CHARLES MGANDA JOHN
Member
- Aug 5, 2019
- 42
- 77
KUELEKEA SIKU YA AFYA YA AKILI DUNIANI
POMBE NA AFYA YA AKILI
Kila ifikapo tarehe 10 ya mwezi wa 10 kila mwaka, dunia huadhimisha siku ya afya ya akili duniani.
Nikiwa kama mdau wa Afya ya akili, naomba nichangie kwenye eneo moja kwanza la Pombe na Afya ya akili kwa sasa!
Kwa kifupi sana ni kwamba, wataalamu wa masuala ya kisaikolojia na afya wanakubaliana kuwa unywaji pombe kiholela una madhara makubwa kimwili, kihisia na kisaikolojia, afya ya akili ikiwemo!
Kuna madhara ya muda mfupi na yale ya muda mrefu!
Mathalani, Msongo, sonona na kujiua ni miongoni mwa athali za wazi zitokanazo na unywaji pombe kiholela!
Tafti zingine zinathibisha kuwa unywaji wa pombe unapelekea kupoteza kumbukumbu (memory loss) Kuona vitu visivyokuwepo (hallucination) kukosa usingizi mnono, na kuelewa ndivyo sivyo!
Mbali na kuathili ubongo, madhara mengine ya pombe ni pamoja na kutoka jasho jingi, kutetemeka mikono, miguu kukosa nguvu nk!
Madhara ya muda nrefu ambayo yamethibitishwa kuchangiwa na pombe ni pamoja na Kiharusi (stroke), Ugonjwa wa ini, saratani ya utumbo (bowel cancer), saratani ya ziwa (breast cancer) saratani yam domo (mouth cancer) na tatizo katika kongojo (Pancreatitis)
MBALI NA SAIKOLOJIA NA AFYA, UFALME WA MUNGU UNAITAZAMA POMBE KWA JICHO HILI!
Nimekuwa nikiulizwa maswali kadhaa juu ya Suala la matumizi ya POMBE katika Ufalme wa Mungu!
Hapa Nazungumzia pombe Kama pombe yaan ile Yenye kilevi yaan hii
CnH2n+1OH
Ni wazi yamekuwepo mabishano kwa muda mrefu, kwa watu wa dini kuhusu pombe,
kundi moja linaitetea, kuihifadhi na kuilinda pombe Kama katiba waliyoapa kuilinda. huku kundi jingine linaizodoa, kuisakama, kuisimanga na kuhitimisha kuwa Ni dhambi.
UKWELI NI UPI? SOMA KWA UTULIVU.
Bila kupoteza muda ninukuu hivi!
Marko 7:15 "Hakuna kitu kilicho nje ya mtu ambacho kikimwingia chaweza kumtia unajisi, Bali vile vimtokavyo, ndivyo vimtiavyo unajisi yule mtu."
Ndiyo kabisa! Kwa habari ya unajisi huwezi kunajisika! Na ndiyo maana hata Mimi siwezi kukuhukumu kwa suala la chakula na vinywaji! Kwa Maana aliyezaliwa mara ya pili hawi Chini ya maagizo na makatazo ya Hapa na pale yasiyokuwa kwa jinsi ya Kristo.
Hapa Mtume Paulo anasema
Wakolosai 2:16 "Basi Mtu asiwahukumu Ninyi katika vyakula au VINYWAJI au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi au sabato."
Tena kwa asili kabisa Hakuna kitu najisi hata kimoja (Warumi 14:14)
Kumbuka baada ya uumbaji kukamilika, Mungu aliviona vyote Ni vyema na vya kupendeza, hakuona unajisi! (Mwanzo 1:25)
KAMA NI HIVYO, JE POMBE NI SAWA?
Ufunuo wa wazi wa kibiblia unamtaka mtu aliyezaliwa Mara ya pili, aishi kwa kutumia Akili zake vizuri na ipasavyo!
1kor15:34 "Tumieni Akili Kama ipasavyo, Wala msitende dhambi Maana wengine hawajui Mungu. Ninanena hayo niwafedheheshe."
Ikiwa biblia inatambua na kuthamini matumizi ya Akili, naamini utaelewa sawia ninachoenda kukizungumzia mapema iwezekanavyo!
HALALI LAKINI HAIFAI
Hapa panahitaji utulivu kidogo. Kuna Mambo mengi sana hayafai kabisa kiafya Japo Ni halali. Kwa mfano uvutaji wa sigara kwa sheria za Tanzania Ni halali kabisa Japo haufai. Mpaka wazalishaji wa sigara huweka onyo, kwamba uvutaji wa sigara Ni hatari kwa Afya!
Ni hatari japo imethibitishwa na tbs! Kwa nini hawaachi kuzitengeneza? Wanataka Akili yako ifanye kazi! Ukiacha kuvuta hawawezi kuzalisha zingine!
Sasa sikia neno lisemavyo!
1Kor6:12 "Vitu vyote Ni halali kwangu, Lakini si vyote vifaavyo. Vitu vyote Ni halali kwangu Lakini Mimi sitatiwa Chini ya Uwezo wa kitu chochote."
Yawezekana Ni halali kabisa, sawa, lakini je inafaa?
Yawezekana Ni halali, lakini Swali je, imeletea uraibu? Umekuwa tegemezi kwa hiyo?
Unaweza kuongezea 1Kor 10:23-26
Kwani sumu Kama benofos siyo halali? Ni halali. Je inafaa? Ndiyo inafaa kwa kuua wadudu shambani . Je, ukiinywa? Ni uamzi wako, maana siyo najisi sawa lakini kwa hakika inaua!
Inaweza ISIWE najisi lakini ikawa na Athali hasi/mbaya.
Kwenye uhalali na kufaa, ndipo panadai uwekezaji wa Akili yako na utashi ili uamue vyema!
UMUHIMU WA KUTAMBUA NAFASI YAKO
Hili Ni Suala wazi Sana, Mtu anayejitambua vyema na anafahamu aina ya majukumu yake huamua Ikiwa awe mnywa POMBE au la.
Katika Ufalme wa Mungu iko hivi.
2Timotheo2:20-21 "Basi katika nyumba havimo Vyombo vya dhahabu na fedha tu, Bali na vya mti na vya udongo; Vingine vina heshima, Vingine havina. Basi Ikiwa mtu amejitakasa kwa kujitenga na hao, atakuwa chombo Cha kupata heshima, kilicho safishwa, kimfaacho Bwana, kimetengenezwa kwa kila kazi iliyo njema."
Wanaofahamu kuwa wametengwa kwa ajili ya kila kazi njema kwenye Ufalme wa Mungu hawawezi kuwa victim wa vileo na POMBE!
ANGALIA HAPA KWA MFANO
Samson hakupaswa kunywa pombe ili atimize vyema wajibu wake.
Waamuzi 13:1-14 zingatia zaidi aya ya 4 na ya 14 "Asile kitu chochote kitokacho katika mzabibu, Wala asinywe divai, Wala mvinyo, Wala Asile kitu chochote kilicho najisi: Na hayo yote niliyomwamuru na ayatunze."
Yohane Mbatizaji, pia hakupaswa kunywa pombe, kwa Maana alipaswa kutekeleza misheni maalum kabla ya ujio wa Yesu Kristo!
Luka 1:15 "Kwa sababu atakuwa mkuu mbele za Bwana: hatakunywa divai Wala kileo, naye atajazwa Roho Mtakatifu hata tangu tumboni mwa mama."
Soma tena Hapo "Kwa sababu atakuwa Mkuu mbele za Bwana hatakunywa divai Wala kileo"
Watu wakuu katika Ufalme wa Mungu hawanywi POMBE, Si kwa sheria, lakini Ni kwa sababu pombe Ni ya hadhi ya Watu wa Chini Sana!
NINI MBADALA WA POMBE KWAO?
Hapohapo Luka 1:15b badala ya Kujazwa pombe?
"Naye atajazwa Roho Mtakatifu hata tangu tumboni mwa *****."
Kwa kujua umuhimu huo, Paulo alikazia hivi
Waefeso 5:18 "Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo. Kuna ufisadi: Bali mjazwe Roho Mtakatifu."
Umeuona mbadala wa POMBE? Ni Kujazwa Roho Mtakatifu
SAIKOLOJIA NA ELIMU YA AFYA
Sisi wataalamu wa masuala ya saikolojia na Afya huwa tunashauri na kusisitiza hivi.
Mwanamke mwenye ujauzito Kama anataka kujifungua mtoto mwenye afya Nzuri ya "Akili" na mwili nilazima asinywe pombe, asivute sigara, etc
Pombe inabomoa ubongo wa mtoto tangu tumboni mwa *****!
Kwani kwenye clinic ya baba, mama na mtoto mnashauriwa Nini?
KWENYE UFALME WA MUNGU TUNA ADABU!
POMBE tangia lini ina adabu? Tangu lini mlevi akawa na adabu? Sasa jua kwamba kwenye Ufalme wa Mungu, tunaenenda kwa adabu!
Warumi 13:12-13 "Usiku umeenda Sana, mchana umekaribia, Basi na tuyavue matendo ya Giza na kuzivaa silaha za nuru. Kama ilivyohusika na mchana na tuenende kwa ADABU; Siyo kwa ulafi na ULEVI....."
Wagumu kuelewa Paulo aliwashauri hivi
Tito 2:3 "Vivyo hivyo na wazee wa kike wawe na mwenendo wa Utakatifu; Wasiwe wasingiziaji, wasiwe Wenye kutumia mvinyo nyingi, Bali wafundishao mema."
Zaidi Mtume Paulo aliutaja ulevi katika kundi moja na ugomvi, uchawi, uasherati, ufisadi uchawi uadui ugomvi wivu hasira fitina faraka uzushi husuda, ulevi ulafi nk!
Soma hapa Wagalatia 5:19-20
Kisaikolojia na kibaiolojia, Pombe hupenya haraka Sana kwenye ubongo na kuharibu vibaya Sana maeneo anuai ya ubongo kama Medulla oblangata, hypothalamus, hippocampus, Cerebellum, frontal lobe na cerebral cortex!
Mifumo hii ikiharibika unakuwa "Zombie" kama mazombi mengine, kwa muda au milele!
Pombe ina change mental state! Mental state ikibadilika anything else can happen!
Hujawahi kuona mtu mzima na heshima zake anakojoa Hazarani?
Unalikubuka tukio la mlevi kupiga watu kwa risasi na yeye kujiua huko Sinza Dar es salaam hivi Karibu?
Na ndiyo maana Kuna Mambo mengi hujitokeza baada ya kulewa kama vile
Mithali 23:29-35 "Ni Nani apigaye yowe? Ni Nani aliyae ole? Ni Nani mwenye ugomvi? Ni Nani mwenye mguno? Ni Nani aliye na JERAHA zisizo na sababu? Ni Nani aliye na macho mekundu? Ni wale wakaao kwenye mvinyo, waendao kutafuta divai iliyochangamka......."
Tatuta usome pote!
ZAIDI ya hayo biblia inasema hivi
Mithali 20:1 "Mvinyo hudhihaki, kileo Huleta ugomvi na akosae kwa vitu hivyo Hana Hekima."
POMBE INA "OLE"
Isaya 5:11 "Ole wao waamkao asubuhi na mapema, wapate kufuata kileo. Wakishinda Sana hata usiku wa manane mpaka mvinyo imewaka Kama Moto ndani yao."
Pombe inaaibisha na kudhalilisha
Mwanzo 19:30-38 (Hapa Lutu analewa Pombe na kufanya ngono na binti zake)
POMBE INALETA UMASIKINI NA KUTELEKEZA MAJUKUMU.
Kama mwanasaikolojia, Nimeshauri wanafunzi wengi Sana wa sekondari, msingi na vyuo vya Kati, ambao masomo Yao yameathirika Sana kutoka na ulevi wa wazazi wao!
Ndoa nyingi na familia zinaomboleza kwa ajili ya Pombe!
Halafu mtu mmoja "anabana pua" ilibarikiwa kabisa kwenye harusi ya kana shame on you!
ELEWA KUWA
1 Timotheo 5:8 "LAKINI mtu yeyote asiyewatunza walio wake, yaan wale wa nyumbani mwake, hasa ameikana imani. Tena ni mbaya kuliko asiye amini."
Pombe imewafanya watu wangapi waikane imani kwa kutokujali wenzi na familia zao?
Mimi Ni zao la jamii hii ya Tanzania, utanidanganya Nini juu ya Pombe?
Wanandoa wangapi wamezini kisa Pombe?
Familia ngapi zimevurugika kisa Pombe?
Kuna Vijana wangapi wamepata magonjwa ya zinaa na UKIMWI Kama matokeo ya ngono zembe kwenye clab za Pombe?
Makasisi wangapi wamedhalilika na kudhalilisha kanisa kisa Pombe?
SIKIA WEWE KIZIWI NENO LA BWANA
Mithali 21:17 "Mtu apendaye anasa atakuwa masikini, apendaye MVINYO na mafuta hatakuwa tajiri."
Hapa Tanzania, familia nyingi ziko kwenye mstari wa umasikini wa kutupwa, hasa vijijini kutokana na Pombe tu! Kama hujui, jua hivyo kuanzia Sana!
Katika individual na family level, poverty inasababishwa na Pombe kwa asilimia zisizopungua 75.
Usitake Sana kubishania Mambo ya kipumbavu! Kwani huna ndugu, jamaa, rafiki, jirani, classmates etc aliyepata majanga na kuharibu kabisa hatima Yake kutokana na Pombe?
KWA NINI MAKANISA BAADHI YANAPIGIA CHAPUO POMBE?
1. Akili za kinabii Tito
Yesu aligonga, tugonge jamani imeandikwa Luka 7:33-35
Nilishangaa watu wakimcheka nabii Tito kwamba anapotosha, wakati kwa masikio yangu nimesikia kwenye mahubiri zaidi ya Mara kumi Makasisi wakihubiri hivyo kuanzia kwenye dini yangu . So ma TITO Wapo kila Kona, kila dini na kila dhehebu, sema wengine wanaheshimika, wengine wanadharaulika, lakini Akili yao moja!
Yesu hakuwahi kuwa mlevi, aliitwa hivyo na wapinzani wake wakuu, hasa mafarisayo!
Zaidi sana Yesu alionya hivi!
Luka 21:34 “Basi jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa kwa ulafii na ULEVI na Masumbufu y a maisha haya; Siku ile ikawajia ghafula, kama mtego unasavyo!”
Kwa nukuu hiyo, unapata wapi ujasiri kusema Yesu aligonga?
2. Mtume Paulo aliagiza tugonge
Ila Nyinyi watu! Paulo aliagiza wapi?
1 Timotheo 5:23 "Tokea Sasa usinywe maji tu, Lakini tumia MVINYO kidogo kwa ajili ya tumbo lako, na magonjwa yanayokupata Mara kwa Mara."
Jamani, hata kwa Akili za usiku Ni kweli Paulo anaagiza hapo tugonge? Hata kwa Akili zangu za darasa la kwanza Mwishoni mwa miaka ya 90 kule shule ya msingi Kawekunelela-Ushetu Kahama, ningeelewa hivyo ?
Kwamba, Wakristo wote tunaumwa tumbo? Na tunapatwa na magonjwa Mara kwa Mara Ambayo tiba yake Ni kwenda baa?
Pombe Kama dawa Haina shida, Maana hata majani ya bangi hutengenezwa dawa na kemikali nyingi zifaazo kwa tiba! Kama daktari kakwambia hivyo sawa, Lakin usihalalishe uraibu wako kwa kigezo Cha dawa wakati huna ugonjwa unaotibika kwa Pombe.
3. Inaleta furaha ya moyo! Zaburi 4:7 na zaburi 104:15
Elewa wazi kuwa, Hii ilikuwa njia Nzuri kwa watu wa agano la kale kujiliwaza kwa Sababu Roho Mtakatifu alikuwa bado hajamwagwa!
Leo hatutegemei Pombe kufurahi, badala Yake tunafuraha Kama matokeo ya kuongozwa na Roho Mtakatifu!
Wagalatia 5:22 "Lakini tunda la Roho Ni UPENDO, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole na kiasi. "
Unasaka furaha kwenye Pombe? Fikiri kiungwana!
Ndiyo maana nimetangulia kusema kule juu na Hapa nakumbusha!
Waefeso 5:18 "Tena msilewe kwa mvinyo ambamo man ufisadi Bali mjazwe Roho Mtakatifu."
Zaidi ya hapo Nisemeje?
4.Kuondoa mawazo!
Mithali 31:6-7 "Mpe kileo yeye aliye karibu na kipotea, kaMpe divai yeye aliye na uchungu nafsini, Anywe akausahau umasikini wake, asiikumbuke Tena taabu Yake."
Kwa kawaida shida, dhiki, umasikini na uchungu nafsini havitoki kwa kunywa Pombe. Zaidi vinakupa temporary relief na Pombe ikiisha matatizo unayakuta yanakusubiri! Wanasaikolojia wote wanaomjua Mungu na WAPAGANI hawawezi kukushauri kunywa Pombe kumaliza.matatizo yako!
MWISHO Kama umesoma na kuelewa Basi fanya uamzi wako Mwenyewe!
Umebarikiwa milele!
Kama hujampa Yesu Kristo maisha yako, hii Ni fursa kwako! Karibu katika Ufalme wa Mungu!
Kumbuka
#Shetani Anaogopa mtu anayejua kitu