T Kaiza-Boshe

Member
May 27, 2013
20
39
20230831_154847.jpg

Je, umesoma kitabu hiki? Angalia picha ya gamba (cover) lake kitabu hicho.

Na, je, unajua maana ya usonji?

Kwanza tuujue usonji (Kiingereza, autism)

Usonji ni hali ya kuwa na changamoto za akili zinazoathiri uwezo wa mtu kuwasiliana na kuchangamana na wengine, pamoja na kuwa na tabia ya kurudiarudia vitendo au mambo.

Hayo ni mambo ya ujumlajumla yanayotambulisha usonji. Hata hivyo usonji unatofautiana kwa aina na viwango vya athari kati ya mtoto/mtu na mtoto/mtu. Hivyo, japo kuna wenye usonji wasioweza kufundishika mambo ya taaluma, wapo wanaomudu taaluma ngumu kama tehama (IT); na cha kushangaza, rekodi ya IQ (kipimo cha akili) ulimwengu mzima sasa hivi imeshikiliwa na binti mwenye usonji!

Bahati mbaya, hadi sasa haijulikani kwa uhakika usonji unatokana na nini. Ila kinachojulikana ni kwamba ni hali inayoanza kujitokeza utotoni, na wakati mwingine kwa ghafla, na kuzua imani za kishirikina.

Kwa vile hali hiyo inamfanya mtoto kuwa na uelewa na tabia tofauti na watoto wa umri wake, inakuwa vigumu jamii inayomzunguka kumuelewa.

Hivyo kuna maswali yasiyokuwa na majibu; vivyo hivyo na changamoto za kulea mtoto wa namna hiyo ni nyingi.

Ukweli kumlea mtoto mwenye usonji kunahitaji upendo mkuu, uelewa, uvumilivu, maarifa na kujitoa.

Aidha, kama ilivyo kwa ulemavu mwingine, kuna wanaume wanaowakimbia wake zao na kutelekeza familia kwa kushindwa kumudu, kuhimili, ama kuvumilia changamoto zitokanazo na kumlea mtoto mwenye usonji.

Hivyo mwanamke kumlea mtoto mwenye usonji peke yake kwenye jamii yetu ni safari ngumu kupita maelezo.

Eng. Shangwe Isaac Mgaya ni mwanamke aliyekumbana na hali hiyo, na kuikabili barabara. Tena kwa mafanikio. Kwa bahati nzuri ana uwezo wa kusimulia safari yake hiyo; na ameweza kuweka simulizi ya mapambano yake katika kitabu chake kiitwacho, "SAFARI YA USHINDI YA MAMA NA MTOTO MWENYE USONJI ".

Kitabu kinasimulia kwa kina na ufasaha yaliyomsibu mama huyu katika kumlea mwanaye kwa namna ambayo ukianza kukisoma, hutapenda kukiweka chini hadi mwisho wa hadithi.

Kitabu hiki kinasisimua, kinasikitisha, na zaidi ya yote, kina mafundisho makubwa ya maisha; si kwa wanaoishi na watoto wenye usonji tu, bali hali yoyote isiyokuwa ya kawaida katika maisha ya wanandoa na kulea watoto.

Aidha kitabu hiki kina mafundisho muhimu kwa wanandoa na wazazi watarajiwa, wazazi, wakwe, ndugu, na jamii kwa ujumla.

Hivyo ni kitabu kinachofaa kusomwa na kila mwanajamii.

................................................

Kitabu kinapatikana Dar Duka la Learning Adventures maeneo ya VIJANA house Mwananyamala wanaweza kumpigia +255 768 608 767 au waweza kumpigia mwandishi: 0764547430.
Bei ni shilingi 20,000/=

Kinapatikana pia Amazon kwa bei ya dola 20
Link ya kitabu Amazon: Amazon.com
........................................

Ndimi, Theonestina Kaiza-Boshe
Email address: tkaiza@gmail.com
 
View attachment 2783619

Video ya watoto wanaojibu swali kuhusu makabila yao haihusiani na post yangu kuhusu kitabu cha mama na mtoto mwenye usonji. Video imepop-up wakati nataka kuweka link ya mtoto mwenye usonji na ambaye ni genius wa ajabu; ana IQ kuliko Albert Einstein! Hiyo sikuweza kui-post. Nitajaribu baadae.
 
Vi NGO vya kipigaji hivi mbaya kabisa. Kuwatumia watu wenye matatizo kujinufaisha ni sawa na ujambazi tu.
 
Back
Top Bottom