Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 1,515
- 4,016
Kocha Mkuu wa Simba SC, Fadlu Davids, amewataka mashabiki na vyombo vya habari kuacha kumwekea presha mchezaji wake Jean Charles Ahoua, akisisitiza kuwa kijana huyo bado ana safari ndefu ya kujifunza.
"Niliwahi kuwaambia kuwa Jean Charles Ahoua ni Mchezaji mdogo sana kiumri, alivyokuwa anafunga na kupika mabao ni vyombo vya habari ndivyo vilimkuza sana kitu ambacho sio kweli hayupo level hiyo, tumpe nafasi ya kukosea na kujifunza, tumtolee presha kwakuwa bado mdogo sana" - alisema Fadlu.
"Jean Charles Ahoua alikuwa na mechi nzuri sana ugenini dhidi ya Constantine haswa kwenye eneo la ulinzi ila changamoto ilikuwa kwenye kushambulia alikuwa anapoteza mipira kirahisi sana na tumekaa nae kumpa darasa nini anapaswa kuboresha ila ni kutokana na majukumu mapya tuliyompa"