mbenge
JF-Expert Member
- May 15, 2019
- 4,825
- 10,405
Leo nikiwa napitia jumbe mbalimbali zinazotumwa ktk mitandao ya kijamii, nimekutana na ujumbe mfupi uliotumwa ili kumfurahisha msomaji lkn ulikuwa hakika ni wenye kutafakarisha.
Ujumbe wenyewe ulikuwa unasomeka, na nina unukuu kama ifuatavyo;
"Wandugu nani ana maunzi laini *(software)* ya kutokomeza mtaliga *(virus) ?* Nataka kusanidi *(install)* kwenye kitumi *(device)* changu aina ya sikanu *(smartphone)* ....nataka niingie mkondoni *(online)* haraka"
Kwa wengi waliousoma umewafanya kufurahia ugumu wa maneno ya Kiswahili na pengine hatimaye kuufuta kisha kuendelea na mambo mengine. Lkn kusema ukweli, maneno mengi ya Kiswahili ni magumu mno kueleweka kirahisi kwa watumiaji wengi wa lugha hii. Acha hiki Kiswahili ambacho tunakizungumza kitaa na kuelewana sisi wenyewe huku tukichanganya "r" na "l"
Nakumbuka kile cha darasani na kwenye mitihani mbona ilikuwa balaa lake ni kubwa, na pia ni ngumu kwa wanafunzi wenye uelewa wa kawaida kufaulu vizuri. Achia mbali maneno kama vile, kiambishi, kishazi, ithibati, kuntu, na mengine kama hayo. Bado mapya mengine yanatokea kutokana na kupanuka kwa teknolojia ya habari na mawasiliano.
Kutokana changamoto ya ugumu wa misamiati iinayoibuka hivi sasa, labda itakuwa ni vyema kukopa neno kama vile lilivyozoeleka kutamkwa kwa lugha ya kigeni, mathalani "live" likatamkwa kwa kionjo cha "laivu" badala ya kama lilivyoletwa na wataalamu wa lugha na kuja na neno "mubashara" na hatimaye "mbashara". Nafikiri muda umefika tuwe na mbadala wa maneno yaliyokuwa magumu mno kueleweka na pia kutokueleweka kwa urahisi, kama vile yalivyotumika ktk ujumbe huo wenye kufikirisha.