Kisauji (babu wa TikTok) afungiwa miezi sita

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
2,168
5,523
1721679836887.png

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limesema limejiridhisha kuwa Seif Kassim Kisauji maarufu Babu wa TikTok ametenda kosa la kimaadili wakati akitekeleza kazi zake za sanaa na limefikia maamuzi kumfungia kutokujishughulisha kufanya kazi za sanaa ndani na nje ya Tanzania kwa kipindi cha miezi sita kuanzia leo July 22,2024 na kumtoza faini ya Tsh. milioni 3 ambayo anatakiwa kuilipa ndani ya siku 7 kuanzia leo.

Baraza limesema limefikia uamuzi huo baada ya kumuita Kisauji kuhusiana na ukiukwaji wa maadili akiwa kama Msanii aliyesajiliwa na Baraza la Sanaa la Taifa kwa usajili Na. BST-9684-2023-2154 ambapo ukiukwani huo wa maadili ni kinyume na Kanuni ya 25 (6) ya Kanuni za Baraza la Sanaa la Taifa za mwaka 2018 na Mwongozo wa Uzingatiaji wa Maadili katika Kazi za Sanaa wa Mwaka 2023.

“Baraza la Sanaa la Taifa kupitia Sheria Na. 23 ya Mwaka 1984 na Maboresho yake ya Mwaka 2019 ina mamlaka ya kusimamia maadili ya msingi kwenye Sekta ya Sanaa kwa Kanuni ya 25(1)-(8) ya Kanuni za Baraza la Sanaa la Taifa za Mwaka 2018”

“Baraza limekwishatoa na kuzindua mwongozo wa maadili katika kazi za sanaa ambao unapatikana katika tovuti yetu basata.go.tz, hivyo ni jukumu la kila Msanii na Mdau wa Sanaa na jamii kuzingatia maadili katika kazi za sanaa”

UPDATE
- Dkt. Ndubaro amuongezea faini babu wa TikTok
 
Mbona hlijatajwa kosa hasa ni nini
Basata! Hukumu bila kuujulisha umma kosa lilikuwa nini..
Kuna video ilitumwa Juzi ikiuonyesha amekaa kwenye kiti halafu kuna dada amekaa juu ya "boloyoung" akikatika huku akinyonywa kifuani na binti then demu akainama kisha Babuu kisauji akawa anamchapa makofi kwenye "MATTERCORE".
 
Back
Top Bottom