JamiiForums
JF Official Account
- Nov 9, 2006
- 6,227
- 5,269
Ndugu wanaJF,
Zile tuzo kubwa kuliko zote Barani Afrika zimewadia. Msimu wa Mavuno kwa wasanii wa muziki kutoka pande mbali mbali za Afrika umebisha hodi. Ni KORA-All Africa Music Awards 2016. Watanzania tusifanye makosa.
Kampuni ya Jamii Media kupitia [B]JamiiForums[/B], kipekee kabisa itakuwa inakujuza kila kinachojiri katika msimu huu wa Tuzo za KORA-All Music Awards 2016 ili kuhakikisha inatoa mchango/sapoti ya kutosha na kufanikisha ushindi kwa wasanii wetu wa muziki kutoka Tanzania.
Taarifa iko hivi;
Fainali za Ugawaji wa Tuzo za KORA zitafanyika tarehe 20, Machi mwaka huu (2016) katika mji wa Windhoek nchini Namibia. Awali ilikuwa zifanyike Desemba 13, mwaka 2015, lakini kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka kwa waandaji, wamelazimika kuziahirisha ili kuzipa nafasi zaidi maana mchuano unatarajiwa kuwa mkali sana msimu huu.
Mbali na tuzo yenyewe, zawadi kubwa ya mwaka huu kwenye kipengele cha ‘Best Artist of the Continent’ itakuwa ni 1,000,000$ USD, sawa na zaidi ya shilingi bilioni 2 za kitanzania.
Sasa basi, Tanzania tumebahatika kupata wawakilishi watano waliopata nomination (teuzi) katika vipengele mbalimbali.
Diamond Platnumz ametajwa kuwania kipengele cha Best Male - East Africa, huku Vanessa Mdee akiwania Best Female - East Africa. Wakazi anawania kipengele cha Best Hip Hop, na Yamoto Band wametajwa kuwania kipengele cha Most Promising Male Artist Of Africa, bila kumsahau Mrisho Mpoto anayewania Best Traditional Male Artist Of Africa. Hapo tunakosa ipi sasa?!
Mchakato wa Upigaji Kura na namba za washiriki utatangazwa muda wowote kutoka sasa.
===========
UPDATE:
Jinsi ya kuwapigia Kura wasanii wetu kutoka Tanzania:
Wakazi: KORA 123
Yamoto Band: KORA 106
Vanessa Mdee: KORA 22
Mrisho Mpoto: KORA 67
Diamond Platnumz: KORA 18
*Tuma Code ya msanii husika kwenda Namba +248 984 000
Tanzania kwanza!