Kitendo cha Wananchi kugoma kuhama katika chanzo cha maji Bonde la Mto Ruhila na kuwafukuza Mgambo kwa Mapanga si dalili nzuri

Sep 23, 2024
64
43
Bonde la Mto Ruhila ambalo Serikali limeweka alama zao kama hifadhi ya mto, wananchi wanaendelea kutumia bonde hilo kwa shughuli za kibinadamu kama vile kilimo, kufua na kuoga hata baada ya kulipwa fidia.

Kuna sababu mbalimbali walizozitoa kwanini wanaendelea kutumia maeneo hayo kwa matumizi yao binafsi wakati kuna alama za mawe zimewekwa kuashiria ni mali ya Serikali.

Wamefanyiwa tathmini lakini hawajalipwa ndio sababu kubwa inayowafanya wagome kuachia maeneo hayo kama hifadhi ya chanzo cha maji kwa Mto Ruhila.

Ujio wa Waziri wa Maji, Juma Aweso mnamo Septemba Mwaka 2024 alikabidhi mfanano wa hundi ya Shilingi Milioni 925 ikiwa na maana ya kukamilisha kwa pesa ambayo wakazi walikuwa wanadai.

Mmoja wa wakazi wa mtaa wa Ruhila Seko, Manispaa ya Songea, Hassan Mbunda (kulia), kwa niaba ya wenzake akipokea mfano wa hundi ya Sh. Milioni 925 kutoka kwa Waziri wa Maji, Jumaa Aweso (wa pili kulia) zilizotolewa kama fidia na Serikali kwa Wananchi waliotoa maeneo yao ili kupisha uhifadhi wa chanzo cha maji katika Bonde la Ruhila, Kata ya Seedfarm, Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mwajuma Waziri na wa pili kushoto Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt Damas Ndumbaro, Septemba 2024. (PICHA: RUVUMA.GO.TZ)

Lakini inadaiwa kuwa wachache walilipwa huku wengi wao wakiwa hawajapata kitu na ndio maana wamegoma kuondoka maeneo hayo.

Kuna janja-janja ya Wakazi wa hapo
Kuna taarifa kuwa baada ya tathmini kufanyika, wakati wenyeji wa maeneo hayo wakisubiri kulipwa na Serikali baadhi walianza kuuza maeneo yao kwa watu wengine ambao hawakuwa na ufahamu wa kinachoendelea.

Kutokana na hali hiyo lilipokuja suala la kutakiwa kuhama baadhi wanagoma kuyaacha maeneo hayo licha ya kutakiwa kuondoka.

Walioacha nyumba mapema hawajalipwa
Inaelezwa kuwa baadhi ya Wananchi waliamua kuhama mapema badala ya kutosubiri kuhamishwa, sasa wahusika walipofika ili kulipa fidia wakagoma wakidai hawawezi kumlipa kwasababu wao hawalipi gofu bali nyumba inayotumika.

Swali, je pesa za hao waliohama kabisa zimeenda wapi kwa kuwa walikuwa wameshaingizwa kwenye listi ya wanaotakiwa kulipwa.

Hali ya sintofahamu inaendelea
Kinachoendelea sasa kwenye maeneo ambayo bado yanashikiliwa na Wananchi ni mgambo kufukuzwa na mapanga.

Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Songea (SOUWASA) wanawatumia mgambo kwenda kuwafukuza wanaoendelea na kilimo, matokeo yake kwa hasira walizonazo Wananchi hao wanawafukuza mgambo kwa mapanga.

Ushauri wangu kwa kuwa nimefika eneo la tukio na kuongea na baadhi ya walalamikaji, mamlaka ipange muda wa kuongea nao wananchi hao na ikiwezekane waruhusiwe kwanza kupeleka malalamiko yao na baada ya kuyakusanya waitishe mkutano waweze kuwajibu hadharani mkutanoni.

Kama kuna namna nyingine ya uonevu juu ya malalamiko yao basi wapewe haki yao kuliko purukushani zinazoendelea kati ya Wananchi na Mgambo inaweza ikaleta hatari kwa jamii hata nchi kwa ujumla.

Pia soma ~ DC Wilman Ndile: Kama kuna Wananchi hawajalipwa fidia ya kuhama Bonde la Mto Ruhila waje ofisini milango ipo wazi
 

Attachments

  • IMG_20241221_134141.jpg
    1.4 MB · Views: 3
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…