The tireless Hunter

New Member
Oct 21, 2016
3
0
Ndugu habari,

Nimemaliza chuo mwaka jana sasa nina shahada ya kwanza ya Ualimu katika masomo ya Hisabati na Kompyuta. niliporudi nyumbani mwaka huu niligundua kuna fursa ya kuzoa taka katika mitaa ya kata yetu. Hivyo sikuchelewa nikachapa barua fasta na kuipeleka kwa mtendaji wa kata nikiomba kazi ya kuzoa taka kutoka kwenye mitaa kwa lori kisha kuzipeleka dampo lililotengwa .

Nashukuru Mungu Mtendaji wa kata alipokea na kuisoma barua yangu na kunishukuru mno kwa wazo hilo nakusisitiza vijana tunatakiwa kuwa hivo. Basi katika kuandika barua hiyo nilikuwa mwenyewe kama unavojua jinsi ilivyo kazi kupata washiriki wakati bado jambo ndio linaanza basi sikutaka kusubiri saana kuhusu hilo lakini mwishoni mwa barua yangu nilisema hivi "Hivo basi mimi kama mdau wa mazingira nilikuwa na wazo la kuunda kikundi cha vijana wasio zidi watano au zaidi kama itabidi ambacho kitahusika katika ukusanyaji wa taka zote zilizohifadhiwa katika mifuko au vyombo vya kuhifadhia taka majumbani na maeneno mbalimbali kwenye mitaa kwa lori kisha kuzipeleka katika dampo lililotengwa na serikali ya kata kulingana na siku zitakazopangwa ndani ya wiki au mwezi"

Basi baada ya hapo Mtendaji wa kata alinitaka kuhudhuria kikao cha "ODC" ili nikaseme wazo hilo mbele ya hao wakubwa kwani kikao kingefanyika siku chache mbele, nilijiandaa nikahudhuria kikao hicho . Nikasema wazo lote mbele ya kikao kila kiongozi akisikiliza nilipomaliza Mh Diwani alifurahishwa na jambo hilo pia alinitaka nionane nae siku iliyofata nikiwa na hao vijana wengine. basi baada ya kuwa wazo limekubaliwa niliondoka kwenda kutafuta vijana wanne ambao pia niliwatambua kabla ilikuwa rahisi kuwapata kwani niliwaambia stori yote. kwa kifupi tuliambiwa tutengeneze kikundi na katiba yake ili waende kutusajiria wilayani. Mpaka sasa tupo kwenye mchakato huo.

Ingawa kikundi kitahusika na usafi lakini mimi kama muanzilishi ninayo maono makubwa sana kwani tutaanzisha miradi mbalimbali ilikutengezeza ajira na kipato zaidi.

Tulichagua viongozi mimi nikachaguliwa kama Mwenyekiti wa kikundi, lakini muda wa uongozi tulipendekeza miaka miwili

Sasanaomba msaada wenu , ikiwa mimi kama muanzilishi na mbeba maono kama unavyo ona jinsi nimepambana kutoka kuwa wazo hadi kuwa kikundi je ningestahili yapi kwenye kikundi hicho ? (kuanzia uongozi na maslahi)
Je ishu ya uongozi kwangu ingewakwaje hapo?

Je, uongozi wangu unafaa kuwa na ukomo? kama ndio baada ya kuwa uongozi wangu umekoma , nitabaki kuwa nani kwenye kikundi?

Nomba msaada wenu wa mawazo kabla kikundi hakijasajiliwa.
bBn
 
Hongera kwa wazo hilo zuri na hongera sana kwa uthubutu wako na ujasiri wa kuchangamkia fursa. Vijana wengi fursa wanaziona ila ujasiri wa kuziendea unakuwa kikwazo

Nakumbuka miaka kadhaa baada ya kumaliza chuo tuliwahi kuwa na wazo kama hilo japo lilikuwa kwa namna tofauti kidogo. Sisi tulilenga zaidi kutoa elimu, kuhamasisha na kuishirikisha jamii kwenye swala zima la kutunza mazingira japo kipengere cha kuzoa taka kilikuwa ndani yake

Muundo wa kikundi chetu kile haukuwa na tofauti na huo wa kwenu na vikundi vingi vina muundo huo wa uongozi

Kwa haraka nachokiona kwako ni hofu kwamba huenda wazo ulilolibuni huko mbele likamilikiwa na wengine

Kikundi chochote au kampuni yoyote unayoiona ilikuwa na mwanzilishi/mtoa wazo.

Mimi sio mtaalamu wa vikundi ila nadhani kwa maana ya umoja/kikundi mko sahihi kwasababu kikundi hakiwi mali ya mtu.

Ndiomaana hata kikundi chenu kikishajitanua mtahitaji kuwa na signatories (hauwezi kuwa peke yako), mkitaka kuomba mkopo mtahitaji kuonyesha usajili na katiba (hauwezi kuwa peke yako)

Vinginevyo ulitakiwa uunde kitu kingine chenye hatimiliki halafu hao wengine wawe kama umewaajili.

Lakini hapo haujawaajili ila mnashirikiana.

Pamoja na hayo wataalamu wa katiba za vikundi wanaweza kukusaidia kuongeza kipengere kinachotamka maslahi yako ya kudumu wewe mwenye wazo kwenye kikundi. Hii naamini inawezekana
 
Hongera sana Mkuu kwa wazo zuri na utashi huo.

Hutakiwi kuanza kufikiria maslahi yako binafsi kama muanzilishi hii mwishowe itapelekea kuvunja kikundi. Nakushauri jitume, onesha haiba ya uongozi, ongeza ubunifu kwa kubuni miradi zaidi ya kikundi, kuwa muwazi, epuka ubadhirifu, usiwadharau wenzio na kujiona wewe msomi zaidi yao, wathamini wote kwa usawa, kubali kukosolewa na kushauriwa naamini hutotumia nguvu kuendelea kuaminiwa na kuwa kiongozi.

Naona kama unataka kutanguliza maslahi yako kwanza kabla jaya hamjaanza kazi, hii sio nzuri.
 
Back
Top Bottom