A
Anonymous
Guest
Nianze kwa kusema kuwa inawezekana matumizi sahihi ya tiketi zinazotumika katika Kivuko cha Busisi - Kigongo Ferry Mkoani Mwanza hayapo sawa au kuna watu wachache wanatengeneza mazingira ya kukosekana kwa usawa.
Kwanza kabisa Hakuna utaratibu wa ku scan tiketi kama ilivyokuwa zamani, wakati wa utawala wa John Magufuli, haya mambo hayakuwepo.
Marehemu alisisitiza njia hiyo itumike kwa kuwa alitaka maslahi au mapato yaende Serikalini tofauti na ilivyo sasa ambapo inaonekana kuna kikundi cha watu wachache wanacheza michezo fulani kimyakimya yakupiga hela.
Nimekuwa nikipita hapo katika hilo daraja kwa muda mrefu scanner zilikuwepo lakini ndani ya kipindi cha miezi mitatu iliyopita utaratibu huo umekufa na kuna mazingira ya upigaji.
Ukikata tiketi kwa ajili ya kuvuka unapewa kisha ukikabidhi kwa wahusika kwa maana ya wakaguzi, hawazichani, wanaziweka kwenye pipa dogo la taka ambapo baadaye inawezekana wanaweza kuzifanyia namna.
Uchunguzi nilioufanya kwa muda wa miezi mitatu nikiwa napita katika kivuko hicho nimeona mara nyingi hali inakuwa hivyo, hakuna utaratibu wa kuchana tiketi wala ku scan.
Kilichoniacha hoi zaidi ni kuwa kuna siku nimewakuta maafisa wapale wakikusanya tiketi zilizokuwa zinawekwa kwenye pipa hilo, sikujua lengo lao ni nini au wanaenda kuzifanyia kazi gani kama hawazichani basi hapo ndio unatimia ule msemo wa “Akili ya kuambiwa…….”
Naomba Jamii Forums msaidie kupaza sauti juu ya kinachoendelea kwenyee mradi huo wa Kigongo Busisi kuna mazingira ya ‘upigaji’ wa wazi kabisa.