Kodi zetu ndio Maendeleo ya Taifa letu

Feb 25, 2012
419
2,169
Kodi zetu ndio Maendeleo ya Taifa letu.

Mwaka 2021/22- Trillions 22.2.
Mwaka 2022/23- Trillions 24.1.
Mwaka 2023/24- Trillions 27.6

IMG_4177.jpeg

====
Pia soma:
 
Kodi zetu ndio Maendeleo ya Taifa letu.

Mwaka 2021/22- Trillions 22.2.
Mwaka 2022/23- Trillions 24.1.
Mwaka 2023/24- Trillions 27.6
Kuna wakati mlituambia kuwa tuko UCHUMI WA KATI ila naona kwenye takwimu ulizoambatanisha hapo inaonekana kuwa UCHUMI WETU UMEPANDA KWA SASA UKILINGANISHA NA NYAKATI ZILE ZA UCHUMI WA KATI. Sasa swali langu ni Je,kama taifa letu limekua KIUCHUMI tumehama kutoka UCHUMI WAKATI,NA SASA tuko kwenye UCHUMI WA DARAJA GANI?
 
1. Mwigulu lipa mkopo wa HESLB wadogo zetu wasome
2. Mnakopa sana, mnakusanya sana kodi ila hatuoni maendeleo, watoto wanakaa chini, vyoo shuleni changamoto, huku mkinunua ma V8 na kujenga mahoteli nchi jirani.
3. Hivi kuna haja gani ya kununua V8 mpya kila mwaka kwaajili ya wakuu wa mikoa, mawaziri na wabunge katika nchi masikini kama hii ambapo kodi zinazo kusanywa zinaishia mifukoni mwenu viongozi wa umma?
 
Kodi zetu ndio Maendeleo ya Taifa letu.

Mwaka 2021/22- Trillions 22.2.
Mwaka 2022/23- Trillions 24.1.
Mwaka 2023/24- Trillions 27.6
Karibu tena Mkuu, baada ya kuadimika humu Kwa kipindi kiasi..

Umekuwa Serikalini ukihudumu nafasi mbalimbali kwenye Baraza la Mawaziri

Swali langu; Kipi kimefanya kiwango cha Kodi tunachokusanya kipande awamu hii kulinganisha na awamu iliyopita?

Swali la pili, pamoja na makusanyo ya kikodi kuwa makubwa kwanini bado tunaendelea kukopa?
 
Wana uchumi hili bango nalo hamkutaka kuliacha kulipigia hesabu kama sehemu ya mapato

Screenshot_20240705-000215.png


Nimeshuhudia maafisa wa jiji pamoja na afisa biashara wakimtoza mtu shilingi 80,000 kwa ajili ya kodi ya bango kama hilo hapo pichani.

Wakati biashara hiyo ina leseni yenye thamani ya shilingi 40,000.

Bado mtu huyu pia anakuja kutozwa shilingi 60,000 ya service levy.

Swali langu ni kwamba inakuwaje kodi ya bango na service levy ziwe zinatozwa kwa kiasi kikubwa kuliko gharama ya leseni??
 
Thamani ya shilling imeporomoka kwa kasi sana . Una mpango wa kumshauri nini rais ili thamani ya fedha yetu isiporomoke zaidi ? Au akili yako imeishia kwenye tozo , kuwakamua watanzania tu na hauna ubunifu wa kuinusuru thamani ya fedha yetu .
 
Jielekezeni sasa kuhakikisha mnajengea uwezo kundi kubwa la vijana linaingia katika nguvu kazi ya taifa na kulipa kodi. Kuna programu moja sidhani kama tukiwashauri mtaikubali watu wa serikali kuokoa kizazi hiki hasa wewe waziri wa fedha. Utakumbukwa sana vijana wa taifa hili.
 
Back
Top Bottom