Kuagiza gari kupitia kutoka japan

piego

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
289
425
habari wakuu
naomba mods msiunganishe uzi huu na nyuzi nyingine za magari ili ipatikane information specific to the topic

nina plan ya kuagiza gari kupitia mtandao wa realmotor.jp . maswali yangu ni haya
1. je ni mtandao wa kuaminika? na vipi wanaprotect buyers from hackers maana naona mawasiliano yao ni kupitia website yao pekee.
2. je wana local office hapa Tanzania au mtu anayewawakilisha hapa bongo? kama ndio naomba contact zao. au mtu yeyote mwenye uzoefu na kampuni hii naomba wadau mtusaidie kutupa taarifa kuhusu kampuni hii.
3. nasikia kuna form za ukaguzi inabidi uzione/wakutumie. zinaitwaje? je unarequest au wanatuma automatically? na hii ni baada ya kulipia gharama za CIF au kabla? na ikiwa gari uliyochagua haijafanikiwa kupita hizo test za ukaguzi nawe umeshalipia gharama za manunuzi, nini kinafatia?
4. kuna kampuni maalum au mtu ambaye unaweza muomba akafanye ukaguzi wa gari kabla hujailipia? ili kujiridhisha na taarifa unazopewa na dealer

swali no. 3 na 4 hayako specific kwa realmotor pekee, hivyo wenye uzoefu na uagizaji magari kupitia makampuni mengine naomba mmwage mauzoefu yenu hapa
asanteni
 
Mimi pia natamani kujua, ngoja nikae hapa nisubiri kuelimika.
 
kama hujawahi ku nunua kwenye mtandao ningekushauri uachane na hii mambo au uende kwabkampuni zenye wawakilishi hapa nchini vinginevyo haya maswali sidhani kama yote yatapata majibu kwa usahihi....kumbuka kuna makampuni ya wanaijeria kibao ukiwapigia simu utagundua kwani wanalazimisha lafudhi binasfi sikushauri uendelee na manunuzi haya ya kielektronik ambayo inaonesha huna ujuzi achilia mbali uzoefu utalia bure na hako kamkopo.....du watu wengine bana yaani kuagiza gari unaanzisha uzi.....sasa ukinunua private jet si utafanya press kabisa
 

Asante kwa ushauri
Ila nikukumbushe tu kuwa si.kila anayenunua gari basi ni la mkopo.
Halafu hata ukiamua kununua hapa kuna siku unaweza.hitaji kuagiza nje bado utahitaji ushauri na maarifa kutoka kwa wazoefu..
 
1. Nimewahi agiza toka realmotors.....ila nilitumia (paytrade..ile ya tradecarview hope nimepatia jina, hivyo sikuwatumia wao direct). Nilifanya hivyo ili kuepuka kubadilishiwa gari na kulizwa.
Ila hao jamaa waduanzi ike mbaya nililipia dec gari nikaitoa march mwanzoni...madai walikuwa holiday

No 2..... sijui

3. Ninachojua unalipia cif with inspection then wanakutumia docs... na waambie gari ifanyiwe ukaguzi hivyo kuna gharama za ziada kama sikosei( si ndio cif with inspection????) Watakutumia certificate

4...sijui....angalia usipigwe
 
Walikuwa hawajui hiyo Vanguard unavyoisubiri...
wangejua wangeharakisha .ha haa
 
Kwa kukutoa hofu mi mwaka jana september nimepokea gari kutoka real motor jp,,wako njema...agiza gari kupitia website yao kwani ukipitia tradecar view kuna gharama zinaongezeka bila sababu ya msingi,,trust me wako njema na gari zao ni kiwango
 
Kwa kukutoa hofu mi mwaka jana september nimepokea gari kutoka real motor jp,,wako njema...agiza gari kupitia website yao kwani ukipitia tradecar view kuna gharama zinaongezeka bila sababu ya msingi,,trust me wako njema na gari zao ni kiwango
Asante kwa mchango wa kutia moyo
Naona wao modality ya payment ni kupitia telegraphic transfer nikawa na wasi wasije ingia mitini coz mawasiliano ni kupitia web yao tu. Halafu wanaonekana wako for quick sales ; 100% upfront
Its true gari zao zinaonekana ni quality with low mileage ;reasonable prices
Ingawa swala la delivery nimeona ktk reviews watu wanalalamika
 
Quality wanajitahidi
Customer care 05%
Milage...usidanganyike wanacheza nazo tu......

Cha msingi ununue gari nzuri.
Ila usisahau kuzichunguza vyema gari zao...kuna nyingine zina vijiscratch mpaka uichunguze haswa picha

All the best
 

Mkuu kwa utaalamu wako ni mwendo wa speed ngapi wa kuendesha gari kwa economy ya mafuta ukiwa safari? na ni kwa nini gari ikikimbia sana ulaji wa mafuta unaongezeka?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…