Hamna asiyekubaliana na hili kuwa mkeo akitembea na mwanaume nje ya ndoa yenu inauma sana na pale utakapogundua kakubambikia na watoto wenu kuwa sio damu yako hapo utatamani usingezaliwa maana maimivu yake hayaelezeki.
Kuna mkasa nimeuona dah mwanzo nikawa nasikitika ila baadae nikabaki nacheka.
Mkasa wenyewe ni mrefu nitajitaidi kuufupisha.
Mke anaitwa Wankyo na mume anaitwa Lincoln,sasa bwana Lincoln alikuwa na rafiki yake anaitwa Kareem mhindi ni mfanyabiashara mkubwa tu wa magari.
Kareem akamzunguka Lincoln akatembea na mke wake Wankyo bila Lincoln kujua hadi akampa ujauzito.
Lincoln akalea mimba akijua yake loh siku Wankyo kujifungua mtoto wa kike muhindi yaani hakuitaji mkemia mkuu kumwambia Lincoln kama kaibiwa.
Tofauti na matarajio ya wengi Lincoln akasisitiza kuwa yule mtoto ni wake watu wakawa wanamcheka dah na Lincoln hakuwahi kumuoji Wankyo Kwanini mtoto ni muhindi.
Loh kumbe Lincoln alikuwa na plan zake moyoni... Akamlea yule mtoto jina Reila kwa upendo wa hali ya juu.
Miaka ikapita Reila alipofikisha miaka 18 Lincoln akamwambia Reila kuwa si unaona mimi na mama yako wote waswahili na wewe muhindi... Akamwambia kuwa tulikuchukua katika kituo cha kulelea watoto yatima tunakulea kama mtoto wetu, wakati wote toka Reila anapata akili Wankyo alikuwa hampendi Reila kabisa pamoja na kuwa ni mtoto wake wa kumzaa Reila hakuwahi kuoneshwa upendo na mama yake hata kidogo, upendo aliokuwa anapata ni kutoka kwa baba naye ni Lincoln.
Bac bana maisha yakaendelea Reila nanunuliwa kila kitu, outing za kutosha na baba yake.Reila alikuwa mzuri balaa baba akanza kummezea mate Reila Khe Lincoln si akamtongoza bintiye Reila , sijui ikawaje Reila akakubali dah bwana Lincoln akawa anakula tunda zuri alilolitunza mwenyewe dah.
Sasa bwana yule muhindi Kareem baba wa Reila muda wote alikuwa anaendelea na maisha yake lakini akijua Reila ni bintiye ila akabaki pembeni akijua Lincoln bwege anamlelea bintiye. Akimwita mume bwege. Ila akaja kugundua kuwa Lincoln kaamamua kutembea na bintiye hadi kumtia mimba....
Kareem si kuchanganyikiwa huko dah sasa Lincoln si ndio kapata kiburi kaanza kumwita Kareem mkwe dah
Sasa hapa mwenye roho mbaya sijui nani maana kugongewa mke inauma ila mwenye mke kuamua kukulea binti yako na kutembea na huyo mtoto inauma nayo loh
Hii stori nimeangalia leo bongo movie inaitwa "Fedhea" youtube chini na producer Lucy Komba