KUB Mbowe kitanzini Dodoma,wafuasi wamuonya asiposusa kweli watampopoa!

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,999
Na Rwabukambara Projest

Kiongozi wa kambi rasmi bungeni na mwenyekiti wa CHADEMA Mh.Freeman Mbowe huenda akakosa ushawishi kutoka kwa wafuasi wa siasa za upinzani endapo atashindwa kutekeleza kauli yake ya kutohudhuria vikao vyote vitakavyoongozwa na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Dr.Tulia Ackson.

Wafuasi hao ambao waliongea na mwandishi wa habari hizi huku wakionekana kukerwa na tabia ya Mbowe kutokuwa na msimamo na maneno anayoyasema.

Mfanyabiashara wa mitumba aliyejitambilisha kwa jina la Masawe aliwaambia wenzake mbele ya mwandishi "Washikaji kuna haja sasa na Mbowe na baadhi ya viongozi waadhibiwe,leo hii CHADEMA tunaandamwa kama tulishawahi kushika dola?...hii haikubaliki" aliendelea kulalamika "Mbowe anakosa msimamo anagoma jioni alafu asubuhi anaingia bungeni huu ni usanii na tukiulea itakula kwetu".

Kijana mwingine aliyetambisha kwa jina la Mapinduzi alisikika akisema "sasa leo Mbowe anasema watasusia vikao vyote vitakavyoendeshwa na Naibu spika,hili haliwezekani ndugu zangu,Je kama Tulia akiedesha vikao vyote vilivyobaki itakuaje?,hii kajiweka kwenye mtego wa CCM" alindelea kulalamika "hata sisi ambao hatujasoma na sio wabunge tunajua hii ni hadaa na ndani ya muda mfupi tutaumbuka,japo nasubiri nione kama watatekeleza"

Aliyewahi kuwa kiongozi na Mbunge wa CHADEMA (jina linahifadhiwa) akiongea na mwandishi wa habari hizi alisema "Siasa za upinzani zinayeyuka kwa kukosa mwendelezo (consistency) wa hoja na wabunge wengi wanafanya siasa za kushambulia watu na sio hoja hivyo wanayemshambilia akiondoka hoja inakufa" mwanasiasa huyo mkongwe alitoa mifano ya hivi karibuni "angalia suala la Lugumi,kuondoka Kitwanga limekwisha ninachokuambia Bwana mdogo upinzani ni lazima uwe na hoja chache za kusimamia na kuziendeleza" alindelea kusema "ni kweli suala la bunge live linamashiko lakini sio muhimu na si hitaji la wananchi wengi kama linavyokuzwa,hizi siasa za kila hotuba ya upinzani kuwa na hoja za bunge live na kudhulumiwa uchaguzi ni dalili za wabunge kutofanya kazi yao,haiwezekani wabunge 100 kuongelea suala hilo hilo" alihoji.

Baadhi ya vijana wa soko kuu hapa Dodoma walionyesha kukerwa na tabia ya kukosa msimamo kijana Selemani Jumbe alisema kinachotokea sasa ni lazima tumpopoe Mbowe akiendelea kutuhadaa,maneno matupu hayavunji mfupa ndugu mwandishi"alimalizia kwa kusema sisi tunaendelea kufuatilia mwaka 2020 sio mbali migomo haileti maji wala barabara".

Nawasilisha kama nilivyokopi.Tujadili kwa upendo.
 
Huu uandishi unatia shaka sana kwani Inaonekana kama hadithi bila kianzio mbadala cha Hadithi hadithi na kiitikio chake hadithi njoo utamu kolea. Kijana mmoja muuza mtumba hapa dodoma, ehee, na kiongozi mmoja aliyekuwa mbunge wa chadema, ehee, wamesema ehee (naomba wengine mmalizie kama mmeielewa hii hadithi)
 
Ajira46, na nawahakikishieni hizo ajira mtapewa ila mtatumbuliwa baada ya muda mfupi sana, akili mzigo.
 
Hata mwaka jana wakati wa kampeni CCM mlichapisha T-SHIRT za CHADEMA na kujifanya wanaCHADEMA mkiwa mnaandamana "ETI" kupinga MHESHIMIWA WAZIRI MKUU EDWARD LOWASSA kuwa mgombea wa urais kupitia CHADEMA lakini mkasambaratishwa kwa kichapo kutoka kwa RED BRIGADE. Sasa rudieni tena muone! RED BRIGADE hapo Dodoma kaeni mkao wa kujenga uzalendo. Chalaza wote watakaowaletea vurugu wabunge wetu wazalendo.
 
Naona mwandishi ya habari hii kakurupuka!
 
Naona hata kwenye kikao cha bunge leo ambapo naibu spika anaongoza kina Mbowe hawapo
 
Vibaraka wenye nia ya kudhoofisha upinzani ndani na nje ya Bunge Hamna jipya, tatizo hamjitambui wala hamtambui haki zenu kama watanzania....poleni
 
Ila km kuna ukweli vile.
Walisememaga hawataingia mpk bunge liwe live, mara hawamtambui rais, sijui na hii itaishia wap, ngoja nichek usannii huu
 
Mtoto mzuri umeielewa hadithi na kuifanyia ufupisho. Haya fanyia kazi uliyoelewa.
 

Source ?Gazeti gani?Chombo Kipi cha Habari ?nimekuambia Mkuu acha kukurupuka
 
Nawasilisha kama nilivyokopi.Tujadili kwa upendo.
Ulivyokopi wapi?umekopi kutoka wapi?
Hiyo hapo juu inahusiana nini na kutohudhuria kwa vikao vitakavyoendeshwa na Tulia?Hotuba za upinzni zinahusiana nini na kutohudhuria vikao vinavyoendeshwa na Dr. Tulia?Kwa Mujibu wa Mwandishi wa nini?

Yaani unakurupuka mpaka unatia aibu anyways alabda sababu umecopy
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…