Korea ya Kaskazini yatishia kuishambulia Marekani

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Korea Kaskazini imetishia kutekeleza mashambulio ya nyuklia dhidi ya Korea Kusini na Marekani iwapo nchi hizo mbili zitaendelea na mazoezi ya pamoja ya kijeshi.

Mazoezi hayo, ambayo hufanyika kila mwaka, mwaka huu yatashirikisha wanajeshi 300,000.

Serikali ya Korea Kaskazini imetoa taarifa ya ikitishia kutekeleza “shambulio la nyuklia kwa ajili ya haki”.

Ni kawaida kwa Pyongyang kutoa vitisho vya aina hiyo na wataalamu wanatilia shaka uwezo wa Korea Kaskazini kuwa na makombora ya nyuklia.

Hisia hupanda kati ya Korea Kaskazini na Korea Kusini na Marekani kila mazoezi hayo ya pamoja ya kijeshi yanapofanyika.

Pyongyang hutazama mazoezi hayo kama mazoezi ya kujiandaa kuivamia.

Mwaka uliopita, Korea Kaskazini ilitishia kugeuza Washington kuwa “bahari ya moto”.

Wizara ya ulinzi ya Korea Kusini imeionya Pyongyang dhidi ya “hatua za haraka zisizo za busara ambazo zinaweza zikailetea maangamizi”.

Mazoezi ya mwaka huu, yanayoshirikisha wanajeshi 300,000 wa Korea Kusini na 15,000 wa Marekani, ndiyo makubwa zaidi kuwahi kufanyika.

Yanaandaliwa siku chache tu baada ya Umoja wa Mataifa kuidhinisha vikwazo vipya dhidi ya Korea Kaskazini kutokana na hatua yake ya kufanyia majaribio bomu la nyuklia na kufyatua makombora.

Korea Kaskazini ilijibu vikwazo hivyo kwa kutangaza itaweka tayari silaha zake za nyuklia na pia ikavyatua makombora ya masafa mafupi baharini.
 
watunguane tu ili tupate suluhisho la silaha za nchi gani duniani ni bora,maana ni mda sasa toka vita ya pili ya dunia mtaifa yajapigana kabisa
 
Ulimi ni kichaka cha moto. Korea kaskazini ichunge ulimi wake isije kuwa kama Iraq. Sadam ulimi ulimponza.
 
Huyu rais kijana nadhani hana washauri wazuri. Binafsi sioni nguvu ya yeye kupigana na nchi zote hizo na sijaona hata supper power nation moja ikimuunga mkono. Anataka tu kuhitimisha utawala wa kifalme kwa nchi hiyo kutoka katika familia yao.
 
Kila siku kanatishia tu si kaanze tuone kama kanaweza sasa,maneno meengi halafu vitendo zero,kwa kumbukumbu zangu hicho cjui ni kitisho cha 100 lakini hata guruneti tu kashindwa kurusha huyo kiduku nafikiri anajua mziki wa USA wenyewe hawanaga vitisho vya kifala wakisema tunakupiga wanapiga kweli,kaka muulize saddam a.k.a wa libya
 
Mimi naisubiria kwa hamu vita ya tatu ya dunia.
 
Ningekuwa dio mimi mmarekani nigemlia timing kuliko nimsubili anianze yeye. Yani wangekuta asuhi na mapema nimeisha mukota yule dogo.
 
huyu jamaa ana mikwara sana lakini vitendo sifuri.
ila USA & KOREA wawe makini huyu dogo anaweza kushawishiwa na mizimu ya babu zake akafanya shambulizi la ghafla.
 
Ningekuwa dio mimi mmarekani nigemlia timing kuliko nimsubili anianze yeye. Yani wangekuta asuhi na mapema nimeisha mukota yule dogo.
We jamaa muvi za kina rambo na anoldi zilizotafsiriwa na lufufu zimekushika sana! Unafikiri vita tena vya nyuklia ni ngumi za van dame na tompoo eeeh!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…