Kisutu: Raia wa China, Liang Hu alipa fidia ya TZS 50 milioni kwa kosa la kuua tembo 511 wenye thamani ya TZS 7 bilion, Haika Mgao ahukumiwa mika 60

Determinantor

Platinum Member
Mar 17, 2008
58,133
92,935
'Compare and Contrast bila mihemko' Naomba tujadili bila jazba.

======

Dar Es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam nchini Tanzania imemhukumu, Haika Mgao (26) kutumikia kifungo cha miaka 60 jela baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na meno ya tembo na ya kiboko yenye thamani ya Sh69.5 milioni, mali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mgao ambaye ni mkazi wa Kimara Saranga, Dar es Salaam alikuwa anakabiliwa na mashtaka matatu katika kesi ya uhujumu uchumi namba 69/2018.

Miongoni mwa mashtaka hayo ni kukutwa na vipande vya meno ya tembo na kiboko, bila kuwa na kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyamapori.

Akisoma hukumu iliyoandaliwa na Hakimu Kelvin Mhina, leo Jumatatu Desemba 16, 2019 Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Godfrey Isaya amesema mshtakiwa ametiwa hatiani kama alivyoshtakiwa.

Amesema upande wa mashtaka uliwasilisha mashahidi watatu ambao walithibitisha mashtaka hayo bila kuacha shaka.

Hakimu Isaya amesema ili iwe fundisho kwa watu wengine wanaojihusisha na vitendo hivyo, mshtakiwa atatumikia kifungo cha miaka 20 jela, baada ya kutiwa hatiani katika shtaka la kukutwa na vipande vinne vya meno ya tembo yenye thamani ya Sh66.2 milioni.

"Pia, katika shtaka la kukutwa na meno mawili ya kiboko yenye thamani ya Sh3,310,500, Haika utatumikia kifungo cha miaka 20 jela na shtaka la tatu ambalo ni kujihusisha na biashara ya nyara za Serikali, utatumikia kifungo cha miaka 20 jela" alisema Hakimu Isaya.

Hata hivyo, Hakimu Isaya alifafanua adhabu hiyo kuwa inakwenda kwa pamoja, hivyo Haika atatumikia kifungo cha miaka 20 jela na kwamba kama hajaridhika na hukumu hiyo anaweza kukata rufaa.

Awali, kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon aliiomba mahakama hiyo itoe adhabu kali dhidi ya mshtakiwa huyo kutokana na tembo kupotea kwa sababu ya ujangili jambo ambalo linaathiri uchumi wa nchi.

"Mheshimiwa hakimu naiomba mahakama yako itoe adhabu kali kwa mshtakiwa huyu hasa ukizingatia mali asili zetu hususan tembo wanapotea kwa ujangili jambo ambalo linaathiri uchumi wetu moja kwa moja," alidai Simon.

Katika kesi ya msingi, mshtakiwa alikuwa anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 69/2018 kwa kujihusisha na biashara ya meno ya tembo na Kiboko

Haika anadaiwa kutenda makosa hayo, Novemba 19, 2015 katika eneo la Kimara, wilaya ya Kinondoni.

Anadaiwa katika shtaka la kwanza, siku na eneo hilo, mshtakiwa alikutwa na vipande vinne vya meno ya tembo vyenye thamani ya dola za kimarekani 30,000 sawa na Sh66.2 milioni, bila kuwa na kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyamapori.

Pia, siku na eneo hilo, Haika alikutwa na meno mawili ya kiboko yenye thamani ya dola za kimarekani 3, 310,500, bila kuwa na kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyamapori.

Katika shtaka la tatu, mshtakiwa anadaiwa kujihusisha na biashara ya nyara za Serikali, bila kuwa na leseni kutoka Mamlaka husika.

IMG-20191216-WA0027.jpeg
IMG-20191216-WA0025.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app

======

Hii ndiyo hukumu ya Mchina aliyeua tembo 511 Tanzania

images-2019-12-13T184614.500.jpeg

Mbali na adhabu hiyo, mahakama hiyo imempiga faini ya Sh 300,000 au kwenda jela miezi mitano.Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu Raia wa China, Liang Hu, kulipa fidia ya Sh 50milioni baada ya kukiri kosa la kuua Temboni 511 wenye thamani ya Sh 7bilioni.

Mshitakiwa huyo amehukumiwa kifungo hicho, leo Desemba 13, 2019 na Hakimu Mkazi, Vicky Mwaikambo baada ya kuingia makubaliano na Mkurugenzi wa Mashtaka Tanzania(DPP).

Akitoa adhabu hiyo, hakimu Mwaikambo, alisema mahakama hiyo imemtia hatiani mshtakiwa kama alivyoshtakiwa.

“Hu utatakiwa kulipa faini ya Sh 300,000 au kwenda jela miezi mtano, lakini mahakama hii imekuhukumu kulipa fidia ya Sh 50milioni kwa kosa la kuua tembo” amesema Hakimu Mwaikambo.

Hata hivyo, tayari mshtakiwa huyo alishalipa fidia ya Sh 50milioni, kama alivyoingia makubaliano na DPP.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Ladislaus Komanya kabla ya hukumu hiyo alidai kuwa mtuhumiwa hana kumbukumbu za jinai na ni kosa lake la kwanza.

“Licha ya kuwa mshtakiwa ni kosa lake la kwanza, naiomba mahakama yako itoke adhabu kali dhidi ya mshtakiwa huyu ili iwe fundisho kwa wengine, wenye tabia kama ya mshtakiwa huyu”.

Katika kesi ya msingi, mshtakiwa huyo anadaiwa kutenda kosa hilo kwa nyakati tofauti kati ya Januari mosi, 2013 na Novemba 30, 2013, katika Poli tengevu la Selou lilipo mkoani Morogoro na Iringa.
 
Nani kakuambia hizo tembo zilikuwa za Tanzania tu ,huyu malikia wa tembo alikuwa na Mtandao kutoka Mozambique, Kenya,Malawi, Zambia na Tanzania hizo pembe sio za bongo tu

Huyu alikuwa anatafuta na UN chini ya mwavuli wa UNESCO ,China,USA, UK ,German, Canada na n.k ndio zilitaka Interpol kumkamata na bahati mbaya akakamatiwa huku na mzigo alikuwa anapitisia Mombasa na Beira

State agent
Kwani tembo ni Wa China au wa Tanzania? Lakini Mpwa tuweke hisia kando, kweli tembo wote hao alipe 50m peke yake? Kweli?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mahakama, sheria na wanasheria, kwa pamoja, hivi vyombo vinafanya kazi na kuhitimisha (hukumu)kwa kuangalia mwenendo wa tukio husika, wahusika mmoja mmoja na ushiriki wao, mazingira ya tukio pamoja na utetezi wa wahusika.

Kwa maana hiyo kesi mbili zinaweza zikafanana lakini hukumu zikatofautiana sana kutokana na niliyoyaeleza hapo juu.
 
Namwoma Rais wa awamu ya sita akifoka kwa jazba. Nchi hii imeliwa mno. Ilikuwa shamba la bibi miaka mitano iliyopita. Wanyonge walinyongwa sana lakini haki yao hawakupewa.
Itabidi afumue mfumo mzima wa mahakama na waendesha mashitaka. Huko wamejaa watu wa kanda maalum ya awamu hii. Majaji wamejazwa kwenye mahakama. Mashemeji na wakwe wameula. Itabidi kusafishwe na steel wire.
 
Kwani sheria zetu zinawapa immunity wasio raia? Mfano . Mhehe akiua mtu hapa Tz na kuthibitika pasipo shaka na mahakama pia raia wa Burundi akiua mtu hapa Tz naye mahakama ikathibitisha pasipo shaka . Hawa watu wawili wanahukumiwa kwa sheria tofauti?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom