Kituo Cha Uwekezaji, TIC, Tanzania, Zapongezwa Kwa Viwanda.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
52,689
119,326

Habari Zaidi ya Habari na PPR-SADC Investment Forum
Kituo cha Uwekezaji Tanzania, TIC, kimepongezwa kuongoza katika uwekezaji katika sekta, ya
viwanda, unaotumia tekinolojia za kisasa kabisa za uzalishaji viwandani, hivyo kuifanya Tanzania iwe ni nchi ya mfano barani Afrika kwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Pongezi hizo, zimetolewa na Wakuu wa Taasisi za Kuhamasisha Uwekezaji, (IPA) za nchi wanachama wa SADC, baada ya ziara yao kutembelea Viwanda vya Serengeti Breweries na Bakhresa mara baada ya kumalizika kwa mkutano wao wa siku mbili mjini Dar es Salaam.

Wakiwa kiwanda cha Serengeti, walishuhudia uzalishaji wa kisasa na unaozingatia usalama ambapo Meneja Mkuu wa Kiwanda hicho, Bi. Helene Weesie Amesema kiwanda chake kinazingatia sana, ubora na usalama, ambapo vivyaji vya kiwanda chake ni vinywaji bora kabisa na ni zaidi ya miaka 3, sasa hakujatokea ajali yoyote kiwandani hapo.

Meneja mawasiliano na Mawasiliano na Mahusiano wa Kiwanda hicho, Abass Abraham, ameipongeza TIC kuwatembeza wageni toka nchgi za SADC sio tuu ili kuona uzalishaji bali pia kuangalia uwezekano wa kujifunza kutoka kwetu na kuongeza uwekezaji kutoka nje.

Wakitembelea kiwanda cha Bakhresa, baadhi ya wajumbe wa nchi hizo, walikilalamia kiwanda cha Bakhressa kwanini kimezibagua nchi zao, baada ya kuambia kiwanda hicho kipopo katika baadhi za nchi ikiwemo Malawi, Zambia, Rwanda na Kongo DRC, hivyo kukitaka kiwanda hicho kianzisha viwanda vyake katika nchi zote za SADC.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Bakhresa, Bw. Salim Aziz, Ameipongeza TIC iliyofanikishwa kuanzishwa kwa viwanda vya Bakresa na ni kupitia vivutio vya uwekezaji vilivyotolewa na TIC ndio vimekifanya kiwanda cha Bakhressa kufika hapo kilipo na kusambaa katika nchi nyingine.

Akizungumzia ziara hiyo, Ofisa wa Uhamasishaji Uwekezaji kutoka kituo cha Uwekezaji Tanzania, TIC, Bi. Lilian Mwamdanga, Amesema lengo la ziara hiyo ni ziara ya kimafunzo kwa kuwaonyesha wenzetu kile tulichonacho ili wao wajifunze kutoka kwetu, na utafika muda sisi pia tutawatembelea kujifunza kutoka kewao kwa lengo la kubadilishana uzoefu katika jitihada za kuvutia uwekezaji kwa nchi hizi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Mkurugenzi Msaidizi wa Viwanda kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Mkurugenzi wa Viwanda kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dr. John Mboya amesema mkutano huo umekuwa na mafanikio makubwa sana, ambapo nchi za SADC wamevutiwa sana na Juhudi za Uwekezaji zinazofanywa na kituo cha uwekezaji Tanzania, TIC, ambapo Tanzania inaongoza katika kuvutia uwekezaji wa FDI, hivyo nchi hizi zimekuja kujifunza kutoka Tanzania.

Mkutano huo wa siku mbili, umemalizika kwa ziara ya kutembelea viwanda na umehudhuriwa na wawakilishi kutoka nchi 17 ambapo mwenyeji wa Mkutano huo ni nchi ya Tanzania kupia Kituo cha Uwekezaji Tanzania, TIC.
Paskali.
 

Attachments

  • DSC_0450.jpg
    185.7 KB · Views: 56
  • Photo 1.jpg
    213.7 KB · Views: 46
  • DSC_0488.jpg
    206.3 KB · Views: 43
  • DSC_0497.jpg
    192.9 KB · Views: 58
  • DSC_0516.JPG
    212.4 KB · Views: 55
  • DSC_0519.jpg
    249.4 KB · Views: 48
  • Photo 6.jpg
    183.4 KB · Views: 52
  • poki 9.jpg
    241.4 KB · Views: 52
Kiukweli hiki kituo kinafanya kazi nzuri sana, ila basi tuu!.

Paskali
 
Kiukweli hiki kituo kinafanya kazi nzuri sana, ila basi tuu!.

Paskali
Baada ya Mtu wako kukatwa,Deal la sherehe za kitaifa kubuma.Naona hili ndilo liliokuwa Tawi lako ulilOkuwa umebakiza.Anyway JIFUNZE KULA KWA JASHO.
 
Wakati naufungua uzi nilitegemea nipate takwimu za viwanda, naishia kukutana na "Wakitembelea kiwanda cha Bakhresa..."

Yaan kweli kabisa?! Na #Pascal Mayalla umehitimisha kuwa kituo kinafanya kazi nzuri sana...ni sarcastic statement ama!!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…