Kuelekea Rais Samia kulihutubia Bunge: Barua ya Wazi kwa Spika wa Bunge Job Ndugai

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
14,237
53,482
Mheshimiwa Spika,

Nakusalimia kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Natambua leo ni siku ambayo rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan analihutubia Bunge la nchi yetu. Na mimi kama mwananchi nimelazimika kukuandikia barua hii ili kwayo uweze kutafakari, pengine itakusaidia wewe katika majukumu yako ya kuongoza chombo hicho muhimu chenye wajibu wa kisheria wa kuisimamia serikali. Kwa mantiki hiyo basi ninayo haya ya kukueleza.

1. Mheshimiwa Ndugai umeshiriki kuvunja katiba ya nchi na hivyo umevunja kiapo chako cha kuilinda na kuitetea na kuihifadhi katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Ndugai, huku ukifahamu wazi kuwa Katiba ya nchi inataka watu waingiao bungeni ni lazima wawe wametokana na vyama vya siasa, lakini wewe umefumbia macho, kusaidia na kuwezesha kinyume cha katiba bunge lako kuwa na wabunge wasio na chama ndani ya Bunge. Huku ni kuikanyaga Katiba bila aibu, na ni kuvunja kiapo ulichokula cha kuilinda katiba huku sisi wananchi tukishuhudia.

2. Kuisaliti katiba ni kuisaliti nchi
Mheshimiwa Spika, Mwalimu Nyerere alitwambia, Lengo mojawapo la kuapisha watu ni ili pindi wakitusaliti tuwashitaki. Ninatambua fika kuwa Wewe na naibu wako mliwekewa kinga ya kutoshitakiwa, na leo hii tumeng'amua kuwa kumbe ile sheria mliyowekewa mapema kabla ya uchaguzi ilikuwa ni maandalizi ya nyie kutumika kwa kazi "chafu" hata ikibidi kuvunja katiba ya nchi kwa ajili ya masilahi machache ya mtu mmoja na genge lake—Hata hivyo baba wa Taifa letu alitwambia, tunawaapisha watu ili wakikiuka viapo vyao tuwaone ni wasaliti, Sasa Mheshimiwa Spika, Unakiuka kiapo chako cha kuilinda na kuihifadhi katiba waziwazi kwa kuruhusu watu wasio na chama chochote cha siasa kuwa wabunge ndani ya bunge lako, Kwa nini sisi tusikuone kuwa umesaliti kiapo chako na hivyo kuisaliti nchi kiujumla?, Je ni precedent ya namna gani umeiweka kwa ajili ya vizazi vijavyo kwa kitendo chako hiki cha aibu?

3. Bunge kuwa na wabunge kinyume cha katiba kunavunja heshima, hadhi na mamlaka ya bunge
Wajibu wa Bunge ni kuisimamia serikali, ni chombo kimojawapo cha checks and balance. Kama Bunge linakuwa kinara wa Kuvunja katiba ya nchi, je Litaisimamiaje serikali kwenye mambo ya kikatiba ya utawala bora?

Kama bunge linafumbia macho uvunjaji wa wazi wa katiba ya nchi je hiyo hadhi na heshima inayolistahiki inatoka wapi?
Mheshimiwa Ndugai, ni lazima ujue kuwa kitendo chako cha kukumbatia wabunge waliomo bungeni kinyume cha katiba ya nchi kinashusha heshima ya bunge. Bunge linalovunja katiba ya nchi siyo bunge lenye heshima wala hadhi, bunge ambalo kuna sheria zitatungwa kwa kupigiwa kura na wabunge wasio halali kwa mujibu wa katiba hilo siyo bunge lenye heshima—Mheshimiwa Ndugai, wewe mwenyewe pima, uone kama ni sahihi kuendelea kuwa na bunge la hivi, bunge lenye wabunge wasio halali kwa mujibu wa katiba ya nchi!

4. Uvunjaji wa katiba ndani ya bunge, kisha uvunjaji huo kutetewa na bunge kunamvunjia heshima Rais ambaye ni sehemu ya Bunge
Huwezi kuvunja katiba bila haya, kisha uvunjaji huo ukatetewa na Spika na bunge husika halafu kitendo hicho kisiharibu Taswira njema ya Rais. Rais wetu ni sehemu ya bunge, Sasa inakuwaje kwa mfano rais awe ni sehemu ya bunge lenye kuvunja katiba? —Kiukweli kabisa hili tendo siyo sawa hata kidogo. Ni lazima hatua zichukuliwe kwa mujibu wa katiba ya nchi na sheria ya nchi kurekebisha hili. Hili suala siyo dogo, ni suala kubwa. Hii tabia ya kutoheshimu vipengele vya katiba ikiota mizizi, huko mbeleni tutapata shida maana itakuwa imezoeleka.

Hitimisho
Mheshimiwa Ndugai, huna justification yoyote au uhalali wowote wa kuvunja katiba ya nchi, maana Uliapa kuilinda.
Unaweza kuivunja Kwa Mujibu wa udikteta na kwa kulindwa na Serikali ambayo ina wajibu wa kuenforce sheria za nchi lakini hivihivi bila kufanya hivyo huna haki, na wala hauko sahihi kwa kitendo chako hicho haramu cha kuvunja katiba ya nchi huku ukijua.

Mheshimiwa Ndugai, uliapa wewe huku Umeshika Biblia, Sasa jipime kama kweli uzito wa Maneno ya Mungu yaliyomo kwenye biblia unayaheshimu au umeamua tu kuyasigina.

Pia ulilitaja jina Mwenyezi Mungu kuwa akusaidie, sasa Jiulize je ulilitaja jina hilo kama kasumba tu au ulimaanisha.

Ndugai MWENYEZI MUNGU HATANIWI, Shauri yako!
 
Mheshimiwa Spika, Unakiuka kiapo chako cha kuilinda na kuihifadhi katiba waziwazi kwa kuruhusu watu wasio na chama chochote cha siasa kuwa wabunge ndani ya bunge lako, Kwa nini sisi tusikuone kuwa umesaliti kiapo chako na hivyo kuisaliti nchi kiujumla?, Je ni precedent ya namna gani umeiweka kwa ajili ya vizazi vijavyo kwa kitendo chako hiki cha aibu?
mama makinda uko wapi japo umshauri mwezio huyu?
RIP Mh.Sitta.
 
Katiba inasema atakachosema Rais ni sheria.

Ndiyo sababu ameweza tengua maamuzi ya mahakama kwa kuwatoa wabakaji ambao mahakama iliwakuta na hatia.

Hivyo basi kama Ndugai alikua anasikiliza kila anachosema Rais ni kwakua Katiba inamtaka kufuata kila anachosema Rais.
 
Spika jukumu lake ni kupokea wabunge na kuendesha vikao.

Tume ya uchaguzi ndio yenye jukumu la kuhakiki majina yanayoletwa na vyama!
John!
Kumbuka uanachama wa mbunge katika chama chake unaweza kukoma angali akiwa mbunge tayari, na ikitokea hivyo mbunge anapoteza sifa za ubunge.

Ndugai hawezi kujitetea kwa technicality yoyote kwa sababu vyombo vyote unavyovijua wewe akiwemo na spika mwenyewe wameshaandikiwa barua ya kuwajulisha kuwa Hao watu 16 siyo wanachama tena wa CHADEMA
 
John!
Kumbuka uanachama wa mbunge katika chama chake unaweza kukoma angali akiwa mbunge tayari, na ikitokea hivyo mbunge anapoteza sifa za ubunge.

Ndugai hawezi kujitetea kwa technicality yoyote kwa sababu vyombo vyote unavyovijua wewe akiwemo na spika mwenyewe wameshaandikiwa barua ya kuwajulisha kuwa Hao watu 16 siyo wanachama tena wa CHADEMA
Nimekuelewa bwashee

Halima Mdee na wenzake walifukuzwa uanachama wakiwa wameshaapishwa na Spika Ndugai.

Uko sahihi ni Spika Ndugai anapaswa kutengua kiapo, NEC wajibu wake uliishia pale Halima Mdee alipokula kiapo!
Kwahiyo Chadema ina mbunge mmoja kama taa ya treni ya bara!
 
Bunge la Ndugai haliisimamii serikali bali serikali ndio inalisimamia bunge
Assadi alisema Bunge ni dhaifu
Mh.Rais Samia amesema Bunge halina afya kwa Taifa. Kweli kama bunge lisingekua dhaifu lingejadili hoja ya Mh.Rais
 
yaani chadema mmejazana ujinga usiyo na maana sasa ndugai kaletewa majina na tume ya uchaguzi kazi yake kuwaapishatu kavunjasheria gani nyie anzieni huko nyuma muulizane ndani ya chadema nani kapeleka majina? mbona mbowe yuko kimya nyie vipanya ndiyo mnarukaruka huku chini?muulizeni mbowe
 
Yaani inabidi Ndugai awe anawekewa mipaka ya kufanya kazi sio tena na katiba labda na mwenyekiti wake
Aambiwe aache kushabikia wanao demka wala yeye asidemke
 
Kaz ya kamati kuu ya chadema iko wazi kufukuza watu uanachama sio sehemu ya kazi yao wao ni kupendekeza tu baraza kuu mkutano mkuu ndio una mamlaka haujakaa hadi leo kisingizio eti corona wakati mnaitisha mikutano ya hadhara ambayo ina watu wengi kuliko kikao cha baraza kuu

Ndugai anasubiri maamuzi ya kikao chenu cha baraza kuu mkutano mkuu .Mbona mna kigugumizi kuuitisha kulikoni?
 
yaani chadema mmejazana ujinga usiyo na maana sasa ndugai kaletewa majina na tume ya uchaguzi kazi yake kuwaapishatu kavunjasheria gani nyie anzieni huko nyuma muulizane ndani ya chadema nani kapeleka majina? mbona mbowe yuko kimya nyie vipanya ndiyo mnarukaruka huku chini?muulizeni mbowe
Sasa hao aliokwishawapitisha wamevuliwa uanachama wa chama chao, na hivyo kwa mujibu wa katiba wamepoteza sifa za kuwa wabunge.
 
Kaz ya kamati kuu ya chadema iko wazi kufukuza watu uanachama sio sehemu ya kazi yao wao ni kupendekeza tu baraza kuu mkutano mkuu ndio una mamlaka haujakaa hadi leo kisingizio eti corona wakati mnaitisha mikutano ya hadhara ambayo ina watu wengi kuliko kikao cha baraza kuu

Ndugai anasubiri maamuzi ya kikao chenu cha baraza kuu mkutano mkuu .Mbona mna kigugumizi kuuitisha kulikoni?
Kasome katiba ya Chadema.

Hata Mdee alikiri kuwa Kamati kuu ya Chadema ina mamlaka kwa maamuzi iliyochukua!
 
Back
Top Bottom