Kisa katika sehemu ya maisha halisi

A.MTALE

Member
Aug 15, 2012
44
23
Mtale Kwanini unaomba ndoo kwa huyo bimkubwa huku ndoo zimejaa ndani?.

Ni swali aliniuliza mfanyakazi mwenzangu niliewahi kuishi naye kwenye nyumba moja.

Kisa katika moja ya maisha halisi ya A.Mtale.

Wakati nimemaliza masomo yangu ya shahada ya kwanza huko Dodoma niliajiriwa na shirika moja lililokuwa likifanya shughuli ya kuwahudumia wakimbizi linaloitwa Doctors Without Borders katika kambi ya wakimbizi Nyarugusu huko Kigoma kabla ya sijahamishwa kurudishwa Masaki Dsm.

Nilipatiwa sehemu ya kuishi lakini pia kulikuwa na wenzangu katika kata ya Makere - Kasulu Kgm.

Jirani yetu kulikuwa na mama fukara haswaa kiuhalisia na watoto wake. Basi mama yule alipata faraja kubwa sana kutokana nasi kuwepo pale.

Nyumba yetu ilikuwa imejitosheleza kwa mahitaji mengi sana. Mama yule Alipoona ana hitaji fulani la kiuchumi au kitu chochote cha kutumia basi alituambia japo kwa hofu kiasi na tulimsaidia. Mara kadhaa alifanya hivyo.

Siku za baadae nilitumia busara moja, kwake yule mama kulikuwa kuna mti wa mlimao basi nilienda kwenye nyumba yake pale jirani yetu na kugonga nikamsalimia na kumuomba malimao mawili na akanipatia, akafurahi sana.

Siku mbili baadae jioni baada ya kutoka kazini japo kwetu kuna ndoo nyingi lakini nilienda kwake kumuomba ndoo ya kuazima na akaniazima akafurahi pia sana. Nilipokuwa nyumbani kwetu na Mfanyakazi Mwenzangu aliniuliza kwa mshangao mkubwa "Mtale Kwanini unamuomba ndoo huyo bi mkubwa na wakati tuna ndoo nyingi ndani?"
Nilimjibu kaka nina busara yangu kufanya hivi.

Basi Matendo yangu hayo mawili yalimfanya yule mama kujisikia fahari zaidi, kuwa huru zaidi kutuomba chochote anachohitaji kwa kuwa aliamini nasi ni wenzake.

Busara yangu ni kwamba Nilifanya vile ili kumuongezea ujasiri yule mama wa kuwa huru zaidi wakati wowote anapokuwa na hitaji lolote basi asisite, asihofu wala asihuzunike kutufahamisha ili nasi kama lipo ndani ya uwezo wetu tumsaidie.
 
Upendo na mwanga vikuongoze..

Kitu kimoja nmekuja kugundua binadamu wote ni kitu kimoja utofauti ni majina tuu tunayoyaitwa, mama huyu na mama aliye nyumbani kwako hawana tofauti.

Nyuzi hizi za Busara huwaga hazina wachangiaji wengi kutokana na hekima wengi hawako nayo.
 
Upendo na mwanga vikuongoze..

Kitu kimoja nmekuja kugundua binadamu wote ni kitu kimoja utofauti ni majina tuu tunayoyaitwa, mama huyu na mama aliye nyumbani kwako hawana tofauti.

Nyuzi hizi za Busara huwaga hazina wachangiaji wengi kutokana na hekima wengi hawako nayo.
Aminaa, Upo sahihi kabisa mkuu. Shukrani sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom