Kodi za TRA

virginity

JF-Expert Member
Jul 1, 2017
895
965
Habari Wana jf.
Naomba kueleweshwa kuhusu makadirio ya Kodi. Nimeanza biashara ya vipuri vya pkpk takribani mwaka mmoja sasa.

Mara ya kwanza kwenda t.r.a nilikadiliwa 89000 na mwaka huu nimerudi tena naambiwa makadirio 250k naomba kueleweshwa kuhusu makadirio haya wanazingatia nini Hadi kukadiria?, Wanaongeza ongezeko kwa % au wanakadilia tu??

Wafanyabiashara wenzangu wa spear hali ikoje huko jamani mbona Kodi nyingi sana

Note: sikuyauliza hayo sababu sikwenda Mimi.

Biashara moja ina;
Kodi pango
Kodi serikalini
TRA
Service levy
Fire
Uchafu
Umeme
Ni Mungu tu atusaidie
 
Nachofahamu mimi Ukadiriwaji wa kodi unakwenda sambaba na Mapato yako unayotarajiwa kwa mwaka husika kwa wale wapya au mwendendo wa biashara yako iliyopita kwa wale waliokwisha kuwa kwenye biashara.Hivo ndugu yangu siyo lazima ukiwa umelipa 89,000 basi kila mwaka ndiyo utakuwa unalipa hivo inaweza pungua au ongezeka kulingana na biashara inavyoenda. Labda nikushauri kueka kumbukumbu zako maana ndizo zitakusaidia kuuliza kama wamekupandishia kwa kigezo kipi. Cha msingi kumbukumbu zako.
 
Kama una mashine ya efd wala hautaongea bali rekodi zako za risiti ndizo zitaongea.

Kodi ni asilimia ya faida ya mapato yako mnagawana na serikali. Wanachofanya tra ni ubabe wa kimamlaka wa kukukadiria sawa sawa na waliokutangulia katika hiyo biashara ili kuweza kupata wanachotaka bila hata kutazama hali yako ya uchumi.

Kama hauna Mashine yao ya risiti unaweza tumia hata simu hizi za mkononi wamerahisisha sana siku hizi unapewa access una download application na unakuwa na kamashine kadogo kamfukoni.

Unawapa watu risiti vizuri tu. Hii itakusaidia kuwa na ushahidi usio katalika kisheria maana ni system yao. Utakwepa usumbufu mwingi sana.

Mteja amekuja kununua kifaa mpatie risiti, umetengeneza pikipiki mpatie risiti. Hapo utaona kama mtagombana kwenye kodi.
 
mzee unamuingiza mwenzako mkenge. sidhani kama kila mtu anatakiwa kuwa na mashine ya efd sababu sheria ukisoma walizotuonyesha wao wenyewe tra ni kuwa mtu akiuza kwa mwaka zaidi ya milioni 11 ndiyo anatakiwa kuwa na hako kamashine. halafu kukadiriwa na wafanyabiashara wenye mauzo chini ya milioni 100 kwa mwaka ndiyo wanatakiwa kwenda kukadiriwa ila kampuni na wale ambao wanazidi milioni 100 wao wanajikadiria na kupeleka mahesabu. Kama unadhani ni hivi ulivyomshauri jamaa analalamika sana sababu mimi sijafikia tumia efd nakadiriwa kwa kuwa na kitabu changu cha mauzo nilitengeneza risiti za mkono na huwa nakomaa nao kwa ushahidi wangu huo.
 
Tsh 250k kwa mwaka ni ndogo sana. Vitu vingine uwe unakaa tu kimya. Au unataka TRA wakutembelee na kukuchimba kwa kina? Hiyo bei ni very fair sema unataka tu kukwepa kulipa hata hicho kidogo. TRA wakisema wafanye uchunguzi wa kina kwa kila mtu na kuhakikisha sheria inafuatwa wengi tutafunga maduka.
 
Vitu vyengine mnafata mumbo Sana 250K ni hela ndogo sana kwa biashara yako ni wala sio kitu cha kulia lia hapo kimahesabu kwa Siku unalipa Tsh 692 tena kutoka kwa net profit sasa unataka kusema kwa biashara yako kwa siku hepatitis 692 ya TRA? Mchawi sio TRA mchaw ni ww mwenyewe, Tanzania wigo wako kibiashara, ungoneza mauzo, ongeza mzigo, kuwa creative katika biashara yako sio kulia lia. Na kimsingi kama kweli unajua biashara hizo kodi wala hulipi ww mlaji ndio atalipa, hakuna tajiri analipa kodi kwa pesa yake mwenyewe. NARUDIA KWA CAPITAL LETA HAKUNA TAJIRI ANAELIPA KODI KWA HELA YAKE MWENYE SISI MASIKINI (WATEJA) NDIO TUNAMLILPIA TAJIRI KODI. jielimishe
 
Back
Top Bottom