Abdul Nondo
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 520
- 2,929
Tangu juzi kumekuwa na mjada wa matumizi ya lugha ya Kingereza ,baada ya DC wa wilaya fulani akionekana kuongea kiswahili huku Mchina akihitaji lugha ya kingereza ili kuelewana ila DC alikataa,bahati nzuri moja ya kiongozi upande wa mchina ,akajipa kazi ya kuwa mkalimani.
Jambo hili lilizua mjadala , wengine hadi kunifuata inbox kusema ,DC yupo ,sawa lazima tudumishe lugha yetu ,na tusiwe na akili ya kikoloni ,kwanini wazungu hawaongei lugha yetu?
Hii imenifanya kuandika haya ili watu tuende sawa ,ipo hivi .
Tuelewane kwanza,kudumisha lugha ya kiswahili ,sio lazima kufifiza matumizi ya lugha ya Kingereza,wala kufifiza lugha ya Kingereza sio njia ya kukuza lugha ya kiswahili.
Mikakati ya kudumisha Lugha ya kiswahili ,yalianza mwaka 1969 ,Kipindi cha pili cha mpango wa maendeleo ya miaka 5 ,(second five year development plan) kuliazimia kiswahili kupewa kipaumbele,baadaye Kuna tume ya Rais juu ya maswali ya Elimu iliundwa (Presidential commission on Education) ,na 1982 ilitoa taarifa yake (report) ikasema imegundua kuwa katika kuangalia lugha ipi ipo imara ili kufundishia ,imegundua bado kuna uwezo mdogo wa ku-master au kuelewa lugha zote 2 kiswahili na Kingereza kwa wanafunzi, msomi Deo Ngonyani ameelezea vyema katika maandishi yake. Tume ikapendekeza Kiswahili kitumike kuanzia kufundishia ,kuanzia shule ya msingi hadi chuo ,yaani shule ya msingi, secondary kianze 1985 na kufikia chuo 1992.
Mapendekezo ya tume hiyo yalikataliwa na serikali pia na Chama cha Mapinduzi (CCM) ,na mwaka 1984 Kingereza kikapewa nafasi Kama lugha ya kufundishia (medium of instructions) kuanzia secondary hadi chuo .
Mwalimu alisema hivi,
" if English was not to be used as medium of instruction ,it might die in the Tanzania community , because English is widely used around the world , especially science and technology for the world knowledge.(Deo Ngonyani's work).kwa kifupi Nyerere alisema Kingereza kisipo tumika kitakufa katika jamii ya kitanzania ikiwa Kingereza ni lugha kiulimwengu.
Watu wanaongea ,Mara hooh kwanini wazungu wanatumia lugha yao ,mara kwanini wachina na wa japani wanatumia lugha yao ,mara hoo kwanini tunafumbwa na fikra za kikoloni kujali lugha yao ,na kudharau vya kwetu.
Ni jambo la ajabu sana kudhani kuwa ukitumia lugha yako na kudharau ,kupuuza kingereza ndio uzalendo. tunatumia lugha ya Kingereza sio kwasababu tumeathiriwa na tamaduni ya kikoloni ,ni kwasababu tunahitaji lugha hii kufikia matarajio yetu, hasa ukiangalia maendeleo ya utandawazi ,sayansi na teknoloji ,muinguliano wa mataifa mbalimbali ulimwenguni ,kiuchumi na kidiplomasia.
Kingereza sio lugha ya kikoloni tena ,sababu haina umiliki tena wa kitaifa ,ina umiliki wa kimataifa,ndio lugha ambayo imeunganisha mataifa na mataifa ,imerahisisha muungano wa nchi kikanda na kimataifa,sasa kuna nchi ambazo zinatumia kingereza lakini hazikupata tawaliwa na muingereza.
Mfano,Namibia ilitawaliwa na Germany waka athiriwa na lugha ya Germanic ,baadaye wakawa chini ya Dutch kama sehemu ya Afrika ya kusini baada ya vita ya kwanza ,wakaathiriwa na Afrikaans ,Ila baada ya Uhuru 1990 walitambulisha Kingereza kama lugha ya taifa katika katiba.
Kwa ufupi nchi nyingi za Afrika ,zinalugha zao za kibantu , zingine kifaransa,kireno ila Kingereza kimekuwa pia kikipewa kipaumbele hivyo kufanya nchi za Afrika nyingi kuwa nchi zenye kutumia lugha nyingi au zaidi ya mbili yaani Multilingual countries ,huku Kingereza kikipewa kipaumbele.
Nchi za Afrika ni nchi maskini sana ,zinahitaji kuboresha mahusiano ya kimataifa ili kurahisisha gurudumu la maendeleo ya kiuchumi na Kingereza imekuwa njia rahisi sana ya kudumisha mahusiano, mawasiliano na nchi za ulaya ,Marekani ,Asia na miongoni mwa Afrika.
Hatupaswi kudharau lugha ya Kingereza ,kwa kigezo cha kudumisha lugha ya Kiswahili.Ila ina paswa tuendelee kudumisha lugha yetu ya kiswahili pia kwa kujali, kuthamini na kutambua umuhimu na nafasi ya matumizi ya lugha zingine pia kama kingereza.
Abdul Nondo.
abdulnondo10@gmail.com