Dawson Muntara
New Member
- Dec 16, 2023
- 4
- 3
Kuchelewa hatua za ukuaji Kwa mtoto (Delayed milestone) na ufumbuzi wake.
Mtoto anapozaliwa anatakiwa kukua kimwili, kiakili, lugha na kijamii. Wengine hukua haraka au hufuata hatua za ukuaji pasipo kuchelewa ila Kuna wale ambao kutokana na sababu mbalimbali huchelewa kuendana na hatua za ukuaji za kawaida kama watoto wengine.
Kumekuwepo na Imani mbalimbali kuhusu sababu au chanzo cha kumfanya mtoto achelewe katika hatua za makuzi. Fuatana nami katika makala hii ili uweze kupata majibu ya maswali yanayoulizwa na wanajamii Kwa ujumla:
Maswali haya matatu yanaulizwa na idadi kubwa sana ya wanawake wanaonyonyesha:-
1. Je nikikutana na baba mtoto, nitambemenda mtoto?
2. Je nikimshika mtoto baada ya tendo la ndoa, mtoto atapata madhara?
3. Je nikikutana na mwanaume asiye baba wa mtoto, nitambemenda mtoto?
Mtoto aliyedhoofu mwili, haongezeki uzito, amechelewa, au hakuwi sawa sawa kama watoto wengine wa umri wake inaaminika kwamba mtoto huyo amebemendwa.
Asili ya kubemenda!
Imani hii imekuwepo miaka sana. Na inapatikana katika maeneo ya Tanzania.
Watu wanaamini kwamba mama anapokutana kimwili, mbegu za kiume huingia kwenye damu na kusafiri mpaka kwenye maziwa. Mtoto akinyonya maziwa hayo anapata madhara. Anakuwa amebemendwa.
Je ukweli ni upi
Ukweli ni kwamba, dhana ya mtoto kubemendwa ni dhana potofu. Mbegu za kiume hazina uwezo wa kupenya kwenye mwili na kufika kwenye maziwa ya mtoto. Hazina uwezo huo.
Hivyo hata mama kumshika mtoto baada ya tendo la ndoa haina madhara yoyote kwa mtoto.
Nini husababisha mtoto kudhoofu
Kuna sababu mbalimbali zinasababisha mtoto kudhoofu afya yake. Watoto wengi wanaosemwa kwamba mama yake amembemenda ukimuangalia ni yule mtoto mwenye matatizo ya utapia mlo, mtindio wa ubongo au maradhi mengine yanayoathiri ukuaji mfano matatizo ya moyo n.k.
Endapo wana ndoa sio waaminifu au mama amekutana kimwili na mwanaume mwingine anaweza kupata maambukizi. Maambukizi hayo yanaweza kumuathiri mtoto pia. Mtoto anaweza kupata maambukizi wa HIV kupitia maziwa ya mama yake
Je ni sawa kukutana kimwili?
Dhana hii ya mtoto kubemendwa ni moja wapo ya mambo ambayo yamesababisha wanaume wengi kuchepuka. Kuchepuka ambako kumeleta magonjwa katika familia. Hakuna madhra yoyote kukutana kimwili.
Endapo utaona mwanao anachelewa kwenye makuzi yake usichelewe kumpeleka aonane na daktari wa watoto ili amfanyie uchunguzi wa kitabibu. Yeye ataweza kubaini chanzo Cha kuchelewa kwenye makuzi ya mwanao.
Pia Tiba Kwa njia ya vitendo ( occupational therapy) itamsaidia mtoto aliyechelewa hatua za makuzi kuweza kupiga hatua katika makuzi ya kiakili, kimwili na kijamii.
Tunashauri mtoto aonwe mapema katika hatua za awali za tatizo (early intervention) ili kuweza kupata matokeo chanya na ya haraka.