Kituo cha Daladala cha Mbezi Stendi upande wa chini, zinakopaki Daladala za Kinyerezi na Bajaji za Malamba Mawili, kuna takataka zimerundikwa kwa muda mrefu sasa zinatoa harufu kali sana, mbaya zaidi Wafanyabiashara wanamwaga hapo matunda mabovu, mboga zilizoharibika na aina nyingine za taka na kusababisha nzi na harufu kali.
Kinachohuzunisha, wakimwaga matunda ambayo wanaona hayafai tena kuuzwa watu wanaotengeneza juisi inadaiwa wanaenda kuyaokota usiku au asubuhi mapema na kuyasaga kwa ajili ya kutengeneza juisi ili waiuze.
Hali ya afya inatishia kwa wanywa juisi lakini kwa watu wanaofika eneo hilo kutokana na harufu kali iliyopo eneo hilo.
Mamlaka husika chukueni hatua muondoe taka hizo. Kipindupindu kipo nje nje.