Kuanzia leo naacha kula Samaki wa Mwanza

Nebuchadinezzer

JF-Expert Member
Oct 1, 2018
1,403
2,546
Leo ndio nimegundua kwanini kanda ya ziwa inaongoza kwa kesi nyingi za kansa...na magonjwa ya matumbo.

Maelfu ya samaki wameonekana wakielea juu ya mto Mara inasemekana wamekufa kutokana na athari za sumu zinazomwangwa ktk mto huo kutoka mgodi wa North Mara.

Serikali ipo wapi?

Hii issue ingetokea Ulaya, sasa hivi ingekuwa issue nyingine.

Serikali haijali afya ya watu wake...kuna faida gani ya kuwa na wawekezaji wanao hatarisha maisha ya raia?

No one Cares, kuanzia leo Sato Sangara bye bye.
 
Utakula wa wapi kusiko na taka tiririka za viwandani? Ukitaka kupinga tafiti fanya tafiti
Ameandika hatakula samaki wa Mwanza kwa sababu ameona samaki wakielea kwenye mto Mara kwa sababu ya sumu za mgodi.

Samaki wa ziwa Victoria atakula ila sio wa kutoka Mwanza k0nd00 hii
 
Ongezea na hutotumia tena maji ya ziwa Victoria. Maana ndipo hao samaki hutolewa
 
kila jambo ni hatari kwa afya ya mwanadamuu, kikubwa mengi huwa hayaonekani katika ulimwengu wa mwiliii

maeneo mengi ungekuwa unafahamu vyakuli tulavyo vinaandaliwaje nadhani wengi tungekuwa tukirejea homu kula ama kubeba vyakula na kutoka navyooo
 
Sukuma gang mko wapi?
Japo siyo ila kwa niaba yao nasema...

TUPOO HAPAAAA...

Ahahahahaa, ndg Alli Hapi mkuu wa mkoa wa Mara kama upo humu au msaidizi wako hebu fuatilieni hili kama ni kweli basi ofisi ya makamu wa rais upande wa mazingira tieni mguu hapo.

Hao North Mara wanapesa so wanafanya makusudi mazito kuua maliasili ya nchi na kuharibu afya za raia.
 
Ina maana environmental impact assessment haikufanyika hadi kemikali za migodi ziweze kuingia kwenye mkondo na kwenda kwenye vyanzo vya maji kwa matumizi ya binadamu na ambamo viumbe mbalimbali ikiwemo samaki wanaotumiwa kama chakula cha binadamu wanakaa.......pollution kwenye maji ya ziwa viktoria ipo juu kutokana na mamlaka kushindwa kusimamia sheria za kimazingira kuzunguka ziwa hilo. Ni wakati sasa mamlaka zisimamie sheria na hao wenye migodi wanyang'anywe leseni na kufilisiwa kwa kuelekeza kemikali kwenye vyanzo vya maji ya matumizi ya binadamu kwa makusudi kabisa, kule kwao hawawezi kufanya hivyo hata kwa bahati mbaya...........​
 
Watanzania wana matumbo ya chuma weewe , watu wanagangonga sumu tangu enzi za machimbo ya mwadui miaka ileee lakini wako imara kama chuma hadi leo hii, kimsingi mienendo ya maisha ya watu wengi hasa kipindi hiki ndio chanzo kikubwa cha magonjwa wala tusisingizie samaki , vyanzo vya magonjwa miaka hii ni vingi mno , life style na ulaji wa hovyo ndio vinachangia saaaana, unakuta watu wamefuga vitambi utadhani wanafanya mashindano ukiuliza umri wengi hata 20 hawajafikisha, kimsingi ni disaster.
 
Ni utapiamlo wa akili kuamini kuwa Tanzania ina Serikali.Mleta uzi jiangalie sana na chunguza akili yako kama ipo sawasawa.

Vibaka ambao muda wote wako busy kutafuta visingizio pamoja na chaka la kuficha madhaifu ya kikundi chao ndiyo unawaita kuwa ni Serikali?

Unaelewa kuwa vibaka hawa ambao wewe unawaita kuwa ni Serikali juzi wameibuka na kudai kuwa bidhaa kama vile mafuta ya kula zimepanda bei kwa sababu ya vita ya Russia wakati sasa hivi ni miaka miwili bidhaa hizi bei ipo juu?
 
Back
Top Bottom