Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,297
- 25,912
Ingawa mimi si mwana-CCM au mwanachama wa chama chochote cha siasa ndani na nje ya Tanzania, tangu utoto wangu nimekuwa nikifutilia siasa. Nikiwa na zaidi ya miaka 40 hapa duniani, nimekuwa mfuatiliaji mkubwa wa siasa na pia kushiriki kwenye chaguzi, kuanzia ule wa mwaka 1995.
Wengi sasa tunajua kuwa Ndugu Abdulrahman Kinana amewasilisha ombi la kujiuzulu nafasi ya Makamu wa Mwenyekiti wa CCM Taifa na imeripotiwa kuwa Rais Samia ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa ameridhia ombi hilo la kujiuzulu kwa Kinana.
Ni wazi kuwa mchakato wa kumpata mrithi wa Kinana umeshaanza. Wapo wanachama wengi waandamizi ndani ya CCM ambao wanatajwa kumrithi Kinana. Kwangu mimi, kulingana na 'utamaduni' wa CCM ambao nimeushuhudia, Dkt. Bashiru Ally Kakurwa ana nafasi kubwa kushika nafasi hiyo.
Pamoja na kuwa Dkt. Bashiru ni mzoefu kisiasa na kiuchaguzi, anayo sifa kuu ya nafasi hiyo ndani ya CCM: kuwahi kuwa Katibu Mkuu wa CCM. Kuanzia kwa Mzee Msekwa, Mangula na Kinana, wote waliwahi kuwa Makatibu Wakuu wa CCM na baadaye kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM-Taifa. Sina maana kuwa Dkt. Bashiru ndiye Katibu Mkuu wa CCM pekee wa zamani aliyepo.
Mzee Mukama na Mzee Makamba wapo. Kwa umri wao, ni rahisi kujenga hoja kwamba wanahitaji kupumzika siasa za moja kwa moja majukwaani kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa mwakani. Lakini, Dkt. Bashiru bado ana nguvu za kutosha kukitumikia chama chake. Ana uzoefu wa siasa za majukwaani na za kiuchaguzi.
Kimsingi, namuona Dkt. Bashiru Ally Kakurwa kama a leading candidate kwenye kumrithi Ndugu Kinana. Kuwahi kushika nafasi ya juu ndani ya CCM-MFANO Katibu Mkuu ni added advantage. Ni mawazo yangu huru tu.