Kubenea na Jacob 'wasambaratisha' uchunguzi Kinondoni

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,136
17,871
Kufuatia kutolewa hadharani kwa mikataba ya kuuzwa kwa Fukwe ya Coco, uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazomkabili Mhandisi Musa Natty umekwama. Mhandisi Musa Natty alikuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni kabla ya kuhamishiwa Mji wa Babati kuwa Mkurugenzi. Alisimamishwa kazi kupisha uchunguzi juu ya tuhuma zinazomkabili.

Kati ya tuhuma hizo ni ujenzi mbovu wa barabara za Manispaa ya Kinondoni pamoja na uuzwaji wa kifisadi wa fukwe za Coco. Baada ya kujitokeza kwa Saed Kubenea (Mbunge wa Ubungo-CHADEMA) na Boniface Jacob (Meya wa Kinondoni na Diwani wa Ubungo-CHADEMA) na kuanika mkataba wa fukwe za Coco, uchunguzi 'umevurugika' na kusimama.

Kubenea na Jacob waliapa kusimama kidete kumtetea asiyehusika na kutaka wahusika halisi waanikwe na kushughulikiwa. Wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanaona kuwa Kubenea alianza mivutano na mamlaka na wafuasi wao mbalimbali. Ndiyo maana, Kubenea amekuwa akishambuliwa kimaneno na kubanwa.

Kubenea sasa amekuwa akizungumzwa vya kutosha kufuatia 'kujitoa muhanga' juu ya kashfa za Kinondoni. Uchunguzi unasuasua. Nani anaogopwa? Filamu inaendelea!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Kitanzi kingine kwa JPM hicho!?!?
 
Kweli Side anawapa shida sana,ndo maana wanakosa sababu na kuanza kudadisi juu ya elimu yake,huku wengine wakienda mbali kwa kudai kuwa hana elimu ya kutosha,lakini cha kustaajabisha ni namna anavyoweza kuwabana wapiga dili na kuwatisa jsmbajamba japo watu wanamponda!!!!!
 
Kitanzi kingine kwa JPM hicho!?!?

Nimekipenda sana hicho kitanzi maana huyu mzee hafuati kabisa utawala wa kisheria. Asemacho anataka kiwe sawa tu sku zote. Big up sana Side.
 
Safi Kubenea tunataka wahusika halisi ambao ni viwavi wa lumumba.

Uscheke na kima kabisa kwenye suala la maendeleo na kwenye ukweli besti angu Kubenea, elewa tu mti wenye matunda ndo hutupiwa mawe sku zote, ungeua fara wala wasinge shughulika na wewe wala kukusemasema kiaina. Kaza buti sana mwana.
 

Hata kama hana Elimu mradi anafanya vitu vya maana ni poa tu. kwanza si wanasema mbunge ajue na kusoma na kuandika tu natumaini jamaa anaweza soma na kuandika.
 
Namkubali sana Kubenea na Viongozi wa ngazi zote UKAWA. Ni waelewa kabisa wakisema wanajua wasemacho.

Tunataka Sangara wawajibshwe na siyo vidagaa kama ilivyo kuwa kesi ya EPA.
 
Namkubali sana Kubenea na Viongozi wa ngazi zote UKAWA. Ni waelewa kabisa wakisema wanajua wasemacho.

Tunataka Sangara wawajibshwe na siyo vidagaa kama ilivyo kuwa kesi ya EPA.
wizi,ubadhirifu na dhuluma ya viwanja vingi kinondoni vilifanywa na vibopa wa ccm na serikali yake leo mnatuletea muziki wa Saed kwamba hana elimu sisi hatutaki kusikia habari za kupotosha ukweli juu ya uuzwaji wa fukwe ya coco bichi mtaanikwa hivi karibuni wananchi watawajua wote kwa majina yenu mnajifanya kubebesha mizigo watu wengine mliofanya wizi mnajuana subirini mtamjua Kubenea ni nani?
 
Kama Natty alikuwepo wakati hizi barabara za Kinondoni za kukaa miezi 6 halafu zinakufa kabisa zinajengwa, sijui kwa nini kina Kubenea wanamtetea. Mfano barabara za kijitonyama za Akachube na ile ya polisi Mabatini, ni aibu tupu.
CDM wawe makini na kutetea hawa watu, wasiishie kusema Natty hausiki tu kwa vile alikuwa team UKAWA, wasema nani anahusika na je wao ni sahihi Coco kuuzwa?
 
visasi vya jp
 
Uscheke na kima kabisa kwenye suala la maendeleo na kwenye ukweli besti angu Kubenea, elewa tu mti wenye matunda ndo hutupiwa mawe sku zote, ungeua fara wala wasinge shughulika na wewe wala kukusemasema kiaina. Kaza buti sana mwana.
na sasa hivi wamempeleka kamati ya bunge ya huduma za jamii ndio watakoma maana sekta hiyo ni mtambuka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…