Ndugu zangu hasa wale wachambuzi wa maswala ya kivita naombeni msaada wa maelezo nini kinaendelea katika sakata hili. Sababu inayowagombanisha ni nini, mchokozi nani. Je hiyo vita ni ya Marekani na Korea Kaskazini au pia nchi nyingine zinahusika na kama kuna nchi nyingine zinahusika Je Marekani anaungwa mkono na nani na Korea washirika wake ni wapi. Je katika vita hivyo nani anaweza kuibuka kidedea. Je nchi zipi zinaweza kuathirika kichumi na kimiundombinu. Mwisho kwa sisi hapa Tanzania tunaweza athirika kiuchumi.