Mtemi Mbojo
JF-Expert Member
- Apr 27, 2017
- 714
- 1,332
Nikiwa kama mdau na mshabiki wa soka la Tanzania, nami nimewiwa kuchangia hili kwa maendeleo endelevu ya soka la klabu ya Yanga na Taifa kwa ujumla
Nashauri klabu ya Yanga ilete kocha kijana mzawa awe kwenye jopo/benchi la ufundi la kocha wa timu ya Yanga( Dar Young African FC). Hii ni kutokana na MAFANIKIO lukuki aliyoyaleta kocha huyu toka nchini Argentina.
Naamini ujuzi, mbinu ,uzoefu na mikakati ya kocha huyu GWIJI ,si vyema kuacha ipotee pindi atakapo amua kuondoka.
Hivyo nashauri klabu ya Yanga kuleta kocha/makocha vijana kwa ajili ya kujifunza UCHAWI wa kocha huyu mkongwe ili hata siku akiondoka tubaki na ujuzi wake. Mbinu hii nimeona klabu ya Simba wakiitumia kwa kuhakikisha kocha wao msaidizi ,ndugu Matola Selemaini kubaki kwenye benchi la ufundi la klabu hiiyo licha ya mabadiliko ya mara kwa mara ya makocha,naamini after time t ,Kocha Matola atakuja kuwa sio HAZINA tu kwa Simba bali hata kwa Taifa..Yanga igeni hili haraka
Mwisho, nawashauri TFF na hata Wizara ya Michezo kuona namna bora zaidi ya kuchota UJUZI wa gwiji hili la soka toka nchini Argentina. Tuitumie fursa hii ya yeye kuwepo nchini
Naomba kuwasilisha
Asanteni