Kocha Amunike atangaza majina ya Wachezaji watakaoenda kupambana na Uganda, Septemba 8

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,508
3,756
Kocha mpya kwa timu ya Taifa 'Taifa Stars', Emmanuel Amunike ametangaza kikosi cha Wachezaji 25 kwa ajili ya mchezo wa kufuzu michuano ya AFCON dhidi ya Uganda

Majina ya Wachezaji hao yaliyotangazwa leo Agosti 21 ni Aishi Manula, Mohammed Abdilrahman, Beno Kakolanya, Shomari Kapombe, Hassan Kessy na Gadiel Michael

Aidha, wengine ni Abdi Banda, Kelvin Yondani, Aggrey Moris, Andrew Vicent, Himid Mao, Mudathir Yahya, Jonas Mkude, Erasto Nyoni, Saimon Msuva na Shiza Kichuya

Wachezaji wanaokamilisha orodha hiyo ni Rashid Mandawa, Farid Mussa, Hassan Dilunga, Feisal Salum, Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu, John Bocco, Shabani Chilunda na Yahya Zaydi

Taifa Stars inatarajiwa kucheza na Uganda mnamo Septemba 8, 2018
 
Kila la kheri Taifa Stars. Chondechonde msitutie aibu kama vyura wa Jangwani
 
Taifa Stars...
IMG-20180821-WA0073.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo Farid Musa toka aende huko Spain sidhani kuna ambaye amewahi hata kuona highlights zake,mwenzie Chilunda kaenda majuzi tu lakini jana kacheza timu ya wakubwa.

Cha ajabu kwenye kikosi cha taifa kutwa yumo.
 
Nitasema kweli daima fitna kwangu mwiko .

Taarifa za vyombo vya habari zinaeleza kwamba Kocha mpya wa Taifa Stars ameteua wachezaji watakaovaana na Uganda Cranes kwa michuano ya AFCON , sasa mimi ninataka kujua kama kweli aliyeteua kikosi hiki ni Amunike amewajuaje wachezaji wazuri bila hata kuwaona uwanjani ? nauliza hili ili matokeo mabaya yakitokea tujue wa kumpa lawama.

Msimchagulie timu halafu mkasema kachagua yeye , mwisho wa siku akatwishwa lawama kwa mtindo wa kuangushiwa jumba bovu , maana hata kwa akili ya vikatuni si rahisi kwa muda mfupi namna hii Amunike aweze kuwajua wachezaji , vinginevyo tutajieni mtu halisi aliyeteua timu hii .
 
Back
Top Bottom