Kitu kikubwa unachopaswa kufanya ni kuwaruhusu wanaotaka kuondoka katika maisha yako waondoke

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Aug 6, 2020
6,167
14,467
Hakuna uamuzi wa busara katika maisha yako kama kuwaruhusu wanaotaka kuondoka waondoke, hii itakupa machungu kwa muda fulani lakini baadae utapona.

Usianze kubembeleza na kusaga meno kwasababu tu mpendwa wako anataka kuondoka katika maisha yako, kumbuka sio kila mtu atakuwa na wewe daima katika maisha haya,,,kuendelea kuamini kuwa kila mtu yupo katika maisha yako daima ni kujitesa bure kwasababu hakuna kitu kama hicho na hakijawahi kuwepo.

Ni ukweli usiopingika yule unaye mpenda akiondoka au kukuacha utapata machungu sana lkn kubali kwamba ndio yameshatokea, hii itakupa nafasi ya kupona na kufuta machozi kisha utakuwa mpya tena

Kumbuka mlango mmoja ukifungwa basi mlango mwengine utafunguliwa,,tena huenda ukawa ni mlango ambao utakupa matumaini makubwa katika maisha yako

MImi ni mpenzi sana wa old school, hawa hapa Boys ll men wanasindikiza ujumbe wangu na mashairi yao murua "End of the road"


View: https://youtu.be/Itdz68o5R5U?si=l5-8Mdus7gBfU580

Ni hayo tu!
 
Kwanini usubiri mtu akuache?
Mimi pindi ninapoona mtu ameanza kutengeneza mazingira ya kuniacha Mimi nawahi kumuacha kabla yeye mwenyewe hajaniacha.

Kama Ni mwanamke anataka kuniacha, nitatangulia kumuacha afu napost Jimbo jipya( new catch) na makopa kopa juu
 
kumbuka sio kila mtu atakuwa na wewe daima katika maisha haya,,,kuendelea kuamini kuwa kila mtu yupo katika maisha yako daima ni kujitesa bure kwasababu hakuna kitu kama hicho na hakijawahi kuwepo.
Ukweli usiopingika kikubwa ni kujiandaa kisaikolojia ili inapotokea maumivu yasizidi sana adi kupelekea kumuona daktari, mbaya hiyo.
 
Back
Top Bottom