Sheria Mama"? Ni kweli Katiba ni Sheria Mama?
- Mihimili ya Serikali na Mhimili wa Bunge ndio ilihusika na ubatili huu, Mhimili wa Mahakama ndio iliotimiza wajibu wake kwa kuutangaza ubatili huo, mpaka hapa ninapozungumza, ubatili huo, licha ya kubatilishwa na mahakama, mahakama ya rufaa, ililirudisha jukumu la kuondoa ubatili huo, kwenye mhimili wa Bunge.
- Anayebatilisha ubatili wowote wa sheria yoyote batili inayokwenda kinyume cha katiba, ni katiba yenyewe na sio mahakama, kazi ya mahakama ni kuthibitisha tuu ubatili, tangu mahakama inapouthibitisha ubatili huu, hapo hapo sheria hiyo inakuwa imebatilika!, swali ni licha ya kujua sheria hii ina ubatili, kwanini tulete sheria mpya yenye ubatili ule ule?!.
- Kama Serikali ilitunga muswada batili, Bunge likatunga sheria batili, Mahakama ikaudhobitisha ubatili huo na kuutangaza ubatili huu, serikali ikafanya mabadiliko ya katiba kwa hati ya dharura, na kuuchomeka ubatili ule ndani ya katiba yetu kiubatili, sheria hii ya uchaguzi tunayoijadili leo, bado inao huu ubatili, kwanini serikali na Bunge waliuchomekea ubatili huu ndani ya katiba yetu?!. Nimewahi kuuliza humu, Watanzania tutaendelea kusubiri mpaka lini Bunge likitunga Sheria batili na kuuchomekea ubatili huo ndani ya Katiba yetu? Tufanye nini?
- Kama mwanzo tulifanya kosa, la kutunga sheria batili, Rais Wetu Samia, ameikuta batili hiyo, kwa vile yeye sio mwanasheria, wasaidizi wake ambao ni wanasheria wabobezi na wabobevu hawajamwambia Rais Samia kuwa sheria hii ni batili!, kwa vile mimi mwenyewe Paskali Mayalla, ninathibitisha nia njema, safi na ya dhati, ya Rais Samia, na dhima na dhamira ya kweli na ya dhati, kuwatendea haki Watanzania, kwa vile Rais Samia sio mwanasheria, she is not part and parcel ya ubatili huu unaoendelea sasa kwenye sheria hii mpya Madudu ya ajabu ya ubatili wa Katiba yetu, mabadiliko "fake" ya sheria na Tume ya Uchaguzi, Rais Samia asilaumiwe kwasababu yeye sio mwanasheria!. hivyo kupewa maua yake ni halali yake!.
Hitimisho
sasa ili kutimiza azma njema yenye dhamira safi kwa kauli na matendo, kwa hili tuu, naomba Rais Samia apewe maua yake!, na nimeisha mpongeza sana kwa hili, ila pia nilimpa angalizo Hongera Sana Rais Samia kwa Miaka Miwili Madarakani. Japo Umefanya Mengi, Makubwa, Mazuri, Lakini Bado! Linalowezekana Leo, Lisingoje Kesho!
Ombi, ili kuitimiza nia njema ya rais Samia, serikali ilete kwanza mabadiliko madogo ya katiba kwa hati ya dharura, kuuondoa huo ubatili, ndipo tuendelee kutunga sheria hii. Mabadiliko ya Sheria Bila Mabadiliko ya Katiba,Sawa na Kula Bila Kunawa!. Je Watanzania Tuna Haraka Sana na Uchaguzi Hadi Tukimbilie Kula Bila Kunawa?
Namalizia kwa kusisitiza, tulifanya makosa huko nyuma, kufanya kosa wakati hujui sii kosa, kosa ni kurudia kosa wakati tayari umeisha jua ni kosa!.
Kwanini tunataka kurudia kosa kwenye hii sheria?.
Paskali