Kubanwa na Bukta kulisababisha Mwakinyo kushindwa kumpiga KO mpinzani wake

Umkonto

JF-Expert Member
Dec 27, 2018
2,401
4,205
BONDIA Hassan Mwakinyo amesema sababu ya kutokumpiga kwa KO, Muvesa Katembo wa Afrika Kusini ni kutokana na bukta yake kumbana.

Katika pambano hilo lilofanyika juzi katika Uwanja wa Jamhuri Jijini hapa, Mwakinyo alishinda kwa pointi ambapo jaji namba moja alimpa pointi 77-74, wa pili 76-75 na watatu 77-74.

Mara ya mwisho kwa Mwakinyo kuingia ulingoni ilikuwa Septemba 3, mwaka jana ambapo alipambana na bondia Liam Smith mjini Liverpool na kupoteza kwa TKO katika raundi ya nne.

Mwakinyo aliyewahi kuingia kwenye 20 bora ya dunia kwenye uzani wa superwelter na namba moja nchini kwenye kila uzani ‘pound for pound’ ameporomoka kote na sasa ni wa pili nchini na wa 66 duniani.

Akizungumza mara baada ya mchezo huo, Mwakinyo alisema sababu ya kutopata matokeo mapema na kushindwa kupata TKO ni kutokana na bukta kumbana.

"Bukta ilikuwa inaninyima uhuru wa kunyanyua mguu, kikubwa nashukuru nimeshinda, nawashukuru mashabiki wamejitokeza kwa wingi licha ya mvua iliyokuwa ikinyesha," alisema Mwakinyo.

Alisema baada ya ushindi huo anajiandaa kwa mchezo unaofuata ambapo atapanda ulingoni Juni 24, mwaka huu kucheza na bondia mkubwa ambaye hakumtaja jina.

Kwa upande wake, Katembo alisema Mwakinyo ni bondia mzuri na ameyakubali matokeo hayo huku akilalamika sehemu ya kuchezea ilikuwa ikiteleza.

Chanzo: Gazeti la Mwanaspoti

Maoni Yangu;

Mwakinyo afundishwe kuongea na vyombo vya habari ili kutoa sababu zinazoeleweka, kuliko anavyofanya kutoa sababu dhaifu.

Kule Uingereza alipigwa akasingizia viatu.

Leo kashinda kwa pointi anasema kwa sababu alivaa bukta ya kumbana.

Sasa bondia mkubwa kiasi hicho anavaa bukta ya kumbana siku ya pambano, kwani kule mazoezini huwa havai bukta?

Au begi la bukta lilisahaulika Tanga, hivyo akapewa bukta ya kumbana?

Na kama alipewa bukta ya kumbana, je hapo Dodoma alishindwa kwenda kununua madukani au mitumbani bukta pana baada ya kujaribu bukta aliyopewa na kumbana?

Mbona mwenzake katoa hoja kwamba, ameshindwa kwa sababu uwanja ulikuwa unateleza. Sababu hii ipo kwa waandaji, lakini hoja ya bukta ni ya bondia husika.
 
Posts za Mwakimyo kwenye social networks ni tambo na majigambo yasiyo ya lazima. Maneno yake kwenye press, ni kituko!

Ninaanza kua na wasiwasi na uwezo wake. Mambo ya kusingizia viatu na bukta, nilitegemea kuyaona kwa Mandonga, sio Mwakinyo!
 
Kabisa.
 
BONDIA Hassan Mwakinyo amesema sababu ya kutokumpiga kwa KO, Muvesa Katembo wa Afrika Kusini ni kutokana na bukta yake kumbana.

Katika pambano hilo lilofanyika juzi katika Uwanja wa Jamhuri Jijini hapa, Mwakinyo alishinda kwa pointi ambapo jaji namba moja alimpa pointi 77-74, wa pili 76-75 na watatu 77-74.

Mara ya mwisho kwa Mwakinyo kuingia ulingoni ilikuwa Septemba 3, mwaka jana ambapo alipambana na bondia Liam Smith mjini Liverpool na kupoteza kwa TKO katika raundi ya nne.

Mwakinyo aliyewahi kuingia kwenye 20 bora ya dunia kwenye uzani wa superwelter na namba moja nchini kwenye kila uzani ‘pound for pound’ ameporomoka kote na sasa ni wa pili nchini na wa 66 duniani.

Akizungumza mara baada ya mchezo huo, Mwakinyo alisema sababu ya kutopata matokeo mapema na kushindwa kupata TKO ni kutokana na bukta kumbana.

"Bukta ilikuwa inaninyima uhuru wa kunyanyua mguu, kikubwa nashukuru nimeshinda, nawashukuru mashabiki wamejitokeza kwa wingi licha ya mvua iliyokuwa ikinyesha," alisema Mwakinyo.

Alisema baada ya ushindi huo anajiandaa kwa mchezo unaofuata ambapo atapanda ulingoni Juni 24, mwaka huu kucheza na bondia mkubwa ambaye hakumtaja jina.

Kwa upande wake, Katembo alisema Mwakinyo ni bondia mzuri na ameyakubali matokeo hayo huku akilalamika sehemu ya kuchezea ilikuwa ikiteleza.

Chanzo: Gazeti la Mwanaspoti

Maoni Yangu;

Mwakinyo afundishwe kuongea na vyombo vya habari ili kutoa sababu zinazoeleweka, kuliko anavyofanya kutoa sababu dhaifu.

Kule Uingereza alipigwa akasingizia viatu.

Leo kashinda kwa pointi anasema kwa sababu alivaa bukta ya kumbana.

Sasa bondia mkubwa kiasi hicho anavaa bukta ya kumbana siku ya pambano, kwani kule mazoezini huwa havai bukta?

Au begi la bukta lilisahaulika Tanga, hivyo akapewa bukta ya kumbana?

Na kama alipewa bukta ya kumbana, je hapo Dodoma alishindwa kwenda kununua madukani au mitumbani bukta pana baada ya kujaribu bukta aliyopewa na kumbana?

Mbona mwenzake katoa hoja kwamba, ameshindwa kwa sababu uwanja ulikuwa unateleza. Sababu hii ipo kwa waandaji, lakini hoja ya bukta ni ya bondia husika.
Mwakinyo ni bondia, asie weza kufikiria kwa anachoongea,ni mropokaji bila kutafakari....

Mwakinyo inabid atafute mtu wa kuongea badala yake, nimesikiliza press nying zake, huwa anaongea uyumbo mtupu

Sent from my M2010J19SI using JamiiForums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom