Kisiasa huwezi ukampuuza Haji Manara na ukamkumbatia Ali Kamwe na ukafanikiwa

Asante CCM

JF-Expert Member
Jun 22, 2023
527
1,902
Haji Manara ni binadamu mwenye connection na watu wengi wafanya siasa na wasio wafanya siasa. Kwalo, inatosha kukupa tija kwa lolote utakalo lifanikiwe.

Bahati mbaya yupo kijana kwa kujulikana ghafla na kupata vi nafasi fulani huko Duniani imempelekea kumwona gwiji wa propaganda Haji Manara ni kiumbe cha kawaida kwenye uga huo. Mbaya zaidi na kwa kiburi kisichotarajika akaamua kumtweza!

Ndugu kijana, tambua kwa kumpuuza mwana propaganda mzoefu kama Manara ni ngumu kwako kutoboa.

Manara ni rafiki mkubwa hata na wana-michezo kama;

Aziz Ki, Chama, Pacome, Diara na mastaa kibao kwenye timu kama Yanga na anao ushawishi kwao wa kuwafanya wakuonyeshe si lolote si chochote kwa rafiki yao Manara.

Uwanda mpana wa siasa za wana-siasa wa Vyama na michezo bado unamhitaji sana mfanya propaganda mkongwe kama Manara na si vijana kama kina Kamwe.
 
Huyu bwana ako kama unampenda sana kampe mamako Yanga tushampunguza
 
We utakuwa mke wa ngapi wa Haji maana naye anaoa kila mara na kuacha. Nyie wanawake hamjui mambo ya mpira.
 
Mchukueni Manara taifa stars aipe kombe la dunia kwa propaganda zake, kwani nyie ccm hamlitaki kombe la dunia?
 
kaka kwani vipi hapo mbona kama kamwe anawatisha zaidi ya huyo manara anajuwa huyo.
 
Sema ally kamwe amezidi mipaka ashawahi kujaribu kugombanisha uongozi wa Azam media na mashabiki wa yangu nikasema huyu jamaa anajiona atakaa hapo yanga mda wote
 
Watu wachache sana watalifahamu unalosema ukweli haji manara asinge nyamaza kimya kwa propaganda za kufungwa sindano Wala mambo mengine.
 
Kwahiyo anacheza manara uwanjani!
 
Kwanza haya maujinga ya kua na mropokaji na msema ovyo wa club dunia nzima hayapo. Wabongo ni nani katuroga kupenda imani za kijinga namna hii na kuwapa umuhimu watu wasiohitaji huo umuhimu???!

Sajilini wachezaji, wekezeni kwenye ubora wa kikosi na nidhamu ya team muone kama hamtopata matokeo. Inasikitisha sana tunawapa umuhimu akina Kamwe na Manara katika mambo yasiyowahusu. Umeona wapi Man City, Barca, Madrid, Liver, etc zikawa na ujinga wa kutegemea walopokaji ili kupata matokeo chanya uwanjani??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…