BigBro
JF-Expert Member
- Jan 9, 2010
- 3,466
- 10,975
Leonor, Princess of Asturias ni binti wa kwanza wa Mfalme wa Hispania, Felipe VI na Malkia Letizia.
Alizaliwa Oktoba 31 mwaka 2005 kwa sasa ana umri wa miaka 18.
Amehitimu chuo na mafunzo kijeshi hivi karibuni na ndie malkia anayefuatia kwa utaratibu wa Ufalme wa Hispania.
Sasa huyu binti anampenda mno mchezaji wa Barcelona, Pablo Martín Páez Gavira maarufu sana kama Gavi aliyezaliwa Agosti 5 mwaka 2004 sasa ana umri wa miaka 19.
Pamoja na kuonesha mapenzi ya dhati kwa Gavi, nyota huyu wa Barcelona hana mpango kabisa na binti huyo. Ingawa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo ndani ya kikosi cha Barca, Gavi wanamuita Prince mdogo.
Sasa kisa cha Gavi kutotaka kutoka kimapenzi na binti hiyo ni kwa sababu, iwapo atataka kumuona Leonor anatakiwa kustaafu soka. Kumbuka ndio kwanza ana umri wa miaka 19.
Kwa mujibu wa sheria, ukioa mtoto wa Mfalme wa Hispania, hutakiwa kufanya kazi nyingine yoyote ya ki- Professional kwani unakuwa unajiandaa kuwa Mfalme ajae.
Hasa ikizingatiwa kwamba, Mfalme wa sasa wa Hispania hana mtoto wa kiume ana mabinti wawili tu.
Hivyo Gavi ameamua kuwekeza Maisha yake katika soka na sio kuwa mfalme ajae wa Hispania.
Mfalme Felipe amejaribu mara kadhaa kumshawishi Gavi amuoe binti yake lakini yeye mpango huo hana kabisa.
Wakati wa kombe la Dunia 2022, Mfalme Felipe ilibidi aende kwenye chumba cha kubadilishia nguo vya kikosi cha Hispania ili kuomba jezi ya Gavi ambayo aliisaini ili ampelekea binti yake, baada ya kushuhudia mchezo wa kwanza wa michuani hiyo kwa nchi yake.
Binti huyo ni shabiki mkubwa mno wa Barcelona ni kwa sababu tu ya Gavi.