Habari zenu wana jamvi,
Nimefikiri namna kompyuta inavyofanya kazi, hasa CPU. Kwa ujuzi wangu mdogo nimeona kuna uwezekano CPU ikaonyesha utofauti fulani kuashiria imetumika sana(imefanya kazi kubwa na kwa muda
mrefu), mf. application kufunguka kwa taabu, au wakati wa kuwaka inachukua muda mrefu(ingawa inaweza sababishwa na hardware pia) n.k.
Nikajaribu kuihusianisha na Ubongo wa binadamu(inasemekana CPU ni kama ubongo wa computer). Binadamu tumetofautiana umri, na mambo tuliyopitia, kuna watu wanafikiri kwa kiwango kikubwa sana(vitu vingi), na wengine wanafikiri kwa kiwango kidogo tu katika kutatua changamoto kulingana na
mfumo wa maisha yao, sasa,Ninataka kufahamu toka kwa "WAJUZI" wa mambo ya ubongo unavyofanya kazi kama kuna uwezekano wa viashiria vinavyoonyesha na kupima kama ubongo wa mtu fulani umefikiri sana kuliko mwingine, yani kama kuna kipimo kuonyesha hii Kichwa(wengine huita Mbongo/ Ndonga) imetumika haswa.
Sababu ya swali hili imechochewa na kuona kuna watu wanasoma sana, wengine kiasi, kuna watu wanapanga mipango mingi hawatoki, lakini mwingine mpango mmoja tu freshi, mwingine ana demu mmoja, mwingine anao hata sita, mtu ana mabiashara mengi, mwingine ana kagenge tu. Sasa hao wote wanafikiri kulingana na majukumu/mfumo wa maisha yao, sasa,
Je utajuaje kama hii KICHWA imefikiri
kwa kiwango kikubwa(kingi) kuliko nyingine.
Wasalaam.