dawa yenu
JF-Expert Member
- Jan 7, 2014
- 2,825
- 3,674
MENE MENE TEKEL NA PERES, kiganja cha mkono kilionekana kikiandika maneno hayo ukutani. Hiyo ilikuwa ni siku ya karamu kubwa iliyoandaliwa na mfalme wa Babeli aliyeitwa Belshaza ambaye ni mjukuu wa Nebukadreza. Siku hiyo walialikwa wageni wa heshima nao wakala na kunywa wakitumia vikombe vya dhahabu na fedha na mabakuli yaliyochukuliwa katika hekalu la Yehova huko Yerusalemu, hili lilikuwa ni chukizo mbele ya Mungu ndipo katika hali ya kustaajabisha maneno yakaandikwa ukutani MENE MENE TEKEL NA PERES.
Ulikuwa ni ujumbe kutoka kwa Mungu kwenda kwa mfalme Belshaza ila nani atatafsiri maneno hayo? Waliletwa “wachawi” wenye akili lakini hakuna aliyekuwa na ujuzi wa kusoma maandishi yale ukutani. Baada ya tafakuri kubwa ndipo mama wa mfalme akapendekeza aitwe Daniel kwa maana yeye anaijua miungu mitakatifu hivyo ataliweza zoezi hili. Baada ya Daniel kuitwa alitafsiri maneno hayo ya Mungu.
Daniel alisema Yehova alimuondoa Nebukadreza babu ya Belshaza asiwe mfalme kwa kuwa alikuwa na kiburi sana, naye Yehova alimuadhibu Nebukadreza. Belshaza aliyajua yote yaliyompata babu yake ila naye anafuata njia ile ile ya babu yake, amechukua vikombe na mabakuli katika hekalu la Yehova na kuvinywea. Ndiyo sababu Mungu amepeleka mkono uandike maneno hayo MENE MENE TEKEL NA PERES yaani “Mungu amezihesabu siku za ufalme wako na kuzimaliza, umepimwa katika kipimo na kuonekana hufai kitu, ufalme wako wamepewa Wamedi na Waajemi.” Maneno hayo yalitimia siku hiyo hiyo na ufalme wa Belshaza ukafikia hatima yake kutokana na kiburi chake.(Daniel 5:1-31)
Naliona anguko la Chadema kama chama kikuu cha upinzani Tanzania. Ni anguko lililodhahiri kama yale maneno ukutani ila kama ilivyo kwa mfalme Belshaza ndivyo ilivyo kwa Mbowe, ameshindwa kuliona anguko hilo, MENE MENE TEKEL NA PERES. Zaidi ya mikutano na matamko yasiyo na tija sijaona jitihada za wazi za kimkakati za kuifanya Chadema iendelee kuwa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania. Ni kama vile viongozi wa Chadema wanadhani chama chao kina “devine right” hivyo kitaendelea kupendwa na Watanzania katika mazingira yoyote yale, hii si sawa.
Chadema ina wafuasi wengi ulikilinganisha na vyama vingine vya upinzani na kama mazingira ya kisiasa yangekuwa fair huenda kina wafuasi wengi kuliko CCM ila sioni hali hii ikiendelea kutokana na viongozi wa chama kutotaka kubadili mbinu kwa kuzingatia mabadiliko ya kisiasa yaliyotokea Tanzania kwa kipindi hiki cha miaka mitatu. Kwa sasa uwepo wa Chadema unategemea zaidi huruma ya Watanzania ila wakati umekaribia ambapo huruma haitokuwa kigezo bali kitaangaliwa chama chenye nia thabiti, mipango na mikakati yakinifu ya kukiondoa chama cha Mapinduzi. Je Chadema wamejiandaa kwa hili?
Chadema sio chama cha upinzani cha kwanza kuwa na nguvu Tanzania, ilikuwepo NCCR MAGEUZI pia ilikuwepo CUF ila kwa sasa vyama hivi havina mvuto machoni mwa Watanzania walio wengi kwa sababu havikuonyesha nia dhabiti ya kusiamamia kile walichokuwa wakikinena. CHADEMA inalijua hili ila inapuuza kama mfalme Belshaza alivyopuuza yaliyoupata ufalme wa babu yake hadi ufalme wake pia ukaanguka na ali hii itaipata pia CHADEMA ikiwa haitajitathmini na kuchuka hatua stahiki kwa ajili ya kujihakikishia uhai wake.
Ni ajabu sana kuona makamanda wa CHADEMA wanavyobeza nguvu ACT-WAZALENDO kwa Tanzania bara. Wanadhani haina nafasi, nadhani wamesahau hata wao hawakuwa na nafasi mwaka 2005 ila jitihada zao za wazi zimewafikisha hapo walipo leo na ndivyo itakavyokuwa kwa ACT-WAZALENDO. Ni wazi vijana taratibu wameanza kumuamini tena Zitto Kabwe na zile kauli kuwa ni msaliti zimeanza kupungua na wengi wameanza kumuona kama shujaa atakayewafikisha nchi ya ahadi, Mbowe umeliona hili?
Wazungu wanasema, “pride comes before a fall” huu ubezaji wanaoufanya akina Yeriko Nyerere hakika ni mwanzo wa anguko la CHADEMA kama lilivyotokea kwa ufalme wa Belshaza. Makamanda ni lazima waache ego na pride zisizo na tija na waitambue nguvu ya Zitto na ACT na kutazama namna gani watasonga mbele pamoja kwa manufaa ya upinzani wote vinginevyo watagawana kura 2020 na CCM itabaki kuwa kinara. Na endapo hili halitafanyika sioni CHADEMA ikiendelea kuwa chama kikuu cha upinzani baada ya 2020.
Ni wakati wa CHADEMA kuyasoma maandishi ukutani, MENE MENE TEKEL NA PERES.