Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,170
- 5,528
Aliyekuwa mgombea wa Mtaa wa Viwandani kata ya Unga LTD Jijini Arusha kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Jumatano Novemba 27, 2024, Julius Shedrack amejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) akieleza kuguswa na mwenendo wa Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Julius amesema Rais Samia amekuwa akifanya kazi kubwa kwa ajili ya kuliendeleza taifa la Tanzania ikiwamo kuboresha miundombinu na elimu hasa kwenye mikopo ya elimu ya juu.
Amesema licha ya CHADEMA kuonekana kutomuunga mkono Rais Samia lakini nyuma ya pazia wanakiri maendeleo aliyoyaleta tangu alipoingia madarakani.
PIA SOMA
- LGE2024 - Chadema wasema Mgombea wao ateuliwa kugombea CCM