Kiwango cha soka Afcon vipi?

four eyes

JF-Expert Member
Jan 11, 2017
905
1,406
Habari wadau?Kwa siku kadhaa sasa nimekuwa nikifatilia Kwa ukaribu mechi za mashindano ya soka ya kombe la afrika maarufu Kwa jina la Afcon yanayoendelea huko Gabon,nilichokigundua mpaka sasa na ambacho kimenisononesha ni kiwango cha chini kinachoonyeshwa na timu zinazoshiriki lakini pia kiwango cha chini cha mchezaji mmoja mmoja(individually),mechi nyingi hazina mvuto ukilinganisha na mashindano yaliyopita ya Afcon ambapo timu kama bafanabafana,Ghana,Nigeria,Senegal,Cameroon,Egypt na nyinginezo ziliweza kutengeneza umaarufu Kwa soka tamu la kusisimua na wachezaj mmojammoja pia waliweza kupata umaarufu mkubwa na hatimaye kupata timu nje Kwa kuwa na soka zuri.karibun wadau tujadiri tatizo laweza kuwa nini ktk hili au nyie mnaonaje soka linalochezwa ktk kombe hilo linaloendelea huko Gabon.
 
Kusema ukweli mpaka sasa AFCON inaendelea vema na ni ya ushindani haswa. Kitu tunachokiona ni namna gani kwenye soka la sasa "ubaba" haupo tena, au twasema upo mashakani.

Tumeona namna gani Ivory Coast, Algeria, Egypt wanavyohenyeshwa. Mpaka sasa hakuna timu ya waarabu iliyoondoka na ushindi: wanaambulia draw tu. Mwenyeji mwenyewe Gabon anatapatapa, mechi ya pili sasa draw!
 
Zimbabwe na Uganda wameshangaza watu. Algeria anahangaika kusawazisha! Ghana anapelekeshwa na Uganda mpaka anaokolewa na penalty! Ivory coast anahaha mzee!

Ila naona kabisa ule u-legend wa baadhi ya timu za Afrika au tunasema "fear factor" inapotea. Cameroon hii sio ya kipindi kile bwana, kipindi wamavaa body tight. Ghana the same na pia Egypt. We missed those moment.

Timu ambazo hazikudhaniwa, kama vile Guinea Bissau, Burkina Fasso, Mali etc wanacheza mpira mzuri sana
 
team za afrika kiwango kinafanana ndo maana ma draw kibao michuano haina hta msisimko kma kipindi kile cha Europa
 
Naifuatilia sana,kwa kweli enzi za kucheza kwa majina zimekwisha.Ule tunaita "ufather" haupo tena.Wapo vijana wapya na wenye sura mpya.

Miaka ile ulikuwa ukienda kuitazama Cameroon basi unajua humkosi Olembe,Song,Idrissa,Etoo,Mboma,Ndiefi na wenzao.

Leo Uganda anamjambisha Ghana mpaka anapata goli la maguu 12.Guinea Bissau kapiga mpira mmoja mkubwa sana akiwa na watoto wadogowadogo.

Zimbabwe sio ike ya kina Benjan,DRC si ile ya kina Lomana Lualua...Nchi nyingi za Afrika zimeona "fursa" katika mpira na zinaanza kuwekeza kwa vijana.Tumebaki sisi tu na Siasa zetu za TFF

Kuna mtoto anaitwa Diawara na jamaa jingine linaitwa Nakouma,hatari sana.Tumewekwa kundi moja na Uganda,Lesotho na Cape Verde kuelekea AFCON 2019.Nimesmsikia NAPE anasema timu zote zinafungika...Sijui yeye atacheza namba ngapi ili kupachika hayo magoli yote
 
Afcon kutoonyeshwa na TV station kama ITV & TBC1 zimefanya watanzania wengi kutoifatilia,kwani hizo station ndizo huonekana sehemu nyingi ya nchi!,
 
Zimbabwe na Uganda zinatashangaza kwasababu viwango vyao vimepanda au Kwa sababu viwango vya sasa vya waliokuwa wababe vimeshuka?
 
Si
Afcon kutoonyeshwa na TV station kama ITV & TBC1 zimefanya watanzania wengi kutoifatilia,kwani hizo station ndizo huonekana sehemu nyingi ya nchi!,
si zinaonyeshwa na azam? Hzo station unazozitaja bado una matumaini nazo ktk vitu kama hv? Hzo zipozipo tu kaka usitegemee jipya kutoka kwao
 
Jam
Jambo la kujiuliza ni je ufather unaosema umekwisha umekwisha sababu timu ndogo zimeboresha viwango au sababu hao mafather viwango vyao vimekuwa vibov?Zimbabwe kwel wameonyesha kiwango kizuri na ile ndio ilikuwa mechi nzur yenye ushindan walipocheza na Algeria,wengine hawaelewek,wachezaj hawana hata ubunifu na utukutu wa kina diof enz zile,au kina ndiefi na wengineo
 
Bingwa atakuwa timu bora ktk timu wabovu. Hata baadhi ya viwanja hassa sehemu ya kuchezea ni vibovu. Hadi sasa viwango bado labda huko mbele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…