Gang Chomba
JF-Expert Member
- Feb 29, 2008
- 20,610
- 4,782
Katika Mchezo wa Final ya Euro 2000 Italy walipoteza Mchezo baada ya Ufaransa kusawazisha goli Maji ya Jioni na kisha kuja kufunga goli la kifo katika zile dakika 30 za Extra Time.
Hii ilituumiza sana wataliano kiasi kwamba kiungo wetu Mswaki wa jini Demetrio Albertini alilia saana kwa uchungu pale Uwanjani.
Baadhi ya wachezaji wetu Vijana kwa wakari ule walikwenda alipo Kaka yao na kisha kumbembeleza huku wengine wakiwa wanalia.
Kiungo wa Ufaransa na Old Lady Lavecchia Signora kwa wakati huo Zinedine Zidane alikwenda kumpa faraja Brother Albertini lakini alikutana na Kiungo mwenzie aliekuwa akicheza nae Klabu moja Angelo di Livio kisha akatolewa maneno makali yalio ambatana na kufukuzwa eneo hilo.
Simba Dume Baba mwenye Nyumba Paolo Maldini alipo ona hivyo alikwenda kumshika mkono Mkulungwa mmwenzie Albertini kisha akawaambia wachezaji wa Italy kuwa wana deni toka kwa Kaka yao na wanapaswa kulilipa kabla hawajatundika Daruga.
Wachezaji wa Italy wakiongozwa na Sandro Nesta, Canavaro, Gianluca Zambrotta, Conte, Totti, Del Piero, Di Livio, Di Biagio na Tordo kwa kauli moja waliitikia kauli hio na kuanza kumsaka Mfaransa kwa hamu na gamu.
Papatu papatu myuuu hatimae Mwaka 2006 wanajeshi watiifu wa kitaliano wakamkamata Mfaransa iliokuwa ikiongozwa na nahodha Zinedine Yazid Zidane…
Itaendelea…
@acmilanswahili⚫️🔴