Ushuru wa stendi za mabasi na vituo vya daladala ni eneo mojawapo ambalo linavujisha sana mapato ya serikali. Ushuru huu kwa sasa unakusanywa na halmashauri na kwa jiji la DSM kwa mfano, kampuni binafsi zimepewa uwakala wa ukusanyaji.
Nipongeze kwanza hatua za waziri was fedha kuhamishia ukusanyaji wa ushuru wa mabango TRA, hatua hii itaziba uholela wa ukusanyaji kodi uliokuwa unafanywa na halmashauri.
Nikirudi kwenye ushuru wa stendi, lengo la kuanzishwa kwa ushuru huu ilikuwa ni kuzifanya standing za mabasi kuwa sehemu salama na safi. Pili ilikuwa ni kuviwezesha vituo vikubwa kuwa na miundombinu rafiki kwa abiria ikiwemo vyoo, shoe shiners na kuondoa wapiga Debe ambayo ni kero kubwa kwa abiria. Na tatu ilikuwa kuzipatia halmashauri mapato yatakayowezesha kumantain Huduma za kijamii ktk stendi hizo.
Mradi huu umekuwepo kwa takribani miaka 15 sasa na ulianzia Mwenge kwa vituo vya daladala na Kibaha kwa mabasi ya mikoani Vila kukihusisha kituo kikuu cha mabasi ya mikoani ubungo ambacho kilikuwa na utaratibu wake. Nimeweka hiyo historian ndogo ili Waziri wa fedha ajue umuhimu wa mradi huu.
Mradi huu kwa jiji la DSM tu unaweza ukaingiza zaidi ya tsh 5 bilioni kama mfumo wa ukusanyaji wake utaimarishwa, na njia pekee ni kuuingiza ktk mfumo rasmi wa ukusanyaji ushuru chini ya TRA.
Kwa sasa hapa jijini zipo daladala zinalipa hadi sh 1500 kwa siku kama ushuru wa stendi, wakati kwenye mfumo rasmi wangelipa sh 1000 tu au pungufu. Tafadhali waziri was fedha chukua changamoto hii kama ambacho mmefanikiwa kwenye kodi ya ardhi ambayo kwa sasa tunalipa kwa njia ya siku na inaingia Mona kwa Mona hazina.
Nawasilisha!