Shemasi Jimmy
Member
- Apr 23, 2021
- 93
- 104
Na Shemasi Jimmy 0659 611 252
Halleluja watu wa Mungu, maandiko yanasema apendaye mafundisho hupenda maarifa, karibu tujifunze kwani elimu haina mwisho. Leo tutajifunza kwa habri ya kukubali kukaa chini ya mchakato au maandalizi katika kuelekea hatima ya ndoto zako huku tukimtazama Yusufu, Daudi na mtume Paulo kama mifano katika somo letu.
Mojawapo ya changamoto inayotuandama vijana wa sasa ni uwepo wa vipaji(karama) vikubwa na vizuri sana ndani yetu lakini hatupo tayari kukaa chini ya mchakato na kujifunza. Ni kweli unauwezo mzuri wa kuhubiri, unauwezo wa kuimba, lakini je, upo tayari kukaa chini na kujifunza? Kule kukaa na kujifunza ndio kitu pekee kitakachokufanya uelekee katika hatima ya maisha yako.
Kitu kikubwa alichokiweka Mungu ndani yako si dhamana ya kukupeleka kwenye Hatima, Ni kweli unakipaji, ni kweli una-potential ambayo Mungu ameweka ndani yako lakini kama hujaandaliwa vema haita kuwia rahisi kufikia lengo lako. Daudi anapakwa mafuta kwenda kuchunga kondoo na si kua mfalme,Taz 1 Samweli 16:13.hii inatufundisha kua na subira, kua wavumilivu, kua wanyenyekevu hata kama kuna mafuta Mungu amekwisha mimina kwako.
Nataka nikwambie kwamba mtume Paulo anayetajwa kuandika vitabu 9 kati ya vitabu 27 vya agano la kale, moja kati ya mitume waliofanya kazi kubwa ya kuhubiri injili, lakini baada ya kukutana na Yesu ilimpasa kukaa katika mchakato au maandalizi kwa miaka 12 kabla hajaianza rasmi kazi yake ya injili. Ndugu yangu, mambo mazuri hayatokei kwa bahati mbaya, hutaftwa. Wenye hekima wanasema yatupasa kutafta hekima kama tutaftavyo FEDHA AU DHAHABU. (Mit 23:23). Kubali kutafta maarifa ili uongeze uwezo(Mit 24:5)
Biblia inamtaja Daudi kama mmoja kati ya wafalme bora kuwahi kutokea katika dunia hii. Naamini daudi asingekubali kua chini ya mchakato na akaingia ikulu baada ya Mungu kumtia mafuta ya mwanzo angekua moja kati ya walfme wabaya kupata kutokea. Uvumilivu, unyenyekevu na moyo wa ustahimuvu ndio umemfanya kua bora katika utawala wake.
Daudi alipakwa mafuta mara TATU (1Samweli 16:13, 2Samweli 2:4 na 2Samweli 5:3).Mafuta ya Mara ya kwanza naya pili hayakumwezesha Daudi kuingia ikulu, masihi wa Bwana anapakwa mafuta na kwenda kuchunga kondoo, ni jambo la ajabu lakini ndio uhalisia.
Yusufu alikua na ndoto ya kua mtu mkubwa, ndoto hiyo aliota akiwa na miaka 17 lakini ndoto inakuja kutimia akiwa na miaka 30.
Haijalishi unaona mambo makubwa kwa kiasi gani lakini usipoanza kuyaishi hivi leo,hakuna wakati yatakuja kutokea kama muujiza kwenye maisha yako. Lazima uanze kutengeneza njia kuelekea kwenye maisha ya ndoto zako. Maji bila mfereji ni uharibifu sawa kabisa na kipaji bila malezi. Kubali kuandaliwa ili pindi maono yako yatakapo kua halisi uanze kuyaishi bila kuumiza wengine wala kumuacha Mungu.
Watu wengi ndoto zetu zimepotea kwa sababu hatukuanza kuziishi zile ndoto mapema au hatukukaa kwenye mazingira ambayo yangetufanya tuziishi zile ndoto au hatukua na taarifa sahihi juu ya nini kifanyike ili uweze kufikia hatima ya maisha yetu.
Kata sasa kufanya mambo bila ufahamu sahihi, tafta ufahamu na maarifa sahihi ya ndoto zako, kataa leo kua mtumwa wa mihemuko na hisia. Kubali kuongozwa na wenye ufahamu wa kile unachokipenda huku ukijifunza kwa unyenyekevu na moyo wa hekima.Dunia imejaa kila kitu kitakachokuwezesha kufikia ndoto zako na kuishi kwenye hatima ya maisha yako.
Mungu akubariki sana kwa kusoma chapisho hili na uwe na wakati mwema.