Kuelekea Sikukuu, TRC yaongeza safari za treni kuelekea mikoa ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,713
13,464
ONGEZEKO SAFARI ZA TRENI NA NAULI

Dar es Salaam, Tarehe 07 Disemba 2024.

Shirika la Reli Tanzania - TRC linauarifu umma kuwa kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka, kutakuwa na ongezeko la safari za treni kuelekea mikoa ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha.

Siku ya Jumatano itaongezeka kujumuisha siku za Jumatatu na Ijumaa hivyo kufanya jumla ya safari tatu kwa juma kuelekea mikoa hiyo.

Ongezeko hilo la siku ya Jumatano ni hatua mahususi za TRC kukabiliana na ongezeko la abiria katika kipindi hiki hususani kuelekea mikoa ya Kaskazini Mashariki mwa Tanzania.

Katika hatua nyingine kila siku ya Jumatatu ya juma kuanzia Desemba 09, 2024 mpaka mwanzoni Januari 2025 Shirika litakuwa likipeleka mabehewa kumi na nane (18) yatakayobeba abiria takribani elfu moja (1,000) mpaka elfu moja na Mia mbili (1,200) kwa wakati mmoja kuelekea mikoa hiyo.

Wakati huo huo Shirika la Reli Tanzania, linawahakikishia wananchi kwamba hakutakuwa na ongezeko la nauli katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka hivyo nauli zitasalia kama zilivyo sasa.

Nauli ya shilingi elfu kumi na sita na mia tano (16,500) daraja la tatu (3), shilingi elfu ishirini na tatu (23,000) daraja la pili kukaa na shilingi elfu thelathini na tisa na Mia moja (39,100) daraja la pili kulala kulala kwenda Moshi, zitasalia hivyo.

Aidha, nauli ya elfu kumi na nane na Mia saba (18,700) daraja la tatu, shilingi elfu ishirini na sita na mia saba (26,700) daraja la pili kukaa na shilingi elfu arobaini na nne na mia nne (44,400) daraja la pili kulala kwenda Arusha, zitasalia hivyo.
Shirika linawakaribisha wananchi wote kwa usafiri wa uhakika na salama.

Fredy Mwanjala
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano
IMG-20241207-WA0106.jpg
 
Back
Top Bottom