Ok, mkuu mtoa mada kwanza naheshimu Mawazo yako, Ni Mawazo mazuri coz ile kuwaza tu ni hatua moja mbele, sijui uzoefu wako katika hili ila ntajaribu kutoa darasa kidogo ili na watu wengine ambao wapo interesting hata wakichangia wajue wanachangia nini!
Movie na Film ni the same, utofauti ni kuwa neno Film lilitumika miaka hiyo wakati wakitumia film kwa maana ya tape ku record, kuanzia zile film (tape) kubwa, mpaka kuanza kutumia Div miaka ya hivi karibu ambapo sasa Camera zimekua na uwezo mkubwa na nyingi zinatumia Memory Card tu kuhifadhi kile unacho record..
Kuna utofauti kidogo Kati ya Short Film na Series! Short film kwa kuokoa nguvu na muda ni aina ya film ama Movie yenye mwanzo Kati na Mwisho, lakini inapokuja kwenye Series huwa haina mwisho otherwise ni uwamuzi wa Producer mwenyewe kuamua Series yangu itaishia hapa! Ila inaweza kuendelea hata miaka 50 kama Producer atapenda.
Kwenye Series huwa kuna Scene, Episode, Season.....kila Scene kadhaa ni sawa na Episode kadhaa, na kila Episode kadhaa zinakamilisha Season moja! Kwenye Series huwa kuna Episode ambayo huisha kila baada ya 45 mins, kwa wenzetu baadhi ya Series kama Merlin kila Episode inaanza na kisa chake mpaka kinaisha, ikianza Episode nyingine inaanza na kisa kingine n.k.....
Mkuu mtoa mada nije kwako, kabla ya kuandaa Series Movie cha kwanza fikilia soko lako, ni la watu wa aina gani? La ndani ama nje? Kama ume target soko la nje basi lazima utizame story yako, (story ni kwanza kabla ya Quality ya Video) Je! Hiyo story inaweza kuleta ushindani huko International markets? Kama jibu ni ndiyo basi tafuta Wataalam waandae Script, (kumbuka Script ndo Movie) mtu wa kwanza kabisa anayeiona Movie ni Script writer.
Kwa series wanaweza kuwa hata writers 5, 24 hrs imeandikwa na Script writers zaidi ya 7, na wote wamepita mule mule, Script writers lazima wawe na uwezo mkubwa, wenye muono wa mbali, elimu pia, Script ikikamilika mnakaa wadau kupendekeza Director, mtakua na vigezo vyenu all in all lazima awe na uzoefu na uwezo mkubwa, wapo Directors wachache wana uwezo ila Producers ndo wanaharibu!
Mkimpata Director atapitia Script atakuja na Mawazo au Mapungufu, mtayafanyia kazi mtaenda na hatua ya kuunda Crew, kumbuka Kila mtu Ana mipaka yake, Director ni kama vile Coach kwenye team ya mpira, yeye ataunda team yake kuona nani ataweza kumsaidia vizuri, assistance director, location manager, Continuity, n.k, atawaleta kwa Producers kwa makubaliano mengine hasa mkwanja! Ikipita mnaenda hatua inayofuta............
Ngoja niishie hapa ntarudi!