- Source #1
- View Source #1
Nimekutana na taarifa mtandao wa X juu ya kuahirishwa kwa kongamano la kitaifa juu matukio ya kupotea kwa raia lilioandaliwa na TLS ambalo lilipangwa kufanyika katika ukumbi wa Ubungo plaza, je taarifa hiyo ina ukweli wowote?
- Tunachokijua
- Chama cha Mawakili Tanganyika (Tanganyika Law Society, TLS) ni chama cha kitaaluma kinachoundwa na mawakili wa Tanganyika (Tanzania Bara). Kina jukumu la kusimamia masuala yanayohusu mawakili na sheria kwa ujumla nchini Tanzania. Hii ni pamoja na kuhakikisha maadili ya taaluma, kuhimiza mafunzo endelevu kwa mawakili, kulinda maslahi ya umma, na kutoa huduma za kisheria.
TLS kupitia kwa Rais wake, Boniface Mwabukusi imeitisha kongamano la kitaifa lililopangwa kufanyika tarehe 05/10/2024 katika ukumbi wa Ubungo Plaza, jijini Dar es Salaam ambapo wananchi watakutana na kujadili changamoto na kushauri juu ya suluhisho kuhusu Matukio ya Kupotea kwa Raia nchini Tanzania.
Mara baada ya kutolewa kwa taaarifa ya kufanyika kongamano hilo, kumeonekana posta ikionesha kuwa kongamano hilo lililokuwa lifanyike tarehe 5/10/2024 Ubungo Plaza kuwa imeahirishwa.
Je, ukweli ni upi?
JamiiCheck imetafuta ukweli kwa kutazama kwenye kurasa rasmi za Chama cha Mawakili(TLS) na Kwenye kurasa rasmi za Rais wa TLS, Boniface Mwabukusi na kubaini kuwa hakuna Taarifa ya kuahirishwa kwa kongamano hilo bali kote wameweka chapisho la kuonesha uwepo wa kongamano lenye ujumbe wa kuwaalika Wananchi kuhudhuria kongamano hilo.
Aidha, JamiiCheck imebaini kuwa kuna tofauti ya dakika 2 kati ya chapisho la Tangazo la TLS kuhusu kuwepo kongamano na hilo la kuzushwa kuahirishwa kongamano ambapo TLS waliweka chapisho lao kwenye mtandao wa X mnamo Tarehe 1/Oktoba 2024, muda wa 2:47 PM( Saa 8 na dakika 47 mchana) kama inavyoonekana kwenye picha hapo chini, na baada ya dakika 2, yaani Saa4:49 PM Oktoba 1 2024( Saa 8 na dakika 49 mchana) aliyechapisha taarifa ya kuahirishwa naye akaweka chapisho lake, hali inayothibisha kuwa amechapisha taarifa isiyo ya kweli.
Chapisho la TLS kuhusu uwepo wa Kongamano
Chapisho la Uzushi kuhusu kuahirishwa kwa kongamano TLS