Ashura9
JF-Expert Member
- Oct 21, 2012
- 740
- 485
Kisa cha mwanamke wa ziwani – 2
Inaendelea......
USHAHIDI huo maarufu kama Jailhouse Snitch ndio uliopewa uzito zaidi na polisi katika kumtia Gordons hatiani. Walidai kuwa katika kipindi cha siku 14 alizokuwa amewekwa rumande akisubiri kusomewa mashitaka ndipo alipokiri kuhusika na mauaji ya mkewe, Carol Park.
Baada ya timu hiyo kukusanya ushahidi, Novemba 2004, Gordons Park alifikishwa mahakamani kwa mara ya pili na kufunguliwa mashitaka ya kuhusika katika mauaji ya mkewe Carol Park. Wakati wa kuendeshwa kwa kesi hiyo iliyokuwa ikisikilizwa na Jaji McCombe katika Mahakama ya Manchester Crown, ilidaiwa kwamba Park alimpiga mkewe Carol kichwani kwa kitu kizito wakiwa chumbani, Julai, mwaka 1976. Baadaye aliuhifadhi mwili huo kwenye jokofu kabla ya kwenda kuutelekeza katika Ziwa la Caniston, wiki moja baadaye.
Mahakama ilielezwa kwamba wanandoa hao hawakuwa katika uhusiano mzuri kipindi cha maisha yao ya ndoa na walikuwa wakijihusisha na shajara za kubadilishana wanawake, maarufu kama 'wife-swapping parties’ ambapo katika tukio moja la shajara ya chakula cha usiku, Carol Park aliondoka kwenda kulala na rafiki wa mumewe aitwaye Colin Foster, huku Gordons Park akiondoka na mke wa Colin Foster kwenda kulala naye katika chumba kingine.
Lakini hata hivyo, ushahidi wote uliokusanywa dhidi ya Gordons Park ulikuwa na utata mtupu kiasi cha kuwavutia watu wengi, yakiwamo makundi mbalimbali ya watetezi wakipiga kampeni ya kutaka Gordons Park aachiwe huru kutokana na ushahidi finyu dhidi yake. Shahidi mwingine alikuwa ni mama mmoja aitwaye Joan Young, ambaye alidai kuwa Julai 1976 yeye na mumewe wakiwa katika mapumziko wilaya hiyo ya Lake, wakiwa kando ya eneo hilo la Caniston, waliona boti ikiwa ufukweni.
Mama huyo alidai kumuona mwanaume akisukuma kitu kilichofungwa kama furushi, ambapo alimtania mumewe kwa kumwambia yawezekana huyo akawa ni mkewe. Hata hivyo ushahidi huo ulizua utata kwa sababu kwanza, siku na muda ulioelezwa ilitofautiana na ule uliokuwa ukifahamika na polisi.
Pili, ingawa mumewe alikumbuka kusikia ule utani, lakini alikuwa akisoma gazeti hivyo hakuona kitu chochote. Tatu, umbali walipokuwa wamekaa na umbali unaosemekana boti hiyo kuwepo, ni vigumu kwa mtu kuweza kuona kitu na kukitambua.
Nne, kama aliona mtu akisukumia kitu ziwani, basi haiwezekani ukawa ni mwili wa Carol Park kwa sababu mwili ulipatikana umbali mrefu kutoka katika eneo ambalo wao Joan Young na mumewe walikaa. Ikumbukwe kwamba mwili ule ulikuwa umefungwa ndani ya begi la plastiki pamoja na vyuma ili kuupa uzito usiweze kuelea, sasa itawezekana vipi kusogezwa umbali wote ule.
Tano, kwa mujibu wa maelezo yake wakati akifafanua kuhusu muonekano wa boti aliyoiona ufukweni siku hiyo alidai kuwa aliona boti la uvuvi kama Cruiser. Lakini wakati mwili wa Carol ulipopatikana ilifahamika kuwa Gordons Park alikuwa akimiliki Boti kubwa ya uvuvi aina ya Yatch.
Lakini mwaka 1976 Gordon alikuwa akimiliki boti ieandayo kwa kasi ambayo ilikuwa ikitumika kwa uvuvi pia.
Ingawa kumbukumbu hazioneshi usahihi wa madai hayo lakini kuna ukweli kwamba boti hiyo haikuwahi kuwepo katika ufukwe wa Caniston katika kipindi hicho cha mwezi Mei majira ya kiangazi, miezi miwili kabla ya Carol hajatoweka, kwani boti hiyo ilikuwa ikitumika kuvua samaki katika ziwa jingine la Windermere.
Kama ikichukuliwa kuwa ni yeye aliyeutelekeza mwili wa Carol, basi mwili ule usingetelekezwa katika ziwa la Canistone na badala yake mwili ule ungetelekezwa mahali ambapo boti ya Gordons ilipokuwa ambapo ni Windermere, na kama ni kuogopa kuonekana na watu akiwa na mwili ule, basi angeenda maeneo ya mbali zaidi na si Conistone mahali ambako katika kipindi hicho cha kiangazi kunakuwa na watu wengi katika eneo hilo
- See more at: Raia Mwema - Kisa cha mwanamke wa ziwani – 2
kama hukusoma part 1 soma hapa chini:
Raia Mwema - Kisa cha mwanamke wa ziwani – 1
Kisa cha Mwanamke wa ziwani - 3