Komredi Kawaida: Huwezi Kutenganisha Maendeleo ya Tanzania na CCM

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,695
1,242
Kuna jambo ambalo yamkini watanzania wengi hawaelewi au wanapaswa kueleweshwa zaidi kuhusu maendeleo ya Tanzania na CCM, ikumbukwe tunapozungumzia maendeleo ya Tanzania siku zote hatuwezi iacha CCM kamwe kwa maana Chama Cha Mapinduzu (CCM) kama Chama tawala ndicho kinachopanga nini kitafanyika au kufanywa ndani ya Uongozi wake kwa kipindi kilichopewa dhamana ya kuongoza na Wananchi, hivyo juu ya nini kitafanywa au kitafanyika hii tunaita ni Ilani ya Uchaguzi ya CCM, ambapo kwa sasa tuna Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya miaka mitano yaani 2020-2025. Hivyo ukiisoma Ilani ya CCM vyema itaweza kukuonyesha kila kilichofanyika hapa Nchini kipo na kiliandikwa kwenye Ilani ya Uchaguzi wa CCM hivyo hakuna hata mmoja alikurupuka au kujiamulia kufanya kitu ambacho hakipo kwenye Ilani ya Chama hiki.

Hivyo maendeleo haya yote na mambo yaliyofanywa na yanayoendelea kufanywa ni kutokana na usimamizi mzuri wa utekelezaji wa Ilani ya CCM kama Vile Huduma za Jamii (Shule, Hospital, maji, Umeme nk), Miundombinu (Ujenzi wa miradi mbalimbali, Barabara, Uboreshwaji,), Demokrasia, na mengine mengi, haya yote ni kutokana na usimamizi mzuri wa utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Tunavyotaja maendeleo ya Tanzania basi tujue tumeitaja CCM kwa kusimamia Vizuri Ilani yake ya Uchaguzi, watanzania Chama Cha Mapinduzi kiliahidi mengi na kimetekeleza na kinaendelea kutekeleza, hivyo tusiwe na mashaka bali tukiunge mkono ili kiendelee kufanya vizuri zaidi na zaidi kukidhi mahitaji ya Watanzania.


#KaziIendelee.
#KulindaNaKujengaUjamaa.

Imetolewa na;
Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM-Taifa.
 
Kuna watu hua wanatia hasira sana hadi naona bora ninyamaze tu....☹️
 
Na huu umasikini, ujinga, maradhi na uhujumu uchumi uliokithiri nao pia hauwezi kutenganishwa na majambazi ya ccm.
 
Back
Top Bottom