Kudhibiti ongezeko la kasi la idadi ya watu Tanzania

Jack Daniel's

JF-Expert Member
May 18, 2015
1,008
835
Kuendelea kwa ongezeko la kasi la idadi ya watu nchini linaweza kuwa kikwazo kwa nchi kuyafikia malengo yake ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Tunahitaji kuwa la asilimia sifuri kwa ongezeko la idadi ya watu (zero population growth)…..Idadi ya watu wanaopungua iwe sawa na idadi ya watu wanaongezeka katika kipindi fulani…..

Kwa wastani, watu 5,020 hufariki kwa siku nchini Tanzania ukilinganisha na wastani wa watu 29,669 wanaozaliwa kwa siku. Ina maana kwa wastani watu 24,000 huongezeka kwa siku. Pia kwa wastani kila mwanamke huzaa watoto 5 kwa mwaka…..

Idadi yetu inakua kwa asilimia 3 kwa mwaka toka miaka ya 1970. Wakati tunapata uhuru tulikuwa watu milioni 10 tu, mwaka 1980 tulikuwa milioni 18, mwaka huu (2016) tupo milioni 55. Toka tarehe 1 Januari 2016 hadi leo watu 3,518,746 wameshaongezeka……

Tukiendelea hivyo, ifikapo mwaka 2020 tutakuwa na idadi ya watu si chini ya milioni 62, mwaka 2050 tutakuwa watu zaidi ya milioni 137……..mwaka 2090 kutakuwa na watu wasiopungua milioni 268……

Tufanyaje:

Matumizi ya njia za kisasa za uzazi wa mpango yapo bado katika kiwango cha chini, ingawa mahitaji ya uzazi wa mpango ni makubwa. Tunahitaji kuhakikisha kwamba kila mtu ana uwezo wa kuchagua, kupata na kutumia njia bora za uzazi wa mpango wakati wo wote anapozihitaji……

Serikali iweke sheria kwamba kila familia isiwe na watoto zaidi ya watatu kwa kuanzia, baadae watoto wawe wawili mwisho….mtu akizidisha hapo apewe adhabu kali……hatuzitendei haki rasilimali tulizopewa na mwenyezi Mungu……Mtu anazaa watoto wengi kwani anataka kuanzisha kijiji chake?

Serikali iruhusu zoezi la kutoa mimba liwe halali na lifanyike mahospitalini na katika vituo vya afya….kuwepo kwa sheria inayobana kunamaanisha hata hospitali zenyewe zinakosa huduma bora ya utoaji mimba, vifaa na mafunzo kwa wauguzi na madaktari……

Nchi tatu Afrika zimehalalisha kutoa mimba, Cape Verde, Afrika Kusini na Tunisia, sio kwamba hawana akili bali wameangalia mbali na kufanya maamuzi magumu…….

Hapa Tanzania inakadiriwa mimba zisizotarajiwa hufika 1,000,000 (milioni moja) kila mwaka na kati ya hizo, mimba 405,000 (39%) hutolewa (na hapo sheria inabana)……

Ongezeko la taratibu la idadi ya watu linatoa fursa kwa ukuaji wa kasi wa uchumi. Pia, kupungua kwa kasi ya uzazi katika ngazi ya nchi kunaweza kusaidia kuandaa njia ya kuondokana na umaskini kwa wananchi wengi…..

Tanzania Population (2016) - World Population Review

Nawasilisha…….
 
mkuu yaani unawaza kama mimi, serikali inatakiwa iweke idadi ya watoto iwe mwisho 3 tu, kweli idadi ya watu inaongezeka kwa kasi sana aisee
Unakuta uchumi wa nchi unakua wa asilimia kubwa lakini wananchi walio wengi bado wanaumia. Fursa zinazotengenezwa na ukuaji huo wa uchumi hazitoshelezi idadi kubwa ya watu.......

Upande wa pili gharama za kuendesha serikali zinaongezeka, kwa mfano, kujenga vituo vya afya, hospitali, mamlaka tofauti, shule, vyuo, miundombinu n.k........
 
Acha tuongeze zaidi ili tupate akili za kutatua changamoto za kijamii.
Mkuu, kwa mfano, China watu walishaongezeka sana na wakaona hailipi ndipo wakapitisha sheria ya kuzaa mtoto mmoja baadae wakapima wakaona hata wawili sio mbaya.....

Sio kitu cha kujaribu, ukuaji wa kasi wa idadi ya watu unagharimu maendeleo ya kiuchumi kwa nchi nyingi duniani....
 
Hizo ni propaganda tu ila ukweli ni kwamba bado tuna sehemu kubwa sana iko wazi...nani atakaa/ataishi hizo sehemu? sehemu kubwa ni pori tu...acha watu waongezeke...watapambana huko mbeleni namna ya kusurvive wakati mimi na wewe tukiwa tumeshasepa zetu. Ni sawa na sisimizi wanazaana wengi say 1000, ili mwisho wa siku wakifa 600 bado 400 wataendelea kuishi na kuzaana. Ndo mambo ya "Darwinism" mkuu.
 
acheni kutetea mauaji nyie!
1. kutoa mimba ni kuua hivyo haifai
2. njia za uzazi wa mpango zisizo za asili kama kutumia vidonge na sindano za kuzuia mimba hazifai kimaadili kwani zinazuia mpango wa Mungu wa uumbaji.zipo njia za asili zaweza kufuatwa!
3. ufisadi na matumizi mabaya ya rasilimali ndo chanzo cha umasikini na kuzorota maendeleo na siyo idadi ya watu. watu ni rasilimali ndo maana Ujerumani na Urusi anayezaa anapata ruzuku toka serikalini.
 
Swala la kudhibiti ongezeko la watu hapa TZ ni muhimu sana kwa uchumi wa nchi. Na sijui kwa nini serikali halitii mkazo katika uzazi wa mpango. Kukuza uchumi bila kudhibiti ongezeko la watu ni kazi bure. Ndio maana kila siku madarasa, madawati, walimu, dispensary nk hazitatosha. Tutakuwa na kazi ya kujenga kila siku. Hivi umeshawahi kusikia ulaya wana kazi ya kujenga madarasa mapya? Hata kama yatakuwepo lakini sio mengi kama sisi. Ni kwa sababu ongezeko la watu halitofautiani sana wanaofariki. Jambo la ajabu serikali yetu iko kimya. Kinachotakiwa ni kutoa elimu juu ya uzazi wa mpango hasa vijijini na hili halihitaji donors au fedha za kigeni.
 
Tatizo sio sehemu ya kuishi, tatizo ni jinsi gani serikali itawapatia maisha bora hao watakao zaliwa?
 
Tatizo sio sehemu ya kuishi, tatizo ni jinsi gani serikali itawapatia maisha bora hao watakao zaliwa?
Huwezi kusolve tatizo ambalo halipo. Tusubiri tatizo litokee ndo tuanze kusolve. Sasa hivi inabidi watu wazae, ili wengine waende wakatawale na nchi jirani...hii ya kuanza kucontrol population growth wakati hata mil 100 hatujafika ni kuogopa changamoto. Ni lini serikali yetu imetoa huduma za kuridhisha hata kipindi hiki ambacho bado tuko wachache? Maana yake ni kwamba, tukiishi kwa kurelax sana tegemea watu wasiofikiria (wasiojua namna ya kupambana na changamoto za kuishi).
Ndiyo maana naunga mkono watu wazae kwa wingi, tutapungua tu naturally maana zipo njia zinazopunguza idadi ya watu naturally..not artificially...refer to Darwinism Theory!!
 
Mimi naona bado tupo wachache sana ukilinganisha na rasilimali zilizopo ....
Kuna mikoa ukifika ni kama hakuna watu kabisaaa...

Tatizo la Tanzania si watu wengi bali watu wengi si wazalishaji Mali hivyo, kiasi cha utegemezi ni kikubwa sana....

Serikali iboreshe elimu
Pamoja na mazingira ya uwekezaji kwa wazawa ili watu wengi wawe productive zaidi na hii itasaidia katika utanuzi wa uchumi wetu...

Population ni uhai wa nchi yetu na haswa ikiwa productive
 
Tatizo litokee mara ngapi? Kaya zinazopata umeme hazifiki 50% ya kaya zote nchini,huduma za afya awapati,maji,elimu,barabara bado unataka serikali iendelee kuongezewa mzigo?
 
Tatizo litokee mara ngapi? Kaya zinazopata umeme hazifiki 50% ya kaya zote nchini,huduma za afya awapati,maji,elimu,barabara bado unataka serikali iendelee kuongezewa mzigo?
Unakubali kabisa hatuna uwezo wa kutoa hizo huduma katika kiwango kinachotakiwa say with reference to USA? Angalia kwa mfano: Je ni wangapi wanaofanya kazi na ni wangapi wanategemea kulishwa? Tatizo siyo idadi ya watu, tatizo hapa ni mentality za watu kutatua changamoto. Hizo rasilimali watu unazotaka kuzifuja kwa kuzuia watu wasizae huoni baadae utarudi kuhamasisha watu wazae ili tupate nguvukazi? Unapozungumzia suala la kucontrol population growth, lazima uangalie pia athari zake kwa kina.
Tuna rasilimali nyingi ambazo hatuzitumii ipasavyo kuendeleza jamii zetu, bado unataka tujiongezee changamoto nyingine ya kuacha kuzaa...by the way hadi sasa hatujastress minds zetu hadi mwisho kukabiliana na matatizo ambayo yako ndani ya uwezo wetu. Unataka kuniambia huduma za afya, maji, elimu, barabara serikali haiwezi kuziboresha zikawa za mfano? No no no siamini hivyo mkuu..tunaweza sema serikali yetu kuna vitu haijaamua.
 

Uzazi wa mpango utakuja wenyewe kwa jinsi maisha yanavyozidi kuwa magumu.
Watu wengi siku hizi wana watoto wachache kutokana na maisha.

Kuhusu ulaya najua kuwa wametutangulia sana wanapojenga wanajenga sio kwa wanafunzi 200 bali 2000 yatajaa kutokana na ongezeko la wanafunzi.

Hata hapa walipokuwepo airport zilijengwa kwa uwezo mkubwa, ingawa zilikuwa zinatua DC10.

Market zinahodhi nafasi mpaka leo ingawa zilijengwa miaka ya 70.

Police headquarters pia mpaka leo hazijaongezwa ukubwa (baadhi) ziko vile vile tangu mkoloni.
 
1. Mimba 405,000 hutolewa kwa mwaka Tanzania, ina maana hata watu wasiporuhusiwa wataendelea kutoa tu, na vipi kuhusu vifo vinavyotokea wakati wa utoaji huo hasa vichochoroni au vifo hivyo havina umuhimu?
2. Zitumike njia zote, kwa watakaoshindwa kutumia njia za asili wanaweza kutumia njia za kisasa, kwani hizo za kisasa zimesaidia wengi na hizo za asili zina kasoro pia
3. Ni kweli ufisadi unachangia umasikini wa watu lakini sio chanzo pekee cha umaskini, tunahitaji kuangalia chanzo kingine kama ukuaji wa kasi wa idadi ya watu.

Ujerumani watu huzaliwa kwa wastani 9,568 na hufariki 12,435 kwa siku na Urusi watu wanazaliwa 24,217 na wanafariki 27,964 kwa siku. Tatizo sio tu ukuaji wa kasi wa idadi ya watu bali hata ukuaji mdogo kupitiliza wa idadi ya watu. Udhibiti wa ukuaji wa idadi ya watu unatakiwa kuzingatia mengi, tunahitaji kuelekea karibu na sifuri, tusiende sana kwenye chanya na pia tusiende sana kwenye hasi.......
 
Kama kuna wastani wa mimba zaidi ya 400000 ambazo hutolwa kila mwaka ndiyo maana nchi imelaanika. Tunawezaje kuua watu wengi namna hii tusichokoze hasira ya Mungu? Lo! Inatisha kama nini.
 
Hayo unayoita mapori yana wenyewe na wafugaji na wakulima wanagombania maeneo ya malisho na kilimo. Lakini pia, idadi ya watu wanaotoka vijijini kwenda mijini kutafuta maisha huongezeka kila siku na hivyo kufanya miundombinu ya mijini kushindwa kuhimili ongezeko la kasi la idadi ya watu......

Wakati wewe unafikiria kusepa na kuacha tatizo litatuliwe na watoto na wajukuu zako, sisi wengine tunafikiria kuiacha nchi katika hali nzuri kuliko tulivyoikuta kwa vizazi vijavyo. Watakuja kutulaumu kwamba kama tuliona tatizo kwanini hatukuchukua hatua madhubuti kudhibiti tatizo kabla halijawa sugu kupitiliza? Kwanini tuwaachie matatizo vizazi vijavyo, matatizo tunayoweza kutatua sasa?
 
Wazo zuri lakini ni vigumu sana kutekeleza hasa haya mahusiano ya kikanda eg EAC Tanzania yaweza kuweka mipango ya uzazi wa mpango sawa tukabaki kupokea warundi,wanyarwanda wanaozaliana kama Panya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…