Pre GE2025 DSM Kisutu: Kesi ya Tundu Lissu leo itaendeshwa kwa njia ya Mtandao. Kila Mtu huru kusikiliza

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,780
56,327
Mahakama ya Hakimu Mkazi Dar es Salaam Inayoketi Kisutu Shauri la Jinai namba 202504102000008606 Jamhuri dhidi ya Tundu Antipace Lissu mbele ya Mhe. Geofrey Mhini, Hakimu Mkazi Mwandamizi.

Tafadhali tumia kiungo (link) kifuatacho kuendela na shauri ya njia ya mtandao>>> JoT - Virtual Court

Shauri limepagwa kwa usikilizaji wa awali leo 24/04/2025 saa tatu asubuhi. Hii ya Uchochezi
Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Chadema, Tundu Lissu alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, na kusomewa shitaka la uhaini.

Tundu anayetetewa kwa sasa na Mawakili sita ambao ni Dk. Rugemeleza Nshalla, Dickson Matata, Jebra Kambole, Michael Lugina, Hekima Mwasipu, na Gaston Garubindi, alisomewa shitaka hilo la uhaini Wakili Nassoro Katuga.

Mbali na Shitaka hilo anatuhumiwa kwa kuchapisha taarifa za uongo kuhusu kuharibiwa kwa uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024, kutumika kwa Polisi kuipa kura na Majaji kutotenda haki kwa kuwa ni wateule wa Rais.

Hata hivyo Mahakama hivyo ilisema haina uwezo wa kusikiliza makosa ya uhaini na kuhairisha kesi mpaka leo April 24, 2024.

Awali Jeshi la Polisi nchini Tanzania lilisema lilimkamata Lissu mkoani Ruvuma kwa tuhuma za kufanya uchochezi wa kutofanyika Uchaguzi Mkuu 2025.

Hata hivyo Jeshi la Polisi limepiga marufuku wananchi kwenda Kisutu kusikiliza kesi hiyo.

====

UPDATES: 10:00hrs

=====

Tundu Lissu akataa kesi yake kuendeshwa kwa njia ya Mtandao kwasababu si kila Mtu ana bando au kifaa cha kuingia online. Hivyo wanaweza kukosa nafasi ya kujifunza sheria inavyo fanya kazi

Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu amegoma kusikiliza kesi ya Uhaini inayomkabili kwa njia ya mtandao hii ni kwa mujibu wa mawakili wake. Lissu alipaswa kufikishwa Mahakamani leo ili kufatilia mwenendo wa kesi hii.

Pia soma > LIVE - Kisutu: Kesi ya Tundu Lissu leo itaendeshwa kwa njia ya Mtandao. Kila Mtu huru kusikiliza

jebra.png


Sasisho kesi ya Lissu kwa Mujibu wa Hilda Newton kutoka mtandao X

Kesi imeanza kusikilizwa Mbele ya Mh. Hakimu Mhini

Mawakili wa utetezi wamefika lakini waserikali na mtuhumiwa watakuwa kwa njia ya mtandao.

Muda huu anaonekana kwenye screen afisa wa magereza (sijui kama ni mkuu wa gereza) lakini Mh. Lissu haonekani. Kesi inaelekea kuanza hapa.

Mawakili wa serikali wanaulizwa wapo tayari nao hawaonekani kwa sasa. Maana wanaendesha kesi kwa njia ya mtandao.

Wakili Mpale Mpoki anasema upande wa utetezi tuko tayari na upande wa serikali walikuwa na taarifa ya kesi na wanajua tarehe ya kesi kwahiyo anasisitiza tuendeleeee

Upande wa Jamhuri tuko tayari, anasikiki Wakili wa Serikali anasema hivyo. Wanaulizwa Magereza mko tayari? Anajibu askari magereza huyu afisa anasema Mshitakiwa amegoma kusikiliza kesi kwa njia ya mtandao.

Anasema nimemjulisha mtuhumiwa na amegoma kusikiliza kesi kwa njia ya mtandao kwahiyo amegoma

Upande wa Jamhuri tupo, Job Mrema wakili wa serikali mwandamizi niko pamoja na

Nassoro Katuga PSA
Cathbert Mbiringi , Tuko tayari kuendelea na Shauri. Shauri lilikuja kwa maelezo ya awali. Ameambiwa atulie kwanza

Utetezi wanajitambulishaa anasema mzee Mpale Mpoki
Alute Mugwai
Ruge Nshala
Peter Kibatala
Jeremiah Mtobesya
Nashon Nkungu
Gaston Garubindi
Deus Singa
Eben Silayo
Deogratias Cosmas Mahinyila
Edson Kilatu
Fredrick Kihwelo
Michael Mwangasa
Catheters Rafael Mandiho
Dickson Matata
Emanuel Chengula
Paul Kisabo
Edward Heche
Jebra Kambole
Maria Mushi
Sisty Masawe
Ikoti Lissu
Fredrick Msaki
Jacob Mogendi
Fikiri Gabriel
Florian Francis
Hekima Mwasipu
Emmanuel Ukashu.

Wakili Mpale Mpoki Anamaliza kutambulisha jopo la Mawakili wa Utetezi.

Wakili wa Serikali Job Mrema anasema yuko tayari kuendelea na shauri ambalo liipangwa kwa ajili ya maelezo ya awali na upande wa jamhuri tuko tayari lakini mshitakiwa hayupo hapo.

Anasema tumewaserve utetezi maelezo ya awali leo asubuhi kupitia wakili Hekima Mwasipu.

Shauri hili lilokuja kwa maelezo hayo na mshitakiwa hayupo mbele ya Mahakama. Kutokana na hali hiyo tuliyoipata kutoka magereza. Kwa upande wa jamhuri tunaomba ahirisho la shauri hili kwa tarehe nyingine.

Ambapo tunaomba kwa upande wa jamhuri tupewe mwezi mmoja kutoka sasa. Watu wanaguna hapa mahakamani.

Anaendelea ili mawakili upande wa utetezi waongee namtuhumiwa ili akubali kuja kusomewa maelezo ya awali.

Hakimu anamuuliza umemaliza au bado?

Anasema Job Mrema Wakili wa serikali kuwa nimemaliza mheshimiwa.

Itaendelea post inayofuata!…..


Anaanza upande wa utetezi Wakili Mpale Mpoki

Anaongea kingereza Ila nitatafsiri hapa.😂

Hata kama Mtuhumiwa aangekuwepo (vituraly) leo, tusingeweza kuendelea kwasababu ingekuwa ni kinyume na sheria kwa sababu sheria inataka maelezo ya awali yafanyike mtuhumiwa akiwepo.

Jambo lingine upande wa utetezi tnajitaji kupata nafasi ya kuonana na mteja wetu. Tumenyimwa kabisa kuonana nae toka amekamatwa kwa ajili ya kumuandaa ili asomewe hoja za awali.

Na sababu za hili kushjndikana ni Magereza kupitia maafisa wake wametukataza mawakili tusionane na mteja wetu licha ya hatua mbalimbali tulizofanya kuonana na mteja wetu Tundu Lissu. Jan na juzi tumekaaa zaidi ya masaa saba na juzi pia tulikaaa masaa nane kuingia na baadae akaruhusiwa wakili mmoja tu kunuona mteja.

Wakili mmoja aliyeruhusiwa kumuona kwa dakika 15 tu na huyo aliruhusiwa kumuona kama ndugu. Hivyo basi nasisitiza hata angekuwepo tusingeleea kwasaabbu hatukuonana na mteja wetu.

Nawaalika Wakili Peter Kibatala na Wakili Jeremia Mtobesya.

Anaanza Kibatala sasa anashukuru. Na yeye anatema ung'eng'e hapa.

Kibatala anasema ataanza na sheria s. 192 ya mwenendo wa makosa ya jinai inasema wazi kuwa

1. Maelezo ya awali yatasomwa kwenye mahakama ya wazi. Yameandikwa kwa herufi kubwa kabisa

Hakimu anasema Kibatala naomba useme taratibu mimi naandika

Kibatala anasema sheria zinasema endapo maneno ya sheria yako wazi na yanaeleweka basi sheria inapaswa kufuatwa kama ilivyo. Kusiwe na janjajanja yoyote.

Na katika kanuni hiyo ya msingi hakuna (exception) ni lazima mtuhumiwa awepo wakati wa kusikiliza Ph

GN. No. 637/2021 inazungumzia kuhusu uendeshaji wa mashauri kwa mtandao. Na hakuna mahali kokote inasema PH isomwe kwa http://mtandao.au mtuhumiwa asiwepo.

Kwa vile tunayo sheria mahsusi CPA inayosema namna Prelkminary hearing (maelezo ya awali) kusomwa basi tutumie sheria hiyo kama ilivyo.

Ni kinyume na sheria na haikubali na ni kujiongoza vibaya sana. Kwa upande wa mahakama kusema Maelezo ya awali yatasomwa kwa mtandao.

Hoja nyingine ni kwamba PH inapaswa kusomwa mbele ya Mtuhumiwa na sio tu mbele yake inasema sheria iwe kwneye mahakama ya wazi.

Nimeanza kuelewa hapa anayosema Kibatala pengine Lissu amekataa kwasababu anajua alipaswa kuletwa mahakamani ndio maana amewagomea Magereza. Huu mpambano mtamu sana.

Kibatala anasema ili tuisaidie mAhakama kutafsiri vizr kifungu cha 192(1) tunaomba isome 192(3) inasema mwisho wa yote hayo baada ya hoja za awali kusomwa PH mtuhumiwa atapaswa kusign memorandum

Mawakili wake watasign na mawakili wa serikali watasign

Sasa hapo neno la msingi ni lazima Memorundum iwe signed. Sasa mtuhumiwa hayupo hiyo memorandum tutampatia bodadboda apeleke magereza halafu aturudishie hapa mahakamani

Hii inaelezea kuwa lazima mtuhumiwa awepo maana ipo nyaraka ambayo atatakiwa kuisign hapa mahakamani.

Hoja nyingine anaendelea Kibatala

Baada ya PH kukamilika. Kunawezekana kuwepo kwa kutolewa vielelezo. Sasa Kanuni ya 5(3) kanuni za kuendesha mtandao inasema kama shahidi anataka kutoa kidhibiti lazima awepo mwenyewe.

Sasa kama itahitajika kuna kidhibiti kitolewe wakati wahusika hawapo kwa kipindi hiki. Kwahiyo inathibitisha kuwa tukiendelea kufanya hapa chochote yatakuwa ni mambo ya hovyo na sheria haitaki hivyo.

Maombi yetu tutayatoa baadae.

Sura nyingine ya pingamizi letu ni kwamba mahakama hii Ni Functus Officio ilishaamua kuwa PH Itafanyika live na mtuhumiwa atakuwepo.

Wakili Kibatala : Sasa haya mambo ya leo kuwa mtuhumiwa hayupo yanatokea wapi, mahakama ilisema mtuhumiwa atakuwepo hapa na mambo haya yalisemwa hapa mahakamani.

Kwahiyo mahakama inalazimika kumfanya mtuhumiwa kuwepo ili mambo yaendelee kama yalivyo pangwa.

Sheria zote nilizotaja hapo zinapaswa kuendana na rule ya Functus Officio kwahiyo mwenendo wa shauri la leo ni kuvunja kanuni kwanuni rule 4 ya kuendesha shauri mtandaoni ilipaswa kuwepo amri ya mahakama kisheria. Na imetolewa kwa pande zote.

Na kama kungekuwa na ulazima wa kusikiliza kwa mtandao tulipaswa kuambiwa

Wakili Kibatala anaendelea kuongea-; Rule 10 No. GN 367 na Hekima Wakili atasema. Tulitumiwa message ya kawaida kuhusu kusikilizwa kwa kesi hii saa tatu usiku.

Sasa haya yote ni nini saa tatu usiku unatutumia message kuwa kesi itasikilizwa kwa mtandao. Je hatuvunji sheria hapo? Rule 10 niliyosema inasema Mahakama ilipaswa kutoa siku 7 kabla taarifa ya kesi kusikiliza kwa mtandao.

Sisi tumepewa taarifa saa tatu usiku jana. Sasa hapo hatuvunji sheria. Hakuna taarifa yoyote (notice) haipo. Uwepo wa notice ni fair hearing kama notice haipo maana yake fair hearing haipo.

Kwahiyo uendeshaji wa shauri hili hauwezi kuwa wa haki na wa maana kama taarifa za namna kesi itasikilizwa zinatolewa kama message za wapenzi kusalimiana na kutakiana usiku mwema. Haikubaliki.

Wakili Kibatala anaupiga mwingi sana mpaka Mawakili Serikali wamepotea hewani 😂

Wakili wa Serikali Wakili Job Mrema kumbe alikuwa hasikilizi anaongea na simu huko ofisini kwao. Tunamuona live kwenye screen kubwa hapa Mahakamani. Watu wanacheka sana😂😂😂

Hakimu anauliza mnafuatilia kweli Mawakili wa Serikali naona unaongea na simu tu hapo.

Wakili wa Serikali Job Mrema anachekesha sana ni kama anaelekezwa jambo kwenye simu, Mahakama imesimama hapa kwa muda. Mambo ya ajabu kabisa. Hawa watu hawa nidhamu kwakweli.

Mawakili wa utetezi wamekerwa sana na kitendo cha mawakili waserikali wanaongea tu na simu huko

Wakili Kibatala anaendeelea, hakimu kasema we endelea acha wasisikilize.

Kanuni ya 10 pia inasema pia hiyo notice ya siku 7 tuliyopaswa kupewa inapaswa kujunuisha mambo mengi ikiwemo ni muda gani kesi hiyo itasikilizwa na mambo mengine kama vile marejeo kadhaaa ya kisheria. Kwahiyo notice ni muhimu na inahitaji mambo mengi.

Wanasheria watapeanaje kesi za marejeo kama hawatakuwa wanaonana. Ndio maana notice inatakiwa siku 7.

Sasa leo mkuu wa gereza anatuambia kuwa Lissu mtuhumiwa kagoma. Wakilili Kibatala anauliza Tunamuaminije yeye? Yeye ni rafiki yake LISSU au ndgu yake? Hatuwezi kumsikiliza yeye hapa.

Amerudi wakili wa serikali anasema hapo mwisho hatujamsikia wakili kibatala arudie.

Watu wanacheka 😂😂😂

Kibatala anasema mimi na mawakili wenzangu tulienda Jela, Ukonga Prison. Niliruhusiwa mimi tu 22/04 na mtuhumiwa aliniambia yafuatayo.

Siwezi kushiriki kwenye mwenendo wowote kwa njia ya mtandao ambao utakuwa kinyume na sheria. Hayo maneno aliniambia lissu mwenyewe kama wakili wake.

Na alisema hawezi kukubali shauri lake lisikilizwe kinyume na sheria. Kwahiyo msishangae leo kuwagomea huko magereza anasema fuateni sheria atakubali kusikiliza kesi yake. La sivyo hatakubali kabisa.

Kibatala anasema, Job Mrema anaomba ahirisho la siku 30 sasa hili ahirisho analoomba ni vituko. Haliko kisheria kabisa.

Anaendelea Kibatala-; Tusingeweza kuahirisha shauri kwa sababu zilizotolewa eti kwa siku 30 zote. Yani anaomba siku 30 tuahirishe kwasababu zipi? Kwanza ni mamlaka ya mahakama kujua kesi inaahirishwa kwa siku ngapi? Ameomba mambo hayapo kisheria. Na mahakama ikiamua lazima ahirisho liwe kwa kipindi kifupi sana.

Na sisi tuko tayari kuwepo kesho. Ahirisho hilo liwe hadi kesho. Tukutane hapa kesho. Na sio hizo siku 30 kama wanavoomba upande wa Jamhuri.

Wakili Kibata anaendelea

Anasema Job Mrema pia ameomba mambo ya kitoto sana hapa mahakamani. Sisi Mawakili tumezuiwa kumuona Mteja wetu kama Mawakili. Kwa mujibu wa sheria huko magereza ili tumuondae mteja wetu. Sasa leo Wakili wa serikali anadai eti mtupatie nafasi tukamshawishi mteja wetu akubali. Tunatumia njia gani? Mizimu au uchawi maana Magereza hawaturuhusu tunaenda kuongea nae vipi?

Katiba inasema mtuhumiwa achukuliwe hana hatia. Haya matendo yanayoffanyika hapa hayaeleweki kabisa. Akija Mzee Alute Lissu Wakili ataendelea eneo hilo.

Itoshe kusema kuwa ombi letu ni kwamba mahakama hii ina wajibu mtuhumiwaaliyepo Ukonga anapata haki yake ya kukutana na Mawakili Wake. Na tunaomba mahakama hii itoe amri kuwa waseme kwanini wametuzuia mawakili kumuona.

Mkuuu wa Jeshi la Magereza Dar es Salaam na Mkuu wa Gereza la Ukonga Wote waje waeleze Mahakamana kwanini wametuzuia mawakili tusiende kumuona.?

Pia tunaomba Mahakama itoe amri kwanini ndugu wa Lissu na mawakili wamefanyiwa matendo ya hovyo na Mapolisi. Wakiwa wanaingia hapa mahakamani.

Kwanini Mapolisi leo wapo wengi hapa Kisutu. Wanawazuia ndugu wa Lissu. Je mahakama iliambiwa kuwa wateja wa mahakama na ndugu wa Lissu watasumbuliwa leo. Je mahakama inafahamu hayo yakiyofanywa na Mapolisi.

Hakuna maombi yoyote (application) kwenye hii mahakama kuwa umma hautaruhusiwa kwenye mahakama hii. Kama ambavyo kifungu cha 186 cha CPA kinachosema umma unayo haki ya kuhudhuria mahakama ya wazi na kuangalia kesi.

Sasa hakuna order yoyote ya mahakama na sisi tunaiomba mahakama iwape haki yao ya msingi ndugu wa Lissu, marafiki wa Lissu, Mawakili wake na umma wote uhudhurie mahakamani kwa mujibu wa sheria ili haki si tu itandeke bali ionekane ikitendeka.

Anamalizia Wakili Kibatala kwa kusema Mahakama ya wazi ni haki ya msingi sana na mahakama iwe na wivu sana kulinda jambo hili kisha anamkaribisha JEREMIAH MTOBESYA.

#UPDATES_KESI_PART5


Wakili Kibatala amemaliza, sasa tunakuja kwa Wakili Mtobesya.


Anasimama Wakili Mpale Mpoki anasema tunaye observe kutoka Kenya Wakili Mwenzetu, @MarthaKarua . Lakini pia yupo Wakili Ferdinand Makore na Michael Lugina kwa upande wa utetezi.


Haya anaendelea Mtobesya anasema atakuwa na mambo matatu.


Hakimu anawauliza mawakili wa serikali mbona kama mmelala mnasikia kweli. Anajibu Wakili wa serikali kuwa kwani anaongea nani kwa sasa mheshimiwa. Kicheko kidogo.


Anaendelea Mtobesya.


Mtobesya anasema S. 192 inasema kuhusu mahakama ya wazi imetolewa maana yake kwenye sheria hiyo CPA ukisoma 186(1) maana yake ni mahali ambapo umma utakuwa huru kufuatilia. Sasa hii habari ya kusikiliza kwa mtandao kwa mujibu wa kanuni za kusikiliza mtandao ni wahusika tu wa kesi na sio umma.


Kanuni ya 8 inasema obeservers wataruhusiwa kushiriki kesi kwa njia ya mtandao hadi mahakama itoe amri sasa huwezi kusikiliza kesi ya jinai kama hii kwa mtandao wakati kanuni husika hazitoi nafasi kwa umma kushiriki.


Sasa PH inasikilizwaje kwa mtandao. Wakati sheria inasemi hizi kanuni zitatumika kwa kuzingatia masharti ya mwenendo wa kusikiliza makosa ya jinai. Sasa kama matakwa ni kesi kusikilizwa mahakama ya wazi hizi kanuni za kusikiliza mtandao haziwezi kutumika kabisa.


Mtobesya anasema naishia hapo kwenye eneo hilo.


Lakini eneo lingine, amesema Kibatala kuwa zoezi la PH lazima memorandum iandaliwe na iwekwe sahihi. Sasa s. 192(4) inasema kuna mambo yakisomwa na kukubaliwa na mtuhumiwa yatachukuliwa kuwa yamethibitishwa na hayatahitaji kuletewa ushahidi mwingine.


Sasa mchakato wa kuweka sahihi sio mchakato mdogo na ambao hauna maana. Ni zoezi muhimu sana kisheria. Sio zoezi la kupoteza muda.


Sasa PH isingewezekana kuendelea kwa mtindo huo. Mtuhumiwa ni muhimu awepo hapa. Wenzetu sijui wanasoma sheria za wapi? Maana mambo haya yako wazi na yanafahamika. Hawako serious.


Vifungu vyote tulivyosema hapa mahakamani vinathibitisha kuwa mambo ya kusikiliza kesi hii kwa mtandao hayawezekani kwa mujibu na matakwa ya sheria. Tunaomba mtuhumiwa aletwe mahakamani ili tufanye kazi hii kwa mujibu wa sheria. Na Bahati nzuri tunaomtetea na sisi sio vilaza tunayafahamu mambo haya vizuri. Naomba kuishia hapa. Kwenye eneo hilo.


Jambo lingine naomba kusema kuwa Lissu kutokuwepo hapa nashangaa kwa kesi hii iliyopo hapa yuko nje ya dhamana maana hii kesi hapa sio ya uhaini.


Kwahiyo wakati mahakama inaahirisha kesi hii inasema mtuhumiwa ataendelea kuwa huru hadi tarehe nyingine. Sasa hawa magereza kwa vile wananshikilia kwa kesi nyingine basi kwa kesi hii walipaswa kumleta mahakamani.


Sasa hata kesi ambayo yuko nje ya dhamana nayo hawataki kumleta. Hii ni nini? Unashangaaa anaomba ahirisho la siku 30 kivipi yani?


Wanateta kidogo hapa. Kuna kitu anaambiwa mtobesya na Mpoki.


Mtobesya Anasema amemaliza, sasa anaingia Wakili Allute Mugwai Lissu


Part 6 itaendelea post inayofuata!…

#UPDATES_KESI_PART6

Anaingia Wakili Msomi Mzee Alute Mugwai, anasema Roll No. 516 nimefanya kazi ya uwakili kwa miaka zaidi ya 40.

Watu wanacheka 😂😂😂😂

Anasema naungana na Kibatala na Mtobesya na naomba niwe kwenye record kuwa nilifika Ukonga Prison saa tano asubuhi kumuona Lissu.

Niliende kumuona Mr. TUNDU Lissu ili anipe maelezo yoyote kuhusu kesi yake ya leo. Lakini sikupata nafasi ya kumuona na nilikaaa zaidi ya masaa 7 hadi saa 11 jioni na kunifukuza eneo la gereza.

Hilo lilifanywa hata baada ya mimi kujitambulisha na kuwaonesha vitambulisho vyangu. Nimewaambia mimi ni wakili tena wa miaka mingi nimesema hapa na nikawaambia mimi ni Kaka wa Damu wa huyo mteja wangu. Na nimesafiri kutoka Arusha hadi dar es salaam kuhudhuria hii kesi dhidi ya mtuhumiwa.

Naunga alichosema Kibatala kuwa pia 22/04 alifanikiwa kumuona pale magereza na aliongea nae kupitia uzio wa vioo na alipewa simu wakawa wanaongea kwa simu huku wanaonana na mtuhumiwa huku asimimamiwa na maaskari magereza wanne.

Wakili wako nyuma ya Kibatala na wawili nyuma ya Lissu. Haya matendo ni ya hovyo kabisa na yanadhariridha kazi ya uwakili.

Kwani kanuni ya 13 ya prison regulation GN. NO. 19/1968 inasema kila mtu aliyepo magereza kwa maana ya mtuhumiwa anapaswa kupewa nafasi ya kuongea na mawakili wake na magereza wanapaswa kuhakikisha mawakili wanaongea kwenye eneo linaloonekana lakini sio kusikiliza maongezi ya mtuhumiwa na Wakili wake.

UN General assembly resolution (Body of principles for protection of all persons in any form of detention) No. 43/173 ambayo ukisoma principle no. 18 inasema Prisoners ana haki ya kupewaanfasi kuonana na mawakili wake, apewe muda wa kutosha na vifaa ili kuzungumza na mawakili wake, haki za mtuhumiwa na prisoner huyo zipewe ndani ya muda na mazungumzo yake yawe ya siri kabisa. Confidentiality rule inataka hivyo.

Hii resolution inatumika hata Tanzania kwa sasa maana tulisharidhia

Mzee Alute anaendelea kuwa, maaaskari magereza hawapaswi kusikiliza kabisa.

Sasa huyu wakili wa serikali anayeomba tuahirishe hilo jambo lingekuwa na maana kama haki za msingi za mawakili zingekuwa zimesimamiwa. Unatuambia mambo ya mbele wakati huku nyuma kuna uchafu mwingi kabisa. Ni sawa na dereva wa baskeli ametangulia mbele halafu uantegemea baiskeli ijiendeshe kutoka nyuma yenyewe na ufike safari unayoenda.

Pia siku ya Pasaka na hata ijumaa kuu na hata jana kule Ukonga, Kiongozi wa Dini Joseph Muyunge alienda lakini mahabusu wengine waliruhusiwa kusali nae isipokuwa mteja wetu.

Na iwe kwenye record kuwa Pope amefariki sisi ni wakatoliki hata hilo hajaambiwa na amenyimwa haki zake za msingi za kusali na kumuomba Mungu wake. Hii ni nini kama sio Unyama na kinyume na sheria za Tanzania na za Dunia yote.

Mzee Allute amemaliza sasa anaingia Wakili Mpale Mpoki

Part 7 itaendelea post inayofuata!….

#UPDATES_KESI_PART7


Sasa anaingia Wakili @MpaleMpoki


Anasema maombi yetu ni haya yafuatayo;


1. Lolote linalohusu mteja wetu basi lifanyike kwa mujibu wa sheria. Mteja wetu alipelekwa Keko Prison na baadae akapelekwa Ukonga. Hatujui na mahakama haijasema lolote. Tulifkkiri mahakama ingekuwa ya maana basi ingetueleza hata mawakili wa mtuhumiwa kuwa ndugu yenu amehamishwa.


Hivyo lolote likifanyika bila utaratibu hatutakubali mfano mwingine ni hili na kesi kusikilizwa kwa mtandao nalo halijafuata sheria kabisa. Tjnahitaji kupewa notice na taarifa yoyote ya hizi kesi.


2. Jambo lingine ni suala la Open justice. Hii mahakama ya wazi ni jambo linalofanya mahakama iwe ya maana. Hiki chombo kimebeba haki za watu na matumaini yao. Hakuna kimachofichwa mahakamani. Hapa hatufanyi matambiko wala uchawi. Tuuachie umma ufuatilie kila kitu. Na kesi hii ijiamue yenyewe kwa uwazi.


Sifahamu ambae amezuia waandishi wa habari kuingia mahakamani. Hao waaandishi ni kiungo muhimu kati ya Mahakama na umma. Sasa waandishi wakinyimwa maana yake tunataka umma uamue kesi hii wenyewe. Kwanini hamjaweka speaker nje ili umma usikie na kufuatilia.


3. Mtuhumiwa ana haki ya kupata chakula kutoka nyumbani lakini yeye amekatwa kupokea chakula kutoka nyumbani hasa ukizngatia hali yake ya afya pia anahitaji uangalizi mkubwa wa kiafya. Huyu mtu amepigwa risasi nyingi sana mwilini wake. Kwanini anyimwe kupelekewa chakula wakati sheria inaruhusu. Anayepika sio magereza wala serikali ni ndugu zake na wanapeleka wenyewe na sheria inaruhusu kabisa.


Na naomba kusisitiza huu utaratibu wa kunyima watu kuingia mahakamani na waandishi kutoingia pia ni suala linalote tafsiri tofauti sana.


Wakili Mpale Mpoki amemaliza sasa anaingia Wakili wa Serikali Job Mrema


Anaingilia Kibatala anasema naomba radhi kuingilia. Mheshimiwa anasema endelea.


Kibatala anasema naomba waongee na wao kingereza maana humu ndani wako mabalozi na observer kutoka nje ya nchi.


Mheshimiwa anasema hayupo anayetaka kusikiliza kwa Kiswahili? Kibatala anajibu kuwa wote waliokuwa wanataka kusikiliza kwa kiswahili wamewakamata wako Polisi hawajaingia mahakamani wamekamatwa na Polisi.


Nassoro Katuga anasema kwa faida ya watanzania tutaongea kwa Kiswahili, Kibatala anamuuliza watanzania gani hao?


Watu wanacheka hapa mahakamani😂 haya majamaaa hayajui kingereza ni vilaza aiseeee.


Haya anaendelea Nassoro Katuga Wakili wa serikali kuwa kwa waliosema wenzetu tunaomba tupewe muda kidogo tujiandae halafu tutarudi kujibu. 😂


Nassoro Katuga amesema anamaombi matatu kabla hawajajibu chochote.


1. Ombi la kwanza ni hilo anaomba ahirisho dogo wajiandae chakujibu. Naona wanataka kupewa maelekezo kutoka juu. Ameulizwa mnajiandaa nini wakati kila kitu kipo wazi mtujibu. Akasema anahitaji kuongea na mamlaka zingine ili ajue atasema nini.


Mamlaka hizo amesema kama vile magereza maana wao magereza hawana nafasi ya kujitetea hapa kwahiyo acha aongee nao.


Wakili Mtobesya anaingilia anasema hivi mheshimiwa huyo anaongea nini hatumsikii kabisa. Hakimu anasema aanze upya kuzungumza.


Kiukweli Mawakili wa serikali hata hawasikiki kabisa. Mitambo inakoroma tu. Watu wanasonya


Nasoro Katuga anasema ombi lao la pili


2. Ombi la pili anaomba nyaraka ambazo wamepatiwa mawakili wa utetezi wasizisambaze huko mitandaoni wanaona kama zinasambaaa. Mawakili ni maafisa wa mahakama. Wasisambaze. Vinaibuka vicheko kwa mawakili wa utetezi


Anasema maombi yao kwa sasa ni hayo mawili tu.


Hakimu anasema mnasemaje watetezi


Wakili Kibatala anasema mimi nitajibu kwa kingereza


Anaendelea kutema ung'eng'e


Haya maombi waliyoomba sio ha kisheria kabisa. Kwanza hayaelewi ahirisho fupi ni lipi? Wanataka masaa manne au matatu na hadi kesho au masaa kumi. Sasa hawajasema mahakama inaahirisha kwa muda upi ambao wao hawajasema.


Lakini wao walisema wakati tunaanza kesi kuwa wako tayari kuendelea. Sasa walikuwa tayari kuendelea na niniwakati sasa hivi wanasema wanaomba muda tena.


Part 8 itaendelea post inayofuata!…

#UPDATES_KESI_PART8

Anaendelea Wakili Kibatala

Hao askari magereza wangeuliza mambo haya kabla ya kuingia mahakamani.

Jambo la pili kuhusu kutosanbaza nyaraka wanasema hili nalo ni ombi ambalo ameshangaa linatoka kwa mtu ambae ni Wakili tena wa serikali. Sheria gani inazuia tusisambaze hizo nyaraka.

Sisi mawakili tunayo haki kuwapatia wateja wetu nyaraka zote zinazohusiana na shauri lao. Sasa atuambie aliyesambaza ni wakili au mteja. Vyovyote itakavyokuwa je ni kosa kufanya hivyo?

Maombi haya mawili tunaona hayana msingi wowote kama sisi tulivyosubmit hapa mahakamani na wao wafanye hivyo hivyo tuendelee. Kwanini sisi tuliyosema si tulishauliza kabla hatujaingia mahakamani. Kuwaruhusu ni kutupotezea muda tu.

Hakimu amefuta jasho na anaendelea kuandika.

Kuna ka kimya kidogo hapa Mahakamani. Ni kama watu wanakereka tu mambo yanavyokwenda. Mawakili ni wengi wameongezeka ambao hawakutanvulishwa awali. Sijui kama watatambulishwa.

Mahakama imeanza tena. Hakimu Mhini anauliza Mawakili wa serikali kama wapo online. Anawaita hawaitiki kabisa. Hawapo. Sijui ndio wameshaenda kujiandaaa. Mawakili wa utetezi wanakasirika wanasema hawa wanatuletea dharau.

Tunawaona kwa screen hawa Mawakili wa serikali wanachart tu

Hakimu anaendelea, Mh. Mhini anasema nimesikiliza maelezo kutoka pande zote kuhusu maombi haya

Nitawapa nafasi kwa kuahirisha shauli hili ili tuje kuwasikiliza pande zote. Na ninatoa katazo maelezo ya awali kabla hayajasomwa mahakamani.

Pia tukikutana baadae tutaendelea kwa njia ya mtandao tarehe 28/04 na kesi hii itasikilizwa kwa mtandao pia siku hiyo. Mawakili wanashangaaa hapa. Wanatikisa kichwa.

Nasisitiza siku hiyo mtahudhuria mkiwa huko huko mtakapokuwa Mawakili wanashangaaaaa!….

Kesi ya Kwanza ya Mhe. Lissu imeisha ambayo ni ile ya Uchochezi jinai Na. 8606/2025 badae kidogo tunaingia kwenye kesi ya pili ambayo ni kesi ya UHAINI.
20250424_114940.jpg
20250424_114934.jpg

Hilda Newtown courtesy
 
Kesi ya Lissu itasikilizwa kwa njia ya mtandao fuata maelezo haya

Mahakama ya Hakimu Mkazi Dar es Salaam Inayoketi Kisutu Shauri la Jinai namba 202504102000008607 Jamhuri dhidi ya Tundu Antipace Lissu mbele ya Mhe. Franco Kiswaga.

Tafadhali tumia kiungo (link) kifuatacho virtualcourt.judiciary.go.tz/kisutu kuendelea na shauri kwa njia ya mtandao. Shauri limepagwa kwa kutajwa leo 24/04/2025 saa tano asubuhi.

Hii ya Uhaini.
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Dar es Salaam Inayoketi Kisutu Shauri la Jinai namba 202504102000008606 Jamhuri dhidi ya Tundu Antipace Lissu mbele ya Mhe. Geofrey Mhini, Hakimu Mkazi Mwandamizi.

Tafadhali tumia kiungo (link) kifuatacho kuendela na shauri ya njia ya mtandao>>> JoT - Virtual Court

Shauri limepagwa kwa usikilizaji wa awali leo 24/04/2025 saa tatu asubuhi. Hii ya Uchochezi
Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Chadema, Tundu Lissu alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, na kusomewa shitaka la uhaini.

Tundu anayetetewa kwa sasa na Mawakili sita ambao ni Dk. Rugemeleza Nshalla, Dickson Matata, Jebra Kambole, Michael Lugina, Hekima Mwasipu, na Gaston Garubindi, alisomewa shitaka hilo la uhaini Wakili Nassoro Katuga.

Mbali na Shitaka hilo anatuhumiwa kwa kuchapisha taarifa za uongo kuhusu kuharibiwa kwa uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024, kutumika kwa Polisi kuipa kura na Majaji kutotenda haki kwa kuwa ni wateule wa Rais.

Hata hivyo Mahakama hivyo ilisema haina uwezo wa kusikiliza makosa ya uhaini na kuhairisha kesi mpaka leo April 24, 2024.

Awali Jeshi la Polisi nchini Tanzania lilisema lilimkamata Lissu mkoani Ruvuma kwa tuhuma za kufanya uchochezi wa kutofanyika Uchaguzi Mkuu 2025.

Hata hivyo Jeshi la Polisi limepiga marufuku wananchi kwenda Kisutu kusikiliza kesi hiyo.
Haya sasaaaa!!! Kwa Sauti ya DJ Mark Kutoka Mtaa wa Uhuru Congo Kariakooo.
 
Back
Top Bottom