Kuanzishwe kodi mpya na ikatwe sh 1000 kwa kila mwezi kwa kila mwenye line ya simu kama sehemu ya income tax

Dennis Roberts

JF-Expert Member
May 30, 2024
808
916
Mtu mwenye line atakua analipa sh 1000 kwa mwezi na sh 12000 kwa mwaka kama income tax

Hatakama watu wanaiba fedha haitaondoa ukweli bado makusanyo yetu ni madogo sana


Usisahau kushare video na mwenzako
 
Mtu mwenye line atakua analipa sh 1000 kwa mwezi na sh 12000 kwa mwaka kama income tax
Usisahau kushare na mwenzako
View attachment 3306110
😅😅😅😅

Hoja yako siyo mpya.

Imewahi kupendekezwa na Zungu, Naibu Spika.

Ikashindikana.


CCM imewahi kuchungulia miamala ya Mpesa, Tigo pesa inapitisha trillions ikaweka Tozo juu ya Kodi, watu wakaanza kukwepa kutumia miamala ya simu, serikali ikapunguza ila bado ipo ipo.

Lakini pia, hoja yako ni ya kizuzu na ya kukwepa uwajibikaji.

Kila vocha mtu anayonunua inakatwa VAT.

Kwenye elfu 1000, kuna Kodi ya 300.

Na vocha ni moja. Ukinunua nyingi, kila siku ni zaidi ya hiyo 1,000.

Lakini ulivyo, kiazi watu wanatumikiswa kwenye viwanda bila mikataba huoni tatizo, ila tatizo unaliona ni watu walipe 1000 kwa serikali na siyo kuweka masharti kwa wamiliki wa viwanda kutoa mikataba ili watu walipe kodi.

Hoja nyingine ya ovyo, eti kwa watanzania milioni 60. Qquma kabisa, hiyo 60 ni mpaka watoto wadogo.

Watu wenye nguvu ya kufanya kazi wanaoingiza kipato hawazidi 30 milioni.
 
Jikite kwenye mada hamnaga tuzo ya matusi
Mkuu Kuna vyanzo vingi vya mapato hatupaswi kuweka tozo kwenye line.

Kuna
Bandari
Mbuga
Madini
Maziwa/mito/bahari
Ardhi yenye rutuba
Wanyama adhimu/adimu

Tuna kila kitu Cha kutufanya tuendelee bila kuitaji Kodi za kwenye laini..ni uvivu TU wa kufikiria.

Naomba tufunge mjadala huu kwa Sasa otherwise tegemea matusi kwa wote wanao jitambua.

Au mtafute mchumi mwigulu umnongo'oneze hili Jambo lako 😅🤣
 
Jikite kwenye mada hamnaga tuzo ya matusi
Mkuu, kuna issue serious kabisa za kuzungumzia...kwanini umechagua tatuzi hili ambalo ni mwiba kwa wanyonge wengi.

Ebu tumpe suluhu ya matatizo makubwa kama hayo ya wizi na madeni makubwa yasiyoingia kwenye manufaa ya kitaifa ila mifukoni mwa watu.

Nadhani uko kwenye process ya kujiandikisha kuwa CHAWA sio?
 
Back
Top Bottom