Kisa cha maiti ya Anna Fritz na vifo vya wanaume waliombaka

SteveMollel

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
8,797
25,177
Wakati wewe ukienda kuhani msiba unaogopa hata kuaga maiti kwa kuitazama au basi ukiaga unaanza kutusumbua wiki nzima kwamba marehemu anakutokea kwenye kona, basi jua kwa hawa mabwana hali ni tofauti.

Kila mnyonge na mnyonge wake.

Wao hawakuishia kuiona maiti, bali waliisasambua kabisa mpaka kusababisha majanga.

Ilikuwa ni hivi ...

Siku hiyo haikuwa ya kawaida kwa bwana Pau, yeye ni msaidizi wa nesi na daktari na ni kweli alizoea kuona maiti maana mochwari ni eneo lake la kazi, lakini maiti hii inayoingia leo inamshtua.

Ni maiti ya mrembo Anna Fritz!

11010e1d30fdace6d755838e6fd85929.png


Huyu ni mwanamke maarufu lakini pia mrembo anayetambulika nchi nzima.

Kwake hii ni bahati ya mtende. Angelimwonea wapi mwanamke kama huyu enzi za uhai wake? Si bure hata salamu yake asingelipokea.

Anapiga picha mwili wa Anna na kumtumia rafiki yake, Ivan. Muda si mrefu Ivan anawasili hapo mochwari akiwa ameongozana na mwenzie, Javi. Wote wamekuja hapa kwa lengo moja tu, kushuhudia mwili wa mrembo Anna.

Wote wana hamu ya kupoza macho yao na mwili wa mrembo huyu, hata kama hauna pumzi tena. Wahenga husema heri ya nusu shari kuliko shari kamili.

Na tena leo hii wana uwezo wa kuutazama mwili huo vile wanavyojiskia wao, kuanzia kichwani mpaka mabondeni yanapoangukia maji, ushindwe wewe tu.

Bwana Ivan anatumia macho yake kufanya 'ukaguzi rasilimali' kwenye mwili huu na kujikuta anajawa na mate mdomoni. Mate sababu ya uchu. Mate ya tamaa.

84e122e0da3c12085f82c21155ab797b.png


4262a9a5731015a21fc52e9269bb18ce.png

Anashindwa kuvumilia, anamuuliza Pau kama kuna uwezo wa kufanya mapenzi na maiti ile ili walau naye aonje, Pau anamwambia ni sawa ila inabidi atumie mate kama kilainishi.

Pau hii si mara yake ya kwanza. Ashawahi kutembea na maiti hapo kabla hivyo ana kiji-uzoefu ambacho huwezi kuombea kazi wala kujitambia mbele za watu.

Ivan anakwea kwenye kitanda cha maiti, kitanda cha bati baridi lakini yeye hajali. Kibubu kikiwa kimejaa, uwezo wa kufikiri hushuka miguuni. Anafanya mapenzi na maiti ya Anna mpaka alipomaliza haja yake, wakati huo wenzake wakiwa wamempisha kumpa faragha.

6521fd3942863fbadb2ae3ce4eb75fb1.png

Baada ya kumaliza, anamkabidhi kijiti mwenzake, Javi, naye ajikatie kiu kadiri ya uwezo wake lakini Javi anakataa kwasababu ya hofu.

Badala yake, Pau anakwea kwenye kitanda cha bati, anapaka mate 'silaha' yake na kuanza kuonyesha uwezo wa kiuno alichopewa na mama.

b4efb41653ea5bfa235413eaedb5b101.png


La haula! Katikati ya zoezi hili la kutafuta kilele kisichoonekana kwa macho ya nyama, Anna anaamka!

Hawezi kujisogeza mwili.

Anayatumbua macho yake akishangaa mahali alipo na kitu kinachoendelea hapa.

Pau anapiga kelele kwa hofu. Maiti imeamka! Wenzake wawili, Javi na Ivan, wanakuja upesi kutazama. Wote wanastaajabu mwanamke waliyemdhania amekufa, kumbe yu hai kama yule ‘mtetezi’ aliyeimbwa na Christina Shusho.

7c6a73e151c78f6f54e1d6044553449d.png

Sasa wanajikuta katika njia panda. Watoe taarifa kwamba Anna hakufariki ili wakumbane na mashtaka ya ubakaji waliokuwa wanafanya ama wammalize kabisa mwanamke huyu ili kufunika uhalifu wao?

Ivan na Pau hawana uchaguzi mwingine zaidi ya kumuua Anna tu, wao wameshiriki moja kwa moja kuzungusha viuno vyao pande zote kumi na mbili za dunia, sasa watawaeleza nini watu?

Hii maana yake Pau atapoteza kazi, hospitali itafungiwa na wote wawili, pamoja na Ivan, watapelekwa mahakamani kuhukumiwa kwa ubakaji.


Lakini kwa upande wa Javi, hali ni tofauti.

Yeye hataki kushiriki kwenye mauaji haya ya Anna, kumbuka pia hakushirki kwenye kukwea kitanda kile cha raha kilichobeba maiti.

Anachotaka yeye ni kutoa taarifa juu ya Anna kurejea kwenye uhai wake.

Lakini itawezekana vipi?

Wenzake je?

Hapa sasa shetani anaanza kufanya kazi yake... hamna namna, inabidi Javi naye afe!

Sasa ni nani atakayetoka salama katika mochwari hii? ....

Tazama "The Corpse of Anna Fritz".

Screenshot_20240329-160545_1.jpg
 

Attachments

  • b4efb41653ea5bfa235413eaedb5b101.png
    b4efb41653ea5bfa235413eaedb5b101.png
    43.3 KB · Views: 30
KISA CHA KWELI CHA FATHER WA VATICAN NA ROHO ILOTAKA KUANGAMIZA KANISA HUKO SPAIN:


Tofauti na ilivyo kwa makanisa mengine kama vile ya walokole, ndani ya kanisa katoliki kuna utaratibu maalum na watu maalum wanaohusika na zoezi la utoaji wa mapepo katika miili ya waumini.

Zoezi hilo linambatana na kibali rasmi na mrejesho pia kwa wakubwa wako wa kazi.

Mwaka 1986, pasipo kutarajia, Father Gabriele - mtaalamu wa 'dermonology' na 'exorcism' - anateuliwa na papa wa katoliki kuongoza 'exorcism ministry', kitengo kinachoshughulika na zoezi la utoaji wa mapepo na majini katika dayosisi ya Rome, dayosisi inayohudumia makao makuu ya Ukatoliki huko Vatican.
ec622cc9dc65776a259d004f6026bc73.png


Tangu hapo mpaka kifo chake mwaka 2016, father Gabrielle alishughulika na kesi za mapepo takribani alfu sitini kwa ujumla. Kesi zenye visa mbalimbali, visa alivyovinukuu na vikatunzwa katika maktaba za Vatican.
51a6d4f77822e79229641801bdfe1bd0.png


Miongoni mwa visa hivyo ni hiki hapa cha huko Spain. Kisa kilichopelekea kutengeneza movie ya The Pope's Exorcist ...

8bd77577edbcb2b88b5b8d627493387d.png


Iko hivi ..

Familia moja kutoka Marekani inawasili nchini Spain. Mama, binti yake na mtoto wa kiume wapo kwenye gari wakielekea kwenye makazi yao mapya huko mbali na mji.

Baba wa familia hii alifariki kwa ajali. Tangu ajali hiyo, mtoto huyu wa kiume hajapata kuongea neno hata moja mpaka leo hii. Anasumbuliwa na kumbukumbu hiyo mbaya isiyofutika kichwani mwake.

Safari yao inakuja kukomea mbele ya jengo kubwa linalofanyiwa ukarabati na mafundi kadhaa. Jengo hilo lilitelekezwa kitambo sana. Sasa baada ya kifo cha baba, familia imeamua kurudi ili walifanyie matengenezo na kuliuza kwa gharama walau wapate fedha za kujikimu.

Lakini ndani ya kitambo kifupi, kwenye jengo hili la kale, wanabaini humu hawapo wenyewe. Mbali na mafundi walio kazini, kuna kiumbe kingine kinachorandaranda.

ca562f3925765ad4ac26048a6d5b24ff.png

Kuna sauti inanong’oneza kwenye kuta, na kuna jicho linaloangaza kila hatua inayopigwa na watoto hawa wawili.

Kuna kama kivuli kinachozengea jambo, hata mafundi wenyewe wanaogopa kufanya kazi eneo hili. Wana hamu kazi iishe hata leo hii waondoke zao.

Nyakati za usiku, katika korido, fundi mmoja anabaini kuna kitu fulani kwenye ukuta. Anasogeza tofali kuangaza. Anaona kiza tu. Anawasha mwanga aone vema lakini mara analipukiwa na moto usojulikana umetokea wapi!

Tukio hilo linawafanya mafundi waache kazi mara moja na hivyo zoezi la ujenzi linasimama. Gari la wagonjwa linambeba mhanga na kutokomea naye kwenda hospitali.

Mara kidogo mama akiwa haelewi kinachoendelea hapa, anasikia akiitwa na mtoto wake wa kike kule kwenye chumba alalacho mtoto wa kiume, Henry.

Anakimbilia huko upesi, anamkuta Henry kitandani, anahangaika huku na kule, macho ameyafumba. Kidogo Henry anasema neno na kila mtu anastaajabu leo imekuaje?
38f1e9def36af8ce19e098e498df9e79.png


Henry anasema nyie nyote mtakufa kisha anajikwangua na kucha zake usoni bila ya huruma kama mtu aliyechanganyikiwa.

Wanafanya jitihada kumpeleka Henry hospitali kufanyiwa vipimo vya kila aina lakini hamna kitu kinachoonekana, mwishowe anarudishwa nyumbani kwaajili ya uangalizi.

Huko nyumbani Henry anaendelea kuonyesha tabia isiyoeleweka. Anaongea kwa sauti ya ajabu na matendo yake yanamtisha mama na dada yake.
88bc5729561d0480e061ce713399ce9d.png


Ajabu mtoto huyu, yaani Henry, anasihi aletewe mchungaji nyumbani kuja kumkabili.

Kwasababu hii, mama yake ambaye mwanzo alikuwa sio muamini wa mambo ya dini, anaamua kumtafuta padre wa karibu, bwana Esquibel ili amsaidie.

Padri anapoingia chumba cha Henry, wanashangaa anatupiwa mbali kama mzigo. Henry anafoka kuwa padre huyo siye yule anayemtaka.

Hawajui kumbe kiumbe kilichomo ndani ya Henry ni jini kubwa linaloitwa Asmodeus na jini hilo halimtaki mtu mwingine isipokuwa Father Gabriele, padri wa Vatican!

Ana jambo la kumalizana na bwana huyo.
e47cedd655d116382605958f9dcc5fc4.png


Upande wa pili huko Vatican – Italia, papa anamwita father Gabriele na kumwambia kuhusu tukio la mvulana Henry huko Spain.

Anamwambia kesi hiyo ni tofauti na kesi zingine kwani mtoto huyo amemezwa na shetani kwa haraka sana na pia eneo wanaloishi lina historia mbaya sana kwa kanisa katoliki.

Historia ya siri ambayo hata papa hakuielezea.

Sasa papa anamtuma mtumishi huyu kwenda huko Spain. Sio tu akapambane na jini bali pia akaliokoe kanisa....


Tazama 'The Pope's Exorcist'
 
PALE SHETANI ANAPOZENGEA (WHEN EVIL LURKS)

Kisa cha mtoto anayeozea ndani huku mama yake akingojea wataalamu waje kumuua....
e7704b0d92913332832185d193aadcb3.png


Baada ya kusikia kishindo cha risasi karibu na eneo lao la nyumbani, ndugu wawili (Pedro na Jaime) wanabeba silaha kwenda kukagua usalama wa eneo lao.

7d354ac0715cd8f5801acf2fa3f49550.png

Huko maporini wanakuta mwili wa bwana mmoja wasiyemfahamu. Mwili usio na uhai. Mwili huo umebakia nusu na nusu nyingine haijulikani iko wapi!

Wanajiuliza bwana huyu ni nani? Ametokea wapi? Nini kimemuua? Kwa kumtazama, hamna mnyama angemla binadamu kiasi kile!

Wanaokota kitambulisho chake na ramani alokuwa anatumia, sasa wanamfahamu jina lake na alipokuwa anaelekea.

Alikuwa anaelekea kwa mama mmoja huko ng’ambo.

Sasa mabwana hao wanafunga safari kwenda kumpasha habari mama huyo, habari ya kwamba mgeni anayekaa kumngojea basi mzoga wake umelala kule maporini.

Wanafika na kumkuta mama huyo akiwa na kijana wake mdogo, mwanaye mwingine yu ndani. Wanawapasha habari walizokuja nazo na mama huyo anahuzunika kweli kwasababu alikuwa anamngoja mgeni huyo kwa hamu zote aje kumuua mwanaye aliye ndani, jina lake Uriel, ambaye ameoza mwili akiwa hai kwasababu ya nguvu za kishetani!

Anasema mwanaume huyo ni ‘professional cleaner’, mtu maalum mwenye ujuzi wa kukabiliana na watu walomezwa na roho chafu pasipo kuleta madhara kwa binadamu na mifugo iliyo hai.

Mabwana wanashangaa kusikia habari hizi, lakini zaidi wanaenda kushangaa walipoingia ndani kumkuta mtoto huyo aliyeoza.

Chumba chote kimejaa harufu kali. Mwili wake umefura, hautamaniki kwa uchafu. Usaha unamininika puani na mdomoni, kitanda alicholalia kimelowana uchafu tepetepe! Si matapishi si kinyesi.

Wote wanaziba pua zao.

Hawajawahi kuona kitu cha namna hii.

Hiki ni nini?
473a62d87d9d2527c670e43b0335725c.png


Wanamuuliza mama huyu kama ametoa taarifa popote pale, mama anasema anaogopa kutoa taarifa kwani mwenye eneo hili akibaini ana mtoto ambaye mwili wake umegeuka kuwa hekalu la shetani, basi atafukuziwa mbali na yeye hana pa kwenda, ni mjane pia ni fukara wa kutupwa.

Mabwana hawa wanaona kuna haja ya kufanya jambo. Wanaelekea polisi kutoa taarifa lakini ajabu hamna anayesumbuka na kesi hiyo, zaidi wanaishia kugombana na maafisa hao wa usalama wakisema hilo sio tatizo lao.

Sasa wanaenda kuonana na mwenye eneo hili, bwana Ruiz, kumweleza habari hizi za kutisha kuwa si muda mrefu shetani anazaliwa katika eneo lao na kila kitu kitageuka kuwa najisi, ikiwemo mifugo wanayoifuga.

Bwana Ruiz kupata hizi taarifa, anajawa na jazba sana. Anahofia ardhi yake. Anadhamiria kwenda kufanya tukio lakini mkewe mwenye ujauzito anamsihi atumie busara.

Anaongozana na mabwana hawa wawili mpaka kwenye eneo la tukio.

Kufika huko, kwa hasira, anataka kummaliza mtoto mgonjwa kwa kumpiga risasi lakini mama wa mtoto anamsihi sana asitumie njia hiyo.

Mtoto inabidi ashughulikiwe na mtaalam la sivyo shetani alokuwemo ndani yake atafunguliwa na kuanza kumeza nafsi za wengine waliohai.

Bwana Ruiz akishirikiana na mabwana wale wawili wanaubeba mwili wa mtoto mgonjwa. Wanaubeba kwa tabu sana maana ni mzito mno. Unachuruza maji machafu. Wanaupakia kwenye pick-up ya bwana Ruiz waende wakautupie mbali huko nyikani.

Njiani, bado kidogo tu, wamgonge mtoto aliyekua anavuka barabara.

Gari linayumba.

Bwana Ruiz anamudu chombo na safari inaendelea. Kufika mbele, washaacha kilomita za kutosha nyuma yao, wanaona hapa ni sehemu sahihi ya kutupia mwili warejee majumbani.

Kutazama nyuma, mwili haupo!

Kilichobaki ni harufu na maji ya taka.

Mwili umeenda wapi? Hamna anayejua.

Au waliuacha pale gari lilipoyumba kumkwepa yule mtoto barabarani?

Pengine.

Bwana Ruiz anaona isiwe shida, kwani lengo la kuutupa mwili si lishatimia?

Wanajipaki kwenye gari na kila mmoja anarejea kwenye makazi yake wakijua kazi ishakwisha.

Kumbe kazi ndiyo inaanza.

Tena kwa kasi zote.

Baadae bwana Ruiz akiwa ametulia ndani kwake, mara anaitwa na mkewe aje kushuhudia kitu kwenye zizi la mbuzi.

Anapofika mkewe anamwonyesha kwa kidole, tazama mbuzi yule.

Mbuzi yule hayuko kawaida.

a1a24dd36d911c7f2c008c0433eee202.png

Bwana Ruiz anapotazama anabaini ni kweli kuna kitu. Mbuzi huyo tayari ashamezwa na roho ya shetani.

Ananyanyua bunduki yake akitukana. Lengo lake ammalize mbuzi huyo mara moja! Lakini mkewe haachi kumsisitiza, Ruiz Ruiz, usimuue kwa risasi kwani ukifanya hivyo utahamisha roho hiyo kwa kiumbe kingine.
79c0bc329341ea2bd3c5a0f92efeb96e.png


Anamsihi kwa kumshika mkono lakini Ruiz hajali.

Mbuzi mwenyewe anamsogelea Ruiz na kukiweka kichwa chake kwenye mdomo wa bunduki. Ruiz anafyatua risasi na mbuzi anaanguka chini akiwa mzoga!

Kufumba na kufumbua, mke wa Ruiz anachomoa shoka kwenye kuni, kama utani vile, anamfuata mumewe na kumkandika shoka la kichwa. Ruiz anaanguka chini akimwaga damu za kutosha.

Anakufa papo hapo.

Mke huyo naye anaketi na kujishindilia shoka la kichwa. Kwa mikono yake mwenyewe. Shoka tih! Shoka tih! Tih! Kichwani.

Damu zinaruka mpaka kifo chake.
6d60afa6323d142cd3e7dd621e612e8b.png


Asubuhi yake, Mabwana wale wawili; Jaime na Pedro wanakubaliana wakimbie eneo hilo kutafuta mahali salama kwani balaa lishazuka.

Hapa hapakaliki tena.

Jaime anaenda kumpitia mama na Pedro anapitia kwa mke wake wa zamani, Sabrina, ambaye sasa hivi anaishi na bwana mpya (Leornado) ili awachukue watoto wake wawili wakimbie.

Anamwambia Sabrina kilichotokea kule kijijiji. Kuna roho inawafuata kuwaangamiza.

Hata nguo alizotoka nazo huko kijijini anazivua sababu zina mabaki ya yule bwana waloenda kumtupia mbali lakini Sabrina haelewi kabisa na hayuko tayari kutoa watoto.

Swala hili linapelekea mzozano mkali baina yao.

Wakiwa wanazozana, hawana hili wala lile, mbwa mkubwa alokuwamo ndani ya nyumba ambaye mwanzoni alionekana akilambalamba zile nguo alizovua Pedro, anamvamia mtoto wa kike wa bwana Leornado na kutokomea naye huko mtaani!
f2233aaa10bf732a88b58397e9a92f56.png


Bwana Leonardo pamoja na Pedro wanatoka kumkimbiza mbwa huyo ili amwachie mtoto.

Pedro anaonya mbwa asipigwe risasi kwani kutakuza zaidi tatizo lakini anachelewa kwani Leornado anampiga risasi mbwa kwasababu ya kumuua mwanae.

Pedro anakimbia kurudi nyumbani kuwachukuwa wanae akimbie eneo hili, ajabu anamkuta mtoto yule alobebwa na kuuawa na mbwa yuko tayari nyumbani na mama yake, tena yu salama salmin!

Sabrina anafurahia mtoto amerudi salama lakini Pedro anafahamu kabisa kuwa yule si mtoto tena.

Hapotezi muda, anawakusanya watoto wake wawili wa kiume, Santino na Jair, na kuwapakia kwenye gari kisha anaondoka akimwacha Sabrina na mwanae wa kike alorejea kimaajabu.
original_mv8M0PqQYicndU7TGgBAHrI4uUo.png


Mtoto huyo wa kike anamwambia mama yake, gari la baba litakuja na kukugonga. Kama masikhara vile, kufumba na kufumbua, linatokea gari lisipojulikana, linamvamia Sabrina vibaya na kumuua papo hapo!

Dereva wa gari ni nani? Ni yule mume wake wa sasa, yaani bwana Leornado! Kama vile mtoto alivyosema.

Pedro anachanja mbuga bila kugeuka nyuma. Yeye pamoja na wanawe alowanyakua.

Lakini unaweza kuikimbia roho ya umauti kwa kutumia matairi ya gari?

Ni wapi anakimbilia na ingali kina analogusa linafungua milango ya kifo?

Tazama filamu hii ... zima taa, washa tv..
fcc9b89f3c3fd467074a6be41b5b8a98.png
 

Attachments

  • fcc9b89f3c3fd467074a6be41b5b8a98.png
    fcc9b89f3c3fd467074a6be41b5b8a98.png
    328.5 KB · Views: 23
  • 473a62d87d9d2527c670e43b0335725c.png
    473a62d87d9d2527c670e43b0335725c.png
    182.8 KB · Views: 16
Mkuu naomba hii story uhadithie ila ikifika patamu kabla haijaisha basi ikatize isiendelee kama ile nyingine.
 
Back
Top Bottom