Wanabodi,
Naangalia huu mkutano wa Rais Magufuli na wafanyabiashara, kiukweli nimeguswa sana na uchapakazi wa rais Magufuli.
Namtafakari jinsi huyu jamaa anavyochapa kazi hadi sijui analala saa ngapi maana aliwahi kusema ana mafaili hadi room.
Angalizo: Kama wewe ni mmoja wa wale wenye allegy na pongezi zozote kwa rais Magufuli, ili kukuzuia usikereke, nakushauri, uishie hapa.
Kuna msemo wa Waswahili, usemao mzigo mzito mpe Msukuma. Kabila la Wasukuma ni wachapakazi kweli kweli. Jee kuna ukweli kuna baadhi ya makabila watu wake ni wachapakazi na makabila mengine watu wake ni wavivu wavivu?.
Inawezekana huu uchapakazi wa rais Magufuli ni kutokana na kabila lake la wachapakazi?.
Specialization za Makabila.
Tukubali tukatae, kuna makabila, they are the best kwenye maeneo fulani, yakiendelezwa in that direction, taifa litapata manufaa makubwa.
Mfano makabila ya wawindaji wa milimani, they make wanariadha wazuri, hivyo kina Bayi, Nyambui, Shahanga, Ikangaa, etc, ni watu wa huko.
Kuna kabila ndio wanaongoza kuuza nyama mabuchani. Kuna kabla ndio wanaoongoza kuchoma nyama mahotelini na mabaa. Kuna kabila ndio mabingwa wa kuchonga vinyago, kabila wadada wao waliongoza kufanya ile the oldest profession, hivyo tukitumia skills za makabila yetu in doing the best, tutapata maendeleo makubwa.
Uchapakazi huu, utaliletea taifa letu maendeleo makubwa, hivyo kama ametokea kiongozi toka kabila fulani, akaonyesha uchapakazi mkubwa, jee kuna ubaya katika kuchagua viongozi wakuu wa taifa letu, kuangalia uchapakazi wa mtu, ili kuhakikisha whoever anayekuwa rais wetu, awe na track record ya uchapakazi?.
Jee kuna ubaya tukiyajua haya makabila ya wachapakazi, ili kuyatumia kama kabila darasa kama ilivyo kwa shamba darasa, makabila mengine yaige mazuri ya makabila yetu, au huu utakuwa ni ukabila?.
Kwa trend hii ya rais Magufuli kuwaita Ikulu watu wa kada mbalimbali, namuona kabisa rais Magufuli akiwaita Wapinzani Ikulu nao watoe kero zao na kujadiliana nao mustakabali wa nchi yetu kisiasa, ambapo siku hiyo, pia rais Magufuli ataiondoa ile marufuku ya vyama vya Siasa kufanya mikutano ya hadhara.
Hongera sana rais Magufuli kwa uchapakazi, namalizia kwa kaswali kadogo tuu, kwa uchapakazi huu wa rais Magufuli, kweli kuna haja ya kufanya uchaguzi wa rais mwaka 2020, au Watanzania tupaze sauti zetu kwa kauli moja, Magufuli aendelee tuu na tufanye uchaguzi mwingine wa rais 2025?, na hiyo 2025 ikikaribia, kama katiba ndio kikwazo cha kuendelea, tuibadili katiba kuondoa ukomo?.
Na hiyo 2025, watu kama hawa ni watu wa kuwaangazia sana, ushauri wa Katibu Mkuu wa CCM Dr. Bashiru ufuatwe, tuwapike vijana wetu kama hawa, ili Tanzania tuendelee kupata viongozi wachapakazi kama huyu kijana
Wanabodi, Kabla Magufuli hajawa rais wetu, sisi wengine wenu tulijua tangu mwaka 2014 na tukasema humu!.Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli Miongoni mwa sifa zilizomuibua Magufuli ni sifa inayoitwa "uthubutu" boldness and sometimes unreasonably boldness...
P
Rejea
Je, kuna uhusiano kati ya IQ ya mtu na kabila lake, umasikini wake ...